Uongo huu wa Kikwete unakera sana!!

Uongo huu wa Kikwete unakera sana!!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
2,312
Reaction score
3,536
Kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa Kikwete akijinasibu kuwa CCM ilishinda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa watanzania. Huwa nakereka sana kusikia maneno ya aina hii.

Ukweli ni kwamba CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu Temeke bwana Mtemvu alitengeneza makundi ya jogging mengi na kuwapa majezi, kuwapeleka beach, kuwanunulia pombe, khanga, tisheti, kofia na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima.

Ni upofu wa kiwango cha PhD kuita hizo ni sera nzuri. Nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.
 
Huenda hiyo nayo ni tafsiri nyingine ya sera
 
Hawabjamaa wanatumua "Ujinga" wa watanzania kubaki madatakani. Wanahakikisha watz hawapati elimu bora itakayo wafanya wajue ukweli kuhusu utawala wao.

Ndio maana hutumia rasilimali nyingi sana kipindi cha chaguzu kushawishi wale wasio kuwa na rasilimali elimu ili wawachague.

Ona wanavyozuga! Eti kipaumbele chao kwenye elimu ni madawati, hivi tutafika kweli, kama mtu ana mapenzi ya dhati yabkuboresha elimu unaanzaje na Madawati na kuacha walimu!
 
Hapa hapo alipo amefikishwa na SERA nzuri za CCM hadi kufikia kukaa nyuma ya LapTop yake na kuandika na kua Mjanja
 
Kikwete ni mwanasiasa aliekomaa kabisa, wewe unakerwa na yako, au utakuwa team lowassa.
mkuu kila anaetofautiana na kikwete/ccm lazima awe team lowassa.unataka kuuaminisha uma kua nje ya hayo makundi hutuwezi kufikiri?,kwamba nilazima tufikiri ndani ya hayo makundi?.
 
Ule haukuwa ukweli na hali halisi. Ile ni lugha ya kisiasa lakini ukweli ni kuwa mfumo wa UCHAGUZI nchi hii sio mzuri na utaendelea kuifeva CCM

CCM imeng'ang'ania kubaki kuwa chama dola na si chama cha kisiasa. Inawatumia kuanzia watendaji wa KATA, WAKURUGENZI, ma DC na ma RC kupika ushindi haramu.

Pili uwanja wa kufanyia siasa hauko sawa kwa vyama visivyo tawala

Anapodai hawatumii nguvu anadanganya
 
Hapa hapo alipo amefikishwa na SERA nzuri za CCM hadi kufikia kukaa nyuma ya LapTop yake na kuandika na kua Mjanja
Think before you leap. Hata wanaoishi nchi za kidhalimu wanajua kutumia laptop na kusoma.
 
kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa kikwete akijinasibu kua ccm ilishnda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa wtz. ukweli ni kwamba hua nakereka sana kusikia maneno ya aina hii, ukweli ni kwamba ccm imekua ikishnda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu temeke bwana mtemvu alitengeneza makundi ya joggingi mengi na kuwapa majez,kuwapeleka beach,kuwanunulia pombe,khanga,tshet,kofia, na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima ni upofu wa kiwango cha phd kuita hizo ni sera nzuri. nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.
ulichozungumza ni kweli,ni bora anyamaze kuliko kusema uongo waziwazi
 
kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa kikwete akijinasibu kua ccm ilishnda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa wtz. ukweli ni kwamba hua nakereka sana kusikia maneno ya aina hii, ukweli ni kwamba ccm imekua ikishnda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu temeke bwana mtemvu alitengeneza makundi ya joggingi mengi na kuwapa majez,kuwapeleka beach,kuwanunulia pombe,khanga,tshet,kofia, na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima ni upofu wa kiwango cha phd kuita hizo ni sera nzuri. nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.

kuna wakati JK alidokeza "..sio kwa kutumia nguvu, bali kwa sera..." kitu kama hicho nilisikia, kama sikosei. Aliposema hayo alikuwa pia hana furaha sana. ni kama tu alikuwa anajilazimisha kufurahi. ukiangalia Dodoma ilivyo, utapata dokezo. huo wingi wa askari polisi. wengi hawakuelewa wanachosema BAVICHA. kwamba point yao imedhihirika kutokana na kwamba kila hoja za kisiasa zinapojitokeza hapa nchini, CCM hujibu hoja hizo kwa kutumia nguvu, mabavu, Polisi. ingewezekana kabisa kuresolve makinzano ya hoja kule bungeni kwa kutumia mijadala, hoja, maridhiano na makubaliano. lakini waliitwa Polisi wenye silaha. ebo! sasa ni nini maana ya nchi kufuata siasa za vyama vingi? hilo la BAVICHA lisingejitokeza kama kusingekuwa na huo unafiki wa kuzuia vyama vya siasa kufanya kazi zake za kikatiba na kisheria. BAVICHA walifanya move hiyo ili ku-underline unafiki wa kisiasa uliopo hapa nchini sasa hivi. Polisi walipoibuka na kuonesha arsenal yao, kufanya mazoezi ya ulinzi Dodoma ili kuonesha nguvu za jeshi la Polisi, ilikuwa ni kuoenesha upeo wa nguvu za CCM. kwamba CCM sasa haina nguvu za kisiasa, bali ina nguvu za kijeshi tu. hiyo peke yake inaleta kejeli kwa kauli kwamba "CCM haijafa!" kama CCM, chama mahiri cha kisiasa, imeshindwa kujibu hoja za kisiasa kwa siasa, ina uhai gani wa kujivunia? hizo mbwembwe za Dodoma zinashangilia pia nguvu za CCM, ambazo kwa kweli hazipo katika siasa bali ni mabavu tu ya serikali.

Alikuwa ni JK huyu huyu aliyewaasa CCM katika moja ya mikutano mikuu ya hivi karibuni, kwamba wajiepushe kujibu ngumi za kisiasa za vyama vya upinzani, kwa kutumia Polisi. leo ni kilele cha CCM kutegemea nguvu za Polisi, kwamba Polisi watawajibia CCM. aibu iliyoje.
 
Hapa hapo alipo amefikishwa na SERA nzuri za CCM hadi kufikia kukaa nyuma ya LapTop yake na kuandika na kua Mjanja
Think before you leap. Hata wanaoishi nchi za kidhalimu wanajua kutumia laptop na kusoma.
[/QUOTE]

Na mtandao wa kasi unaotumia,na umeme unaochajia simu na laptop kijijini kwako na kale kashule ka kata ulichopitia zote ni miongoni mwa sera anazosema JK. Tujifunze kushukuru
 
Kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa Kikwete akijinasibu kuwa CCM ilishinda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa watanzania. Huwa nakereka sana kusikia maneno ya aina hii.

Ukweli ni kwamba CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu Temeke bwana Mtemvu alitengeneza makundi ya jogging mengi na kuwapa majezi, kuwapeleka beach, kuwanunulia pombe, khanga, tisheti, kofia na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima.

Ni upofu wa kiwango cha PhD kuita hizo ni sera nzuri. Nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.
wanatumia ujinga na umaskini wa watanzania kujipatia maslahi yao ya kisiasa
 
Kama ilivyo ada jana nikamskia mheshmiwa Kikwete akijinasibu kuwa CCM ilishinda uchaguzi kwa sababu ya sera nzuri na zinazoeleweka kwa watanzania. Huwa nakereka sana kusikia maneno ya aina hii.

Ukweli ni kwamba CCM imekuwa ikishinda chaguzi nyingi kama si zote kwa sehemu kubwa kwa kutumia mbinu chafu, huku kwetu Temeke bwana Mtemvu alitengeneza makundi ya jogging mengi na kuwapa majezi, kuwapeleka beach, kuwanunulia pombe, khanga, tisheti, kofia na hali imekua hivyo maeneo mengi sana nchi nzima.

Ni upofu wa kiwango cha PhD kuita hizo ni sera nzuri. Nadhani ifike wakati viongozi wetu wabadilike waseme ukweli ili siasa zetu zibadilike.

ukweli kutoka kwa mwanasiasa? ni sawa na Bikra kwa changudoa!!!
 
Lowasa ameshakubali kuwa alishindwa kihalali kwenye uchaguzi
 
Huo sio ujinga wa viongozi ni uzombi wa wananchi 95% ni misukule
 
CCM Mbele utaongea na kukereka viongoz wako wa ukawa wametulia ww ndo unaumia xawa pole
 
Leo hii mkutano mkuu wa ccm amemsifia Shein kwa kumgalagaza Maalim. I laughed and laughed and laughed- ulaghai mwengine bana. Tumeshuhudia mchana kweupe Shein kuomba msaada wa Jecha baada kuzidiwa.
 
Pesa sio za jk ni mikopo Ambayo wote tutalipa........na michango tunayo Changa Kwenye Mafuta na bill za umeme

Na mtandao wa kasi unaotumia,na umeme unaochajia simu na laptop kijijini kwako na kale kashule ka kata ulichopitia zote ni miongoni mwa sera anazosema JK. Tujifunze kushukuru[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom