Thanks for this initiative.
Hapo ndipo wabongo imeshindikana kabisa kuiga. Tuko radhi kuiga vichupi wazungu wanavyovaa ufukweni nasie twavaa maofisini na wengine hata makanisani na misikitini, na kuacha migongo wazi kumbe wenzetu wazungu wanakuwa commanded na mazingira yao na wala sio kwa kutaka. SI unaona mtu avaa vipande vitatu vya suti na tai kali DSM ndani ya daladala?
Nchi nyingine za wazungu wamejenga maeneo rasmi ambako mama akitaka kunyonyesha anaenda kulw anawakuta wenzake wananyonyesha pia. Lakini ukifumwa unanyonyesha hadharani unayo kesi ya kujibu.
Sasa wabongo kwa kuwa kuona nyonyo ni dawa ya akili, especially kama nyonyo yenyewe ikiwa bado haijambo, ni ruksa tu kuanika hadharani hata kwa kisingizio cha kunyonyesha. Nchi nyingine ziwa waruhusiwa kuliona lakini chuchu marufuku mpaka kibali maalum cha mwenye chuchu. Wahindi tumbo ni ruksa kuliona, linaanikwa peupeee, mali ya serikali. Wabantu tatizo lao liko kwenye makalio na mapaja, ndio maana dawa za kuongeza makalio zinakuja kirahisi kwetu na tena mashindano ya Miss Bantu yapo ambayo sifa mojawapo ni nyonyo kubwa na makalio makubwa.
Sasa Kama tunadhani sio vibaya leo kunyonyesha hadharani, basi Halmashauri zijenge majumba ambako kina mama wataenda kunyonyeshea. Sie wengine tumekulia katika mtindo wa mambo hadharani, sio sambi. Kwa kuwa tumeona wazungu wanasema sambi ndio nasi tuanze wimbo wa sambi?
Tuache hayo, watu wanapiga kelele ati nguo fupi zinawashawishi, kwani walazimishwa kuangalia? Mtoto anapolia anatulizwa kwa nyonyo. Sasa wataka aendelee kulia na tiba ingalipo? Wengine kina mama sio tu hawataki kunyonyesha hadharani, bali hawataki kabisa kunyonyesha eti kwa sababu yatarefuka na wao watapoteza mvuto, kwani wameshaona kwamba wanaume wa kiafrika akili yao iko kwenye vifua mviringo. Sasa wameanza na makalio kuyavimbisha, hata wengine wanavimba kalio moja na lingine nusunusu, wanahangaika mahospitalini sasa.
We want natural beauty, nothing less, nothing more. Nyonyesha basi ili mwanangu akilia atulie nami roho yangu ifarijike. Taabu ni kwamba tunatangulia kuzeeka akili kabla ya mwili.
Ibra