Nadhani kila aliyeona hii picha ameshtushwa na unyama huo. Lakini, binadamu tuna tatizo la kusahau haraka. Hivi kweli, hakuna kati yetu aliyeona hiyo picha ambaye yuko kwenye kamchezo hako ka kipumbavu??
Weye mwanamke, unayekubali kudanganywa ati usiogope, mi ni mkubwa fulani akikupiga tu nitamfunga, nasema weye ni Pum.bafuu kabisa. Huyo aliye lala hapo chini naye aliambiwa ka weye. Sasa huyo mtenda hata akifungwa miaka 100 huyo mama hapo atafaidi kitu??
Weye mwanaume uliyeona hilo, hebu mhurumie huyo mke wa mtu unayemdanganya, unamweka hatarini saa yeyote, aweza kuwa kama huyu. Je utapata faida gani akifanywa hivyo? Hata akipona, weye utakubali kumchukua kwako na mikovu mikubwa hivyo?
Nawasihi ndg mlioona hizo picha, badilikeni. Mke wa mtu SUMU. Na weye mleta thread, unatufanya tumchukie aliyetenda unyama huu. Kwani alirukwa na akili au ni baada ya kuvumilia nakuonya sana lakini mtendwa akawa kichwa ngumu?? Siutetei unyama lakini tusaidie kuupunguza unyama usitokee. Mstahili mwenzako, do not cheat by all means. Tutapona