Tetesi: ununuzi wa umma Mh Rais TRC/PPRA

Tetesi: ununuzi wa umma Mh Rais TRC/PPRA

charles RMD

Member
Joined
Aug 6, 2008
Posts
18
Reaction score
13
Jana wakati wa hotuma ya Mh Rais uapisho wa viongozo mbali mbali kuna sehemu kuhusu maelekezo ya Mh Rais kuhusu matumizi ys sheria za PPRA uachwe,
Ushauri wangu kwa jopo la washauri wake wangemsaidia kuhakikisha anasisitiza matumizi ya sheria za umma na kuwepo na uharaka katika utekerezaji.
Sheria tulizo nazo zina maeneo mbali mbali .....ya utekerezaji na eneo la emergency procurement iko .
VEMA HILI LIONWE KWA JICHO LA PEKEE...
NAWEKA NUKUU YA SERA MH Makamu wa Rais kwa Niaba ya Mh RAIS,

Eneo la ununuzi wa umma ni moja kati ya maeneo yenye matumizi makubwa ya bajeti ya Serikali. Eneo hilo linalohusisha matumizi katika upatikanaji wa bidhaa, kandarasi za ujenzi na huduma, linakadiriwa kuwa na matumizi yanayozidi asilimia 70 ya bajeti ya Serikali. Matumizi hayo makubwa, yanakabiliwa na changamoto nyingi. Changamoto hizo, zimesababisha kuwapo kwa matumizi ya rasilimali za nchi yasiyo na tija. Katika kipindi cha mwaka 1965 hadi mwaka 2000 ununuzi wa umma ulikuwa ukitekelezwa kwa kufuata mwongozo uliorithiwa kutoka kwa Serikali ya Wakoloni wa Kiingereza uliojulikana kama “Financial Orders Part III, 5th Edition” ya mwaka 1965. Mwongozo huo uliotumika kwa takribani miaka thelathini na mitano, ulionesha upungufu mkubwa wa kiutekelezaji kutokana na kutoendana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kitekinolojia, n.k yaliyokuwa yametokea ulimwenguni katika kipindi chote hicho.

Ili kuendana na mabadiliko hayo, Serikali iliona haja ya kuboresha utekelezaji wa shughuli za ununuzi na ugavi kwa kutunga Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 3 ya Mwaka 2001. Mwaka 2004, Serikali iliifanyia marekebisho Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 3 ya Mwaka 2001 baada ya kubaini upungufu mkubwa katika utekelezaji wa sheria hiyo. Marekebisho hayo, yalipelekea kutungwa kwa Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 21 ya Mwaka 2004. Sheria hii, ilizipa mamlaka taasisi nunuzi kufanya maamuzi yote ya ununuzi kupitia bodi zao za zabuni. Ili kuboresha utendaji katika sekta ya ununuzi, Serikali kupitia sheria hiyo, ilianzisha mamlaka za usimamizi wa utekelezaji wa ununuzi na ushughulikiwaji wa malalamiko ya wazabuni.

Mwaka 2011, Serikali iliifuta Sheria ya Ununuzi wa Umma Na. 21 ya Mwaka 2004 kwa kutunga sheria mpya ya Ununuzi wa Umma Na. 7 ya Mwaka 2011. Sababu kuu za kutunga sheria hiyo zilikuwa; kuzipa nguvu zaidi za utekelezaji mamlaka za usimamizi wa ununuzi wa umma, kuweka utaratibu wa ununuzi wa vifaa vilivyotumika, kuweka utaratibu wa ununuzi wa bidhaa na huduma mtambuka, kuweka utaratibu wa ununuzi wa dharura, kuweka utaratibu wa ununuzi kwa njia ya kielektroniki, kupunguza urefu wa michakato ya ununuzi, kuongeza viwango vya adhabu kwa wakiukaji wa sheria ya ununuzi, n.k. Pamoja na mabadiliko hayo, utekelezaji wa Sheria ya Ununuzi wa Umma No.7 ya Mwaka 2011 nao umekutana na changamoto mbalimbali. Baadhi ya changamoto hizo ni; ukubwa wa gharama za uendeshaji wa michakato ya ununuzi, ukubwa wa bei za bidhaa na huduma zinazonunuliwa na taasisi za umma, urefu wa muda wa michakato ya zabuni, kiwango kidogo cha uadilifu, n.k. v Kufuatia changamoto hizo Serikali iliamua kuifanyia marekebisho kwa kuipitisha Sheria ya Ununuzi wa Umma Na.5 ya Mwaka 2016 kama ilivyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Juni 2016.

Pamoja na jitihada hizo za Serikali, utekelezaji wa shughuli za ununuzi umeonesha upungufu unaotokana na kukosekana kwa miongozo mahsusi ya kisera. Upungufu huo, umekuwa ni chanzo cha mabadiliko ya mara kwa mara ya Sheria ya Ununuzi wa Umma na umejitokeza katika maeneo mbalimbali kama; matumizi ya TEHAMA katika ununuzi, usimamizi wa mikataba, migongano ya kimaslahi, ushirikishwaji wa makundi maalum ya kijamii, ukuzaji wa viwanda vya ndani na matumizi ya rasilimaliwatu na malighafi za ndani, n.k. Hali hii, inaonesha umuhimu wa kuandaliwa kwa miongozo ya kisera kupitia Sera ya Taifa ya Ununuzi wa Umma. Sera hii itaiimarisha sekta ya ununuzi na kuongeza mchango katika kuleta maendeleo ya Taifa. Mwisho, ninapenda kuwashukuru wadau walioshiriki kufanikisha ukamilishwaji wa Sera hii. Dkt. Philip I. Mpango (Mb) Waziri wa Fedha na Mipango
 
Back
Top Bottom