SoC03 Unyago wa Dar es Salaam ni wetu

Stories of Change - 2023 Competition

web developer

New Member
Feb 21, 2017
3
1
Kutoka kijiji kidogo cha wavuvi kwa umaarufu Mzizima mpaka kuwa Jiji kuu na kitovu cha biashara nchini Tanzania ni safari ndefu sana kwa Dar es salaam, Jiji lenye eneo na km za mraba 1800 na wakazi zaidi ya milioni tano.

Changamoto kubwa kwa jiji hili ni msongamano wa magari na makazi kwa baadhi ya maeneo. Niwapongeze viongozi wa jiji hili na wa nchi kwa jitihada zao kubwa za kutatua changamoto ya msongamano, mfano; wanaboresha barabara kila mwaka, wamejenga barabara za juu katika baazi maeneo ya makutano ya barabara, wamejenga madaraja mfano la kigamboni, wameboresha miundombinu ya reli na kuanzisha safari za treni, pia wamejenga barabara za mwendokasi na bado wanazidi kuzijenga, hongereni kwa uongozi bora na wenye uwajibikaji unao onekana.

Ukiachia mbali uongozi bora na wenye uwajibikaji unao unekana katika jitihada za kuhakikisha wananchi tunaendesha shughuli zetu za kiuchumi kwa ufanisi bado tatizo la msongamano lipo na lenye athari nyingi.
Ifuatayo ni mifano ya athari za msongamano wa makazi na magari Dar es salaam:-​
  1. Chuki baina ya wananchi au wananchi na askari wa usalama pia chuki baina ya wananchi na serikali. ambapo baadhi ya chuki hupelekea watu kupigana au kusababisha vurugu.​
  2. Uchafu, idadi inavyokuwa kubwa ya watu na vyombo vya moto pia uzalishaji taka nao unakua ni mkubwa na ili hali eneo lenyewe ni dogo.​
  3. Huaribifu, kuna baadhi ya muda vyombo vya usafiri ulazimika kupita pasipo ruhusiwa na kufanya huaribifu, watu pia ujenga maeneo ambayo hayaruhusiwi.​
  4. Chanzo cha magonjwa, tabu ya msongamano huleta magonjwa ya akili yanayosababishwa na msongo wa mawazo na yale ya mlipuko.​
  5. Hasara kwa taifa, Taifa kila mwaka upoteza zaidi ya trilioni moja kutokana na foleni za magari jijini Dar es salaam.​
Hasara tajwa hapo juu zitakuwa zinazidi kila mwaka ikiwa viongozi wa jiji na wa nchi hawata wajibika ipasavyo, na mpaka tulipo fika ni kutokana na kawaida ya viongozi wetu kufikiria kutatua jambo kwa malengo ya muda mfupi, sio hivyo tu aya yanayofika katika kutatua changamoto hizi ni kwa sababu nchi hatuwajibiki kuwekeza katika elimu ya teknolojia.

Uongozi wetu unabidi utuamini watanzania na utujali tupate elimu bora na si elimu isiyo na manufaa kwa taifa, kama wananci tungepewa elimu bora viongozi msingekuwa na haja ya kuhitaji wakandarasi kutoka nje kuja kutujengea miradi mikubwa ikiwemo miundombinu ya barabara na reli, gharama pia ingekuwa ni nafuu kama nchi itatushughulisha sisi wenyewe wazawa.

Lakini lawama hizo zote mhusika mkuu wa kuzibeba ni wizara ya elimu, kwani wizara hii ikiamua nchi iendelee kwa kasi basi itaendelea na ikiamua nchi iendelee kwa mwendo wataratibu basi itakua hivyo, kwani wao ndio injini kuu ya nchi.

Nawapongeza kwa jitihada wanazo zifanya lakini bado wanahitajika kuwajibika kwa kiwango kikubwa kwani wakumbuke tupo katika vita kubwa ya uchumi na wanabidi watambue chochote wanachofanya wanabidi wakipime kama kinamanufaa kwa nchi na manufaa kwa watu wengi.

Zifuatazo ni hatua ambazo serikali wanatikiwa kuzifanya ili kutatua tatizo la Msongamano Dar es salaam:-
  1. Wizara ya elimu, ipeleke vijana wanaosoma sayansi nje ya nchi wakapate elimu ya teknolojia ya treni za umeme au sumaku na zinazopita chini ya ardhi, lakini kabla hawajaenda wapewe mafunzo ya jeshi ya mwaka mmoja ili kuwajengea uzalendo wa nchi yetu katika akili zao na mioyo yao.
  2. Wasomi wakirudi nchini kwa msaada wa serikali wajenge viwanda vya kuzalisha vifaa vya kisasa kwa ajiri ya ujenzi wa treni za umeme zitakazopita chini ya ardhi.
  3. Wasomi hao wachore ramani za ujenzi wa reli zitakazopita chini ya ardhi kuzunguka ndani ya jiji na ziende mpaka nje ya jiji. Mfano, reli toka Mkuranga Pwani kupitia Vikindu mpaka Stesheni au Posta Dar es salaam, reli toka Mlandizi mpaka Posta Dar es salaam, na reli toka Bagamoyo mpaka Posta Dar es salaam.
  4. Wafanye ujenzi wa njia na watengeneze treni kwa ajili ya misafara.
Ujenzi wa usafiri wa treni za umeme au sumaku chini ya ardhi utakuwa na faida zifuatazo kwenye kutatua foleni za magari na msongamano wa makazi Dar es salaam:-
  1. Zitabeba watu wengi kwa pamoja, kwa hiyo tabia za kupigana vikumbo na kugombania kuingia ndani ya usafiri zitaisha au kupungua kwa kiasi kikubwa.
  2. Abiria watapata sehemu za kukaa, kwa hiyo wazee, mama wajawazito, watoto na wagonjwa hawata taabika tena.
  3. Tiketi zitakatwa za kisasa, yaani ule usumbufu wa makonda hautakuwepo.
  4. Mwendo wa treni utakuwa ni wa kasi, kwa hiyo watu watafika kwa haraka zaidi maeneo mbalimbali ya jiji hali itayopelekea uchumi upae kwa kiwango kikubwa.
  5. Uwakika wa kuagiza na kupata bidhaa kwa bei nafuu.
  6. Uwepo wa kamera utapelekea, Usalama wa watu na mali zao kuwa ni mkubwa.
  7. Kupanga chumba au kupanga nyumba au kujenga nyumba Dar es salaam itakuwa sio lazima tena, watu wataishi nje ya Dar es salaam na watakuwa na uwakika wa safari ya haraka ya kufika jijini na kuendelea na shughuli zao na uwakika wa kurudi nyumbani kwa wakati hali itakayo punguza msongamano wa makazi ndani ya Dar es salaam.
  8. Watu watapata muda wa kupumzika na kuziangalia familia zao yaani ndoa zitadumu na upendo utaongezeka kwa sababu hofu ya kuchelewa popote itakuwa imeondoka.
  9. Usafiri huu utadumu miaka mingi sana, vizazi na vizazi kwa hivyo serikali itakuwa inavuna faida tu, maumivu na gharama za mradi itakuwa ni stori tu.
  10. Usumbufu juu ya ardhi ya Dar es salaam utakuwa umepungua kwa kiasi kikubwa sana.
Ikifika hatua hiyo tatasema uongozi umewaza kuona mbali na tutauita ni uongozi ulio bora kwa manufaa ya wengi.

Tukumbuke Tanzania itajengwa kwa ubora na uzalendo zaidi na sisi wenyewe na kwa gharama nafuu zaidi, basi kila mmoja wetu anatakiwa awajibike kwa nafasi yake ili nchi yetu iweze kuendelea kwani mali tunazo ila kuvuna na kutumia ndio mtihani.

Dar es salaam ndio kitovu cha biashara basi serikali iwe na malengo ya muda mrefu na ya kuondoa tatizo kabisa.

Ili tuone raha na raza ya ngoma ya unyago tuingie wanjani kutimua vumbi wenyewe, tusiishie kuwatolea macho .
 
Back
Top Bottom