Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

Uoga wa Zitto Kabwe kwa Tulia Ackson

The Tomorrow People

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2013
Posts
2,690
Reaction score
2,853
Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson.

Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge.

Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake.

Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!!

Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson.

Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza.

Suala hapa sio unaibu spika bali ni maslahi ya mifuko ya Zitto Kabwe na hatma ya maisha yake ya kisiasa.
 
scandal ahofie mtu ambaye yuko nje ya mfumo?you are kidding with your cheap propaganda
 
The Tomorrow People

Zitto kajenga hoja yake based on separation of Power kati ya Bunge na serikali wewe unaleta hoja ya ndoa za watu?

Mambo mazito juu ya mustakabali wa taifa letu unataka kuyahamishia kwenye trivialities.Inakuwa matrimonial case?

Baadhi yetu watanzania sijui tukoje.
 
Last edited by a moderator:
Halafu unaposema mifuko ya zitto unazungumzia kitu gani?kama ni pesa usijisahaulishe Mbunge aliyekuwa hachukui posho ya kukaa,
 
Zitto kajenga hoja yake based on separation of Power kati ya Bunge na serikali wewe unaleta hoja ya ndoa za watu?

Mambo mazito juu ya mustakabali wa taifa letu unataka kuyahamishia kwenye trivialities.Inakuwa matrimonial case?

Baadhi yetu watanzania sijui tukoje.

Hatutaki watu wakupiganiwa tunahitaji watu wanaojipigania wenyewe...Mama Mhagama atosha.
 
Jamii ya wanazuoni imekuwa ikijiuliza ni kwanini mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe anampiga vita mgombea unaibu spika Dk.Tulia Ackson.

Wanahoji ni kwanini Zitto Kabwe anamhofia huyu mwanamama wakati ana vigezo vyote vinavyompa "credibility" ya kugombea.Imefikia hatua Zitto anamnadi Mussa Azzan ambaye ni mbunge wa Ccm na kusahau kuwa yeye ni mpinzani ndani na nje ya bunge.

Hapa ndipo dhana ya usaliti kwa Zitto Kabwe inapozidi kumea kwenye masikio ya watanzania.Zitto Kabwe hataki kukubali kuwa siasa ya bunge sio yake peke yake.

Mnakumbuka sakata la aliyekuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ambaye PAC ikiongozwa na Zitto Kabwe iliamuru akamatwe na kuwasilishwa polisi!?Tena kwa makosa ambayo PAC ilikuja kuangukia pua!!

Namzungumzia Andilile Mwainyekule.Huyu ni mume wa ndoa wa Dk.Tulia Ackson.Zitto Kabwe anauona ugumu wa yeye kuiyumbisha serikali kwa skendo za kupika kama kiti kitasimamiwa na Dk.Tulia Ackson.

Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza.

Suala hapa sio unaibu spika bali ni maslahi ya mifuko ya Zitto Kabwe na hatma ya maisha yake ya kisiasa.

Cheap politics
 
Zitto siyo kabisa kwa maslahi ya taifa, mi mwenyewe nilisoma maoni yake hadi nikashangaa sana hoja kama zile kutolewa na zitto, nikajisemea hapa lazima kuna kitu si bure

Kumbe yule mkurugenzi wa TPDC ni mume wa Tulia, haaaa sasa naunganisha dots, ndo maana kumbe Zitto anashikwa na tumbo la kuhara
 
...Zitto Kabwe anahofia Dk.Tulia Ackson kutumia mwanya wa kujua kwa undani sakata la TPDC na kuiokoa serikali na hoja ambazo Zitto Kabwe anategemea kuziibua na kuziendeleza...

Aisee! Kumbe Naibu Spika anatarajiwa kuiokoa serikali bungeni? Kwa nini serikali isijiokoe kwa hoja? Sasa naanza kuungana na ZZK walau kwa jambo hili la barabara ya upatikanaji wa Naibu Spika inavyochongwa na serikali!
 
Tulia nani asiyejua Dr Tulia ni mtoto wa Dada yake Dr Migiro. Mama mdogo akapendekeza apewe unaibu Mwanasheria Mkuu?

JK alimtaka Migiro kuwa Rais na Membe akashindwa wakachukua mrengo wa mbali for their interest ....Kuna nini .....Zitto amejenga hoja Zungu anakubalika na ingekuwa kuongoza ni vyeti Kawawa wasingekuwa mawaziri kina Mtemeke Sanga wangekuwa PM ila kuna hoja ya kumtega JPM asichague PM mchapakazi kisa Nyerere hakufanya hivyo.

Anaitajiii kina Tuliaa Ma God JPM sikiliza sana mwombe Mungu ushauri na Hekima ya Kutawala kwa haki na usawa. Byeeeee
 
huna hoja bali vioja tu, wenye akili tunaona jinsi serikali hii chovu inavyotaka kulitumia bunge kupitisha viroja vyake na kuligeuza bunge kuwa nyumba ndogo ya serikali
 
Ndg mleta mada, unajenga hoja kuwa usaliti wa Zitto unamea masikion kisa kumpinga dr Ackson na kumuunga mkono mr. Zungu, SWALI, vp km angemuunga mkono dr Ackson na kumpinga mr Zungu, bado huo usaliti ungeendelea kuwepo?
Tusiwe wepesi wa kutoa maneno tusiyokuwa na uhakika nayo au pasipo kuyatafakari vema, amani iwe nawe
 
Get your fact correct dude.

Mkurugenzi mkuu wa TPDC ni Dr. James Mataragio.

Huyo Andilile Mwainyekule atakuwa mkurugenzi mkuu wa TPDC ya pichu yako.

Mbona ameandika "aliyekuwa Mkurugenzi wa TPDC........"? Hilo neno "aliyekuwa " hukuliona?
 
Mko kama mlivyo alaah,,,wauliza tena!
 
Back
Top Bottom