Unyenyekevu kwenye ndoa


Mimi ni mwanamke lkni ninapingana na baadhi ya wanawake wanaotaka haki sawa na mwanaume.najua kuna baadhi ya wanawake humu wataniponda lkni ukweli ndo huo.hata maumbile yetu yako tofauti pamoja na wanaume..haki sawa ni ndoto za mchana kweupeeeeee[emoji109][emoji114]
 
Big up.
 
Wanaume wengi neno "Samahani"halipo katika vocabulary zao.
 
Naomba kuyafahamu hayo majukumu......
 
Haki sawa ni muhimu...tatizo watu hawaelewi ni katika nini. Kusema haki sawa hakumaanishi mwanamke ampande kichwani mmewe, kwa kuwa hata mwanaume hatakiwi kumfanyia ubabe wa kijinga mkewe. Katika mengi haki sawa ni mwanamke apewe nafasi ya kuongea na kusikilizwa (mf. Kutoa ushauri) kumiliki mali na ardhi, kupata elimu na kujoendeleza, kufanya kazi au biashara ( halali) nk. So kama mtaishi kwa maelewano hakuna atakaeona anakosewa haki ktk vitu vidogo..haki sawa sio kupika, kudeki, kuosha vyombo, kukaa baa nk. Tuwafundishe binti zetu wajielewe na sio kujinyenyekeza huku unanung'unika...aaah ngachoka..
 
Mmebaki wachache sana wenye busara kama zako. Mnafaa kuwekewa ulinzi kama wa Faru J, maana mko hatarini kutoweka.
 
Mwanaume mpende mkeo,na mwanamke mtii mumeo!!
Haya yakienda sambamba lazima ndoa iwe na tabasamu kila siku!!

Wanawake wengi siku hizi tunapenda kuchukua nafasi ya mume kama kichwa cha nyumba kitu ambacho hakitokaa kiwezekane,haijalishi mke umemzidi kifedha au cheo mumewe lazima kichwa cha nyumba ni mume wako tu.
Embu mpe nafasi mume wako aone una muheshimu then mambo yatanyooka tu.

Lakini pia wanaume wengine wanajisahau sana,akishaona mwanamke anamsikiliza kwenye kila kitu basi anamuona boya.
Asanteni.
 
Namuomba Mungu anijaalie mke mwerevu. Na nikimpata hata kesho namuoa Inshaallah.
 
Wanaume wengi neno "Samahani"halipo katika vocabulary zao.
Whatever,.. Samahani yapaswa kutoka pande zote mbili umekosewa hatoi samahani something has to be done upone rohoni... Mtu samahani adimu kwako yet unaongoza kwa maudhi SMH..
 
Hivi hii haki sawa mnayoiimba mnaielewa ni katika nini?
 
Reactions: BAK
Afadhali umedadavua, maana watu wamekazana na haki sawa hata bila kuelewa misingi ya hiyo hakisawa wanayoiongelea.
 
Umenifurahisha sana Mkuu. Nimeupenda huu mchango wako. Heri ya mwaka Mpya Mkuu.

 
Wanaume wengi neno "Samahani"halipo katika vocabulary zao.
Na hapo ndipo tatizo linapokuja, suala la unyenyekevu lapaswa kuwa la pande zote, sio kiburi na kujiona ndio unadeserve kunyenyekewa tu.
Wote hatujakamilika, basi pale unapogundua umemkosea mwenzako basi nyenyekea na omba msamaha, neno samahani ni dogo lakini lenye uzito sana.

Ila msamaha wenyewe uwe umemaanisha, sio kila siku warudia kitu hicho hicho alafu utegemee mambo yawe sawa na unyenyekewe tu.
 
Halafu hawa wanaume hawa hawa ambao wako radhi kuwanyanyasa wake zao hivi, hawako tayari kuona mabinti zao wananyanyaswa kama wao wanavyowanyanyasa mama zao. Huwa nashindwa kuwaelewa kabisa. Iweje wewe uone ni sawa kumnyanyasa mkeo kwa kila namna na vipigo asivyostahili juu lakini hutaki binti yako atendewe kama unamvyomtendea mkeo! Mkuki kwa nguruwe.....

Afadhali umedadavua, maana watu wamekazana na haki sawa hata bila kuelewa misingi ya hiyo hakisawa wanayoiongelea.
 
Ndio hapo unisaidie kushangaa!!
Kuna boya mmoja alidai wanawake ni wa kuchapa tu na kusepa huku nae ana mtoto wa kike, nikamwambia karma is a biatch, hata bintio atafanyiwa hivyo hivyo, weeeeh alikuwa mkaliiii.

Usichopenda bintiyo,dada yako afanyiwe basi usimfanyie binti au dada wa mwingine, and vice versa.
 
mume agombezwi, mume afokewi, mume afanyiwi kiburi wala jeuri, akinuna na wewe unanuna mpendwa utaipoteza ndoa yako
Nahisi wewe hujawahi kukutana na mwanaume kisirani wasioona hata jema moja kwa wake zao.

Anyway..hapo kwenye red,hivi wanawake peke yao ndio wenye jukumu la kulinda ndoa?
 
Nahisi wewe hujawahi kukutana na mwanaume kisirani wasioona hata jema moja kwa wake zao.

Anyway..hapo kwenye red,hivi wanawake peke yao ndio wenye jukumu la kulinda ndoa?
Umesahau mama kuolewa ni kamsaada kwa mwanamke, hivyo ni jukumu lake kuhakikisha anabaki humo!
Ndio maana lawama zote kwa wanawake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…