Unyang'anyi Mahakama Ya Mwanzo Buguruni

Unyang'anyi Mahakama Ya Mwanzo Buguruni

Myfancyface

JF-Expert Member
Joined
Dec 23, 2016
Posts
948
Reaction score
900
Katika hali ya kushangaza nimekutana na mjane mmoja ambaye kanisimulia juu ya dhuluma na udhalimu anaotendewa na so called "wasimamia sheria". Huyu mama ana kesi ya madai ambapo mshitakiwa amekiri kosa. Cha kushangaza yametengenezwa mazingira ya rushwa kiasi kwamba mdaiwa amekuwa ndio rafiki wa makarani, askari na hakimu. Sijui sheria ila nimemshauri amuandikie mwanasheria mkuu wa serikali aombe kesi ihamie mahakama ya wilaya. Kama kuna ushauri mwingine au uzoefu karibu kwa maoni.
 
Nadhani ungezungumza kwa undani kuhusu sakata hilo, ili wanaojua/ wanasheria wamshauri muhusika....ingependeza zaidi.
 
Nadhani ungezungumza kwa undani kuhusu sakata hilo, ili wanaojua/ wanasheria wamshauri muhusika....ingependeza zaidi.
Ni kwamba huyu mama anamdai mtu milioni kadhaa. Ndugu wa mtuhumiwa walifika mahakamani mapema na kupanga mikakati na watu wa mahakama. Mojawapo ni kumfundisha mtuhumiwa jinsi ya kujibu. Lakini mbele ya hakimu, mshatakiwa akakiri kosa. Cha kushangaza hakimu akaahirisha kesi. Ili iweje?!! Maskini mjane huyu.
 
Mheshimiwa Luhwago hebu fuatilia hii kitu mie nilikuwa na kesi ya kubambikiwa na tajiri yangu mwarabu pale buguruni wakanifunga kifungo cha nje miezi sita. Nilipokata rufaa uliisimamia vizuri na kwa haki nikashinda. Naomba umsaidie huyu mama pliz mnyalukolo.
 
Ahsante sana mkuu.
 
Ndivyo mahakama nyingi nchini rushwa 7na uonevu ni kama kawaida. Hata ujaribuś5 vipi wanakuwa hivyo umesema ka kikundi kukumaliza.

Nashangaa kwanini hawatoi namba itakayoaminika na wananchi au hata anuani ya e-mail ili wanaoonewa waripoti kinachowatokea.

Ingependeza zaidi hiyo hata kuwa chini ya ofisi ya Mh. Majaliwa au Rais kabisa.
 
Back
Top Bottom