Uonevu vijijini utakwisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uonevu vijijini utakwisha lini?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Mar 30, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mwanakijiji,ingawa pia ni mfanyakazi wa serikali.Vijiji vingi vina kasoro nyingi za wazi za kiungozi,kwa kweli there is much to be desired.Kuna uonevu wa wazi wa wananchi.Siku moja katika hali ya kusikitisha nilishuhudia wanakijiji katika kijiji changu cha Dakawa ambao walishindwa kulipa mchango wa mradi wa maji wakifungiwa kwenye darasa la shule ya msingi kwa masaa kadhaa, eti mpaka walipe mchango huo!Wanakiji walio wengi wa kijiji hiki ni maskini wa kutupwa,na kuwaambia walipe Sh.3,500 ni sawa na kuomba jamvi msibani.Tabia hizi zimekuwa za kawaida kabisa katika kijiji hiki,bila hata kujali hali halisi za wanakijiji hawa.Vitisho kwa wanakijiji ni vingi ikiwa pamoja na kutishiwa kwamba watafungwa ikiwa hawakutoa mchango huu au ule,sijui kwa kutumia sheria zipi!Lakini unapochunguza hasa kwanini mambo yanakuwa hivi, unagundua kwamba fujo zote hizo zinafanywa ili kupata fedha kwa ajili ya kushibisha matumbo ya viongozi,na wala sio kwa sababu ya maendeleo ya wanachi.Ninalojua ni kwamba michango yote ni hiari, na wananchi wanatakiwa wahamasishwe katika uchangiaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo yao na sio kulazimishwa.

  Katika hali nyingine isiyokuwa ya kawaida,wanachi waliambiwa waandikishe majina ili hatimaye wapate mbolea ya ruzuku.Wananchi kwa kujua kwamba kwa vile ndugu yangu Waziri wa Kilimo Wasira alikuwa ameongelea swala hili kwa uzito sana,na kwa vile pia alishasema mbinu ya wakati huu ya kutumia coupon itafanikiwa,walijiandikisha kwa wingi, huku wakijua kwa hakika kwamba watapata mbolea.Kilichitokea hata hivyo ni tofauti kabisa.Wanachi walio wengi waliojiandikisha hawakupata mbolea,eti kwa vile wao wana uwezo wa kununua mbolea isiyo ya ruzuku.Sababu hii sio ya kweli kwa vile wapo wengi ambao hawakupata mbolea na hawana uwezo!Sina hakika hata hivyo kama mbolea ya ruzuku ni ya watu wa kipato fulani tu.Cha kushangaza ni kwamba wale waliopata mbolea hiyo walikwenda kuchukua kwa kutumia vyeti vya kupigia kura badala ya coupon tofauti na waziri alivyokuwa ameahidi,hali inayotoa mwanya wa kuweza kuuza mbolea hiyo kinyume cha utaratibu.Kwa ujumla zoezi zima lilikumbwa na mizengwe ambayo inaashiria ufisadi!

  Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba kama kweli ina nia ya kusaidia wakulima wake, ni bora mbolea yote inayotumika nchini ikawa ya ruzuku,hasa kwa vile mbolea yote inayoingizwa nchini inatumika kwa shughuli za uzalishaji wa kilimo,vinginevyo matatizo haya hayatakwisha kabisa.Watu wasio waaminifu watatumia mbinu zozote zile kujinufaisha kwa kutumia mianya iliyopo.Sina shaka kabisa kwamba kama serikali ikijipanga vizuri,uwezo huo inao.Nina hakika matukio ya aina hii na aina nyingine sio isolated kwa Dakawa peke yake,lakini yamesambaa nchi nzima.Ni vema basi serikali ikawa karibu zaidi na wananchi, ili wananchi wasionewe na kukatishwa tamaa katika harakati za kujiletea maendeleo yao.
   
  Last edited: Mar 30, 2009
 2. K

  Kwaminchi Senior Member

  #2
  Mar 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2007
  Messages: 154
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  Mimi nakubaliana nawe kuwa uonevu upo. Na uonevu huu si kwamba upo Dakawa tu au vijijini tu, la hasha. Uonevu wa aina uliyouelezea upo mpaka Jijini Dar na sehemu zote Tanzania.

  Nilikwenda kumtembelea mkwe wangu Jijini Dar. Nikamkuta mwanamama aliyeongozana na gari la kuzoa takataka mitaani akimfokea mkwe wangu na huku kashika kitabu cha risiti mkononi akimtaka amlipe shilingi 1,500 ili takataka zake zizolewe.

  Kadri mkwe wangu alivyokuwa akimwambia hana pesa ndivyo kadri sauti ya yule mwanamama ilivyozidi kwenda juu na ndita kuongezeka kwenye paji lake.
  Uzalendo ukanishinda na ustaarabu ukanitoka, nikaingilia kati kishenzi. Ndipo takataka zikazolewa bila malipo.

  Siku nyingine hapa hapa Dar tena nyumbani kwangu, ingawa nilishalipa bili ya maji na ankara ninayo wakaja watu wa maji wakidai nadaiwa badala ya kufunga mita ya maji, wakakata bomba la mpira unaoleta maji. Pakawa hapatoshi mpaka waliponunua bomba jipya na kunifungulia maji siku hiyo hiyo. Lakini ndio tulikosa maji siku hiyo karibu mchana kutwa.

  Katafute shamba au kiwanja uone serikali ya kijiji itavyokufanya. Si mikutano hiyo na kila mkutano, wewe mwomba shamba au kiwanja utailipia hiyo mikutano mpaka mfuko ukwambie umechoka kutoa fedha. Na mwisho wa yote ukute shamba au kiwanja ulichouziwa ni hewa.

  Mifano ya uonevu na unyanyashaji ipo mingi. Na ikiwa Jijini Dar ndio hivyo, huko vijijini ndio balaa.

  Hiyo ndio serikali ya chama tawala, nambari wani CCM. Chama cha wanyonge na wafanya kazi.

  Wakulaumiwa ni sisi wenyewe kwani tunayataka wenyewe. Ni miaka karibu 50 sasa, lakini hatujifunzi. Tunafurahia kubadilishiwa sura za mvuto. Tunasahau kuwa sahani mpya na safi haibadilishi chakula kilichochacha.
   
 3. Ndamwe

  Ndamwe Senior Member

  #3
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 107
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ndio hao hao watu wa kijijini wanaoshabikia rushwa kwa kupewa wali tu na vikofia wakati wa uchaguzi na kuchagua ccm bila hata kuwa na uchambuzi makini wa uamuzi wa kura zao, wanavuna wanayopanda. ukipanda uharibifu unavuna huo huo. wakati mwingine nasema ngoja waipate labda watapata akili baadae
   
 4. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #4
  Mar 30, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  No,naomba usiwa condemn kiasi hicho.Tatizo lao ni ukosefu wa civic education,nina hakika wakielimishwa vya kutosha wanaweza kubadilika!Ndio maana serikali haitilii mkazo civic education, kwa sababu wanajua wakielimika hawa wamekwisha,vikofia na vifulana hawatataka tena.

   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Mar 30, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Huu ni ujambazi tu. Mengine haya ni kinyume cha katiba, kama kutumia militia kufunga watu kinyume cha sheria.

  Inabidi wanasheria/ wapinzani waivalie njuga hii issue.Hata kama hawana altruism ya kutaka justice, kama wanataka kura hili swala lina kura bwena, mimi nawashangaa wapinzani nchini mwetu hawako creative kabisa.

  Wezi wa EPA walioiba mabilioni wako huru, wakulima maskini ambao GDP zao wengine ni chini ya $ 100 kwa mwaka wanadaiwa 3,500/- na kam hawana wanafungwa na kuteswa!

  Shocking!
   
 6. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #6
  Mar 30, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  sasa maji kama hawalipii wanataka wapewe bure??

  Watz tunapenda sana vya bure kwa kujificha ktk kiwingu cha eti 'mie maskini'!

  Hakuna huduma ya bure! huduma zote zilipiwe!

  Wananchi hao2 hufanya sherehe na ngoma na kutumia maelfu ya pesa! Ila kutoa 3,500 kwa mwaka kulipia maji eti wanasema eti wao ni maskini!
   
 7. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 30, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ndugu yangu Mzalendohalisi, haya maneno yanatoka kinywani mwako. Hivi una ufahamu vizuri umasikini wa mtanzania. Mtu analima mazao yake halafu anakopwa. Ukija katika suala la pembejeo za kilimo, hapa ndio tunapoua kilimo Tanzania, utakuta wengi hawawezi kununua mbolea na dawa, ama wakinunua kuja kurudisha fedha zao inakuwa kazi.

  Unashangaa mtu kushindwa kulipa 3,500, tembea uone, ama uliza utaambiwa. Kuna watu TZ wanakula mlo mmoja, na ni wengi, sio kwamba hawataki kula milo zaidi ni uwezo. Sasa kwa mujibu wa web ya BBC, GNI per capita: US $400 (World Bank, 2007). Hiyo ni kama dola 33 kwa mwezi. Sasa kweli Tsh. 34,000 kwa mwezi mtu asomeshe, alishe, ajitibu na kutibu wenzake, unaweza sema kweli kushindwa kulipa 3,500 kwa mwaka ni jambo la kujitakia?.
   
Loading...