Uongozi dhaifu na siasa za kiuaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uongozi dhaifu na siasa za kiuaji

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mharakati, Oct 10, 2011.

 1. m

  mharakati JF-Expert Member

  #1
  Oct 10, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1,275
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Niliposikia prof Mwandosya amepata leukemia ghafla sikujiuliza sana nikawa namuombea apone haraka..sasa nasikia Dkt Mwakyembe nae ana kila dalili za kua posoined.Hii kama mwananchi ninaetakia tanzania mema inanitia hofu. itakuaje viongozi wawili wapatwe na matatizo ya afya yanayohusu mfumo wa damu, ,(ambayo yanaweza kwa kiasi kikubwa kua induced na sumu katika mfumo wa damu) katika miezi mitatu tukiwa miaka michache tukielekea uchaguzi muhimu kuliko yote hapa tanzania? na wote walikua katika kampeni za 2005, (mwandosya kama mgombea urais na mwakyembe kama leading team member)..kingine je inawezekana wakiungana tena 2015 wakati mwakyembe akiwa anajua mengi zaidi kuhusu Richmond itakua shida kwa kina Lowassa? tunajua mwakyembe na mwandosya walikua viongozi waadilifu at least kwa standard za CCM za siku hizi na walitoka eneo lenye wapiga kura wengi, (mbeya), sasa kama wapinzani wao waliwaona ni hatari je Tanzania tumefika hatua ya kuuana katika siasa? na kama ni hivyo hao wanaotaka madaraka kwa nguvu zote hadi kutumia sumu kwa wapinzani wao wanachotaka ni nini haswa kutoka kwenye tanzania hii?

  Nakumbuka historia ya Africa haya mambo yalitokeaga nchi zilizokua na matatizo ya uongozi, vita, utawala wa kijeshi, utawala wa kiimla wa watu wachache na nyingi ya nchi hizi zimejitahidi kutoka huko kwenye giza kwenda kwenye uwazi na ushindani wa kisiasa usiotumia mbinu za kudhoofisha au kukatiza maisha ya mtu/watu. Sasa sisi ndiyo tunataa kuelekea huko walipotoka wenzetu.

  Siasa ni ushawishi, kujenga hoja na imani, kutoa hongo, kudanganya wananchi na ahadi zisizotekelezeka, kujenga alliance na wenzano ili mshinde, kutengeneza scandal kwa wapinzani wako n.k lakini siyo kuwekeana sumu mtu adhoofike kiafya au kufa...hata kifo cha mwalimu sasa nakiona katika darubini nyingine kabisa namna hii.
   
 2. O

  Omr JF-Expert Member

  #2
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi nashaka sana na CHADEMA, hawa watakuwa ndio wamemwekea sumu.
   
 3. Matango

  Matango JF-Expert Member

  #3
  Oct 10, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 511
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Tunaendelea kujadili hisia.... Kama ni kweli hisia hizo. Unapoua unataka kumuongoza nani ???
   
 4. F

  FUSO JF-Expert Member

  #4
  Oct 10, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,866
  Likes Received: 2,339
  Trophy Points: 280
  no wonder RA akaziita siasa uchwara.......kujiita mpiganaji ndani ya CCM ujue unajitafutia makuu.... ngoja nikapate lunch narudi...
   
 5. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #5
  Oct 10, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  chama chetu cha majambazi sasa kimefikia mwisho.mwaka 2010 mlipigwa mawe mbeya kwa sababu ya siasa zenu za kizushi safari hii mmekuja na siasa za mauaji.
  tafuteni mbeleko ya kuwabebea wanyakyusa.
   
 6. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #6
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kaka umenena, wahakikishe hawa jamaa wawili wanarudi wakiwa wazima, la waisahau Mbeya.
   
 7. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #7
  Oct 10, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nakumbuka alishawataarifu polisi kuhusu njama za kumuua sasa sijajua intelenjensia kama imeshindwa kutulinda au la, lakini hapa inaonesha polisi wameshindwa kuwalinda viongozi na watz kwa ujumla kama itathibitika kalishwa sumu.
   
Loading...