Kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa Kikwete akijinasibu kuwa CCM ilishinda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa watanzania. Huwa nakereka sana kusikia maneno ya aina hii.
Ukweli ni kwamba CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu Temeke bwana Mtemvu alitengeneza makundi ya jogging mengi na kuwapa majezi, kuwapeleka beach, kuwanunulia pombe, khanga, tisheti, kofia na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima.
Ni upofu wa kiwango cha PhD kuita hizo ni sera nzuri. Nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.