Uongo wa ccm unavyowatafuna

bid2015

JF-Expert Member
Sep 6, 2011
302
55
Mwaka 2009/2010 ccm ilipita vyuo vikuu ikawarubuni wanavyuo ambao ni wanachama wa chama cha mapinduzi ikawadanganya kuwa wajiorodheshe ili wawekwe kwenye database kwa ajili ya kupata kipaumbele wakati wa kupata ajira(KUWARUBUNI).
Kama ilivyo ktk misemo ya Kiswahili hasa huu usemao njia ya mwongo ni fupi au“HUWEZI KUDANGANYA SIKU ZOTE” haukupita muda ukaja uzungushaji wa fomu ya raisi waliopata nafasi hiyo ni watotot wao(WATOTO WA VIGOGO WA CCM) na rafiki zao Mfano RIZ1 na rafiki zake,
Sasa vijana woooooooote wale waliodanganywa na ndugu,rafiki, jamaa na jamii nzima na wasomi wa vyuo vikuu wameuona uongo wa ccm sasa hawaitaki, wanataka rasilimali za taifa lao ziwanufaishe watz woooooote na c wachache ambao ni wateule mfano akina Riz1,January,Nape n.k sasa ccm inatapatapa.
Ni bora ukakaa kimya kuliko kutoa ahadi za uongo zitakazokunufaisha kwa muda mchache na kukupa hasara ya muda mrefu!!!!!!!!!!!
MUNGU IBARIKI TANZANIA na UWAADHIBU WOOOOOTE WANAIANGALIA KWA HUSUDA NCHI YETU nakupenda TANZANIA!!!!!!!!!!!
 

samoramsouth

Senior Member
Jan 16, 2011
190
28
BID umesema, hata UDOM walipitisha fomu yao ILI VIJANA WAJIORODHESHE kuwaweka vijana kwenye data base ili wapate ajira. Niliiitoa hiyo habari hapa jf, MAGAMBA waliidharau, lakini impact yake kwa ccm ni kubwa kwani itachukiwa na hao wote.
 

kidi kudi

JF-Expert Member
May 17, 2011
2,317
1,855
mkubwa samora umena ukweli mtupu,mfano (UDOM) college of education baadhi ya vijana wanaotoka mkoa wa dar walikua wakijiandikisha majina kwa ajili ya kuwasilisha kwa mbunge wao wa jimbo 1 hivi la dar kwa ajili ya kuhakikishiwa nafasi ya kubakishwa mkoa huo! Jamani hivi kama hata hawa wasomi wetu wanadanganywa kiurahisi na wanasiasa hawa nina wasiwasi kuwa tunatengeneza nchi ya wasomi wajinga.. Kwasababu jiulize swali dogo tu,ahadi hiyo kwa wanafunzi hao ambao kwa masikitiko makubwa baadhi yao ni marafiki zangu wakubwa,ni kwa ajili ya wana-udom pekee? Vyuo vingine na wao si wamepewa ahadi kama hiyo na mbunge huyohuyo,je ni kweli wooote hao watapata nafasi za ualimu dar? Au hiyo ofa ni spesho kwa wao wana-udom (kwa vile anawapenda sana)? Nonsense!! Kwa hili kumbe basi tusiwalaumu wazazi wetu maskini+wajinga waliopo vijijini wanaorubuniwa kwa vipande vya khanga na kofia ilhali watoto wao 'wasomi' nao wakigeuzwa majuha kwa staili ileile! Wasomi wetu hawa wamesahau kuwa wizara ndio yenye jukumu la kupanga vituo vya kazi au labda 'wanatufungua macho' kwamba wabunge ndio wapanga post za ajira nchi hii kitu ambacho sikiamini asilani?! Ishu hii ilinisikitisha na itaendelea kunisikitisha unless it proves failure!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom