Ununuzi wa ndege za Boeing: Serikali iwe wazi vinginevyo sijui...

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,695
149,921
Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia na mashaka ya aina hii yataendelea kujitokeza kila siku.

----
Patriote said,
Kuna taarifa mitandaoni kuwa ndege tajwa hapo juu ambayo tanzania ineshajicommit kuinunua inaweza kununulika kwa bei ya chini tofauti na ilivyoeleza. Katika taarifa ya ununuzi wa ndege hiyo, Tulielezwa kuwa ndege tunayonunua ina thamani ya USD 224.6 Mil sawa na TZS (482.89bn/-) kulingana na rate ya dollar ya wakati huo wakati Serikali inaseal deal na Boeing.

Ukiangalia kwenye mtandao wa Boeing (Boeing: 787 Dreamliner to become part of Air Tanzania fleet). Hela tunayolipia kunnua ndege hiyo haipo wazi sana mana imesema Tanzania inanunua ndege hiyo ambayo thamani yake kwenye price lists za Boeing inaonyesha ni USD 224.6 Mil. It says "Boeing and the United Republic of Tanzania have confirmed an order for one 787-8 Dreamliner, valued at $224.6 million at list prices".

Naimani watu wa Boeing wanajua sana English, sijaelewa kwanini wameshindwa kuelezea bayana kabisa kuwa Tanzania imenunua ndege hiyo kwa bei fulani. Ieleweke pia kuoneshwa kwa bei fulani kwenye pricelist ya supplier haimaanishi ndio final proce utayonunulia bidhaa hiyo mana kwenye biashara kuna kuburgain/kuombe upewe discount. Na kwenye ununuzi wa kitu kama ndege ndio kuna mambo mengi zaidi mana unaweza hata kuicustomize ndege unatotaka kununua ikawa tofauti na nyingine kwa either kuwa more luxurious or kuwa more economic/basic au ukaburgain kununua bei iliyododa kwa bei rahisi kama walivyofanya wenzetu.

Wakati hali ikiwa hivyo toka Boeing's website, taarifa nyingine zinaeleza kuwa Kampuni hiyo ilikuwa ina ndege aina hiyo hiyo Boeing 787-8 Dreamliner ambazo zilikuwa zimedoda (Zilikosa wanunuzi kwa miaka kadhaa kutokana na kuwa nzito zaidi ya kawaida). Ndege hizo zilizododa zinatambulika kama "Terrible Teens" na kwenye pricelists ya Boeing hao hao inaonyesha ni around USD 224. Mil, ila kwa kuwa zimedoda taarifa kutoka vyanzo vingine zinasema kuwa ndege hizo zinauzwa kwa nusu bei yaani around USD 115 Mil. Nchi ya Ethiopia ni moja kati ya wateja waliokwisha kununua "Terrible Teens" kwa bei ya punguzo (half price). "Ethiopian Airlines is in advanced discussions to buy eight of the early-build 787s (Terrible Teens), said four people who asked not to be identified because they weren’t authorized to speak publicly".

Vilevile, taarifa zaidi zinasema kuwa Boeing inakiri kupata mteja atayenunua Terrible teen iliyobakia ila inakataa kuweka wazi taarifa na jina la mteja wa mwisho anayeinunua hiyo terrible teen ilobakia. Ilichofanya Boeing iliweka information za wadau wawili kuwa ndio watanunua hiyo ndege moja ilobakia.( http://www.bizjournals.com/seattle/...-orders-a-new-boeing-787-8-dreamliner-to.html).

Kulingana na maelezo yangu hapo juu maswali yafuatayo yanahitaji majibu.

1. Tanzania imeweka order ya kununua ndege aina ya Boeing 787-8 Dreamliner . Je ndege tunayonunua ni moja kati ya Terrible Teens???

2. Kama tunanunua Boeing 787-8 Dreamliner ambayo ni moja kati ya Terrible Teens, Je tunanunua kwa USD ngapi??? Kwa taarifa zilizopo tumeambiwa thamani ya ndege hiyo ni USD 224.6 Mil. Nimepekua maeneo mengi haipowazi kwa kweli kama tutatoa hiyo hela kama ilivyo kwenye pricelist au na sisi tutanunua kwa bei ya punguzo au lah?? Hapa wabunge tunaomba mtueleze budget iliyotengwa kununua hii ndege ni USD ngapi

3. Kama tunanunu moja kati ya Terrible Teens, kwanini tumechagua kufufua shirika letu la ndege kwa kutumia ndege ambazo zimekuwa challenged na mashirika ya ndege yenye uzoefu mkubwa na yenye wataalam waliobobea wa kuassess ubora wa ndege?? Yaani motivation yetu ni nini katika kununua moja kati ya Terrible Teens?

4. Kwanini Shirika la Boeing limeshindwa kuweka wazi details za mteja anayenunua Terrible teen iliyobakia??? Je kuna connection kati ya kutoweka wazi jina la mteja huyo na Order ya Tanzania?? Ikumbukwe kwamba Boeing liliingiza order details za unidentied buyer katika kipindi hicho hicho ambacho wameingia mkataba wa Ununuzi na Tanzania. Check hii site (Magufuli holds talks with top Boeing official)

Toa maoni yako kulingana na hii mada. Unaweza kujiridhisha kwa kusoma taarifa kwenye mitandao mbalimbali mana hizi ndege zimeleta mijadala sana katika anga za kimataifa.
 
Dada yetu Mange kule Instagram kaja na mapya juu ya ununuzi wa Boeing 787-8 Dreamliner.Anaetaka kujua kaandika nini aende huko akajione mwenyewe

Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia.
Jaribuni kufanya research haki kidogo kabla ya kulalamika kwani mnaishushia JF hadhi. Hizo ndege anazodai ziliuzwa/zinauzwa bei ndogo mna uhakika gani ndizo Tanzania imenunua? Hizo ndege ni version za mwanzoni za Dream liner ambazo zilifanyiwa modification ili zikidhi viwango. Baada ya kufanyiwa modification zikaongezeka uzito hivyo kukosa uwezo wa kuruka masafa yaliyokusudiwa wakati wa ku-design dream-liner hivyo zikapunguzwa bei kidogo. Zilikuwa chache kama 10 au 12 sina uhakika. Cha muhimu (KABLA YA KULALAMIKA) ni kujua kama Tanzania imenunua hii version au imenunua version ya kawaida!
 
Jamani huyu Mange nae asitushike akili kama vile kila anachobandika unakuwa kama msitari kutoka kwenye biblia! Ndege dreamliner kama ilivyo haina tatizo, ni ndege ya kisasa sana, state of the art; hayo aliyoandika Mange sijayasoma na sitayasoma kwa sababu huwa simuoni kama mwandishi "Objective"; kama yanahoji mikataba na kusigana na sheria za manunuzi au uwezo wetu kuiendesha kibiashara ndege hiyo na kwa faida, labda ana hoja; vinginevyo ni maneno ya Mange yale yale tu ya Udaku na agenda za self promotion!
 
Jaribuni kufanya research haki kidogo kabla ya kulalamika kwani mnaishushia JF hadhi. Hizo ndege anazodai ziliuzwa/zinauzwa bei ndogo mna uhakika gani ndizo Tanzania imenunua? Hizo ndege ni version za mwanzoni za Dream liner ambazo zilifanyiwa modification ili zikidhi viwango. Baada ya kufanyiwa modification zikaongezeka uzito hivyo kukosa uwezo wa kuruka masafa yaliyokusudiwa wakati wa ku-design dream-liner hivyo zikapunguzwa bei kidogo. Zilikuwa chache kama 10 au 12 sina uhakika. Cha muhimu (KABLA YA KULALAMIKA) ni kujua kama Tanzania imenunua hii version au imenunua version ya kawaida!
Ndio maana nikasema uwazi ni muhimu maana kama unachosema ni kweli na kinajulikana haya tusingeyasikia.

Kwanini hamshauriki?
 
Nimeisoma na nimemuelewa binti Kimambi.. nime Google nimeona hicho anachoongelea kuna chembe chembe za ukweli..Ngoja niwasiliane na Mbunge wa jimbo langu ili akaulize hili swala Bungeni..Inawezekana huyu MTU na kijana wake Bashite na vile visafari vya America wanatuibia hawa
 
Dada yetu Mange kule Instagram kaja na mapya juu ya ununuzi wa Boeing 787-8 Dreamliner.Anaetaka kujua kaandika nini aende huko akajione mwenyewe.

Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia na mashaka ya aina hii yataendelea kujitokeza kila siku.
Kipi Mange alichofanikisha katika serikali hii? Alianza na Makamba taahira wewe na wenzio wa chadema mkalivalia njuga mkiamini Mh Magufuli atamtumbua, ikashindikana. Ikaja maneno ya kusu mama Janet kuugua ghafla. Nayo ukayabeba kama zuzu. Kawaona mafurushi sasa kaingia kwa Paul Makonda nayo umeshupaa kiasi hata kushindwa kuihudumia familia yako. Jana mange alikuonesha mali za Makonda. Ulivyojuha unaziamini alizozitaja mange kuliko zilizopo tume ya maadili. Leo kakupa ununuzi wa ndege nawe unamuamini kuliko atakavyosema CAG. Kweli mmeo kapata hasara huyo.
 
Acha frustrations za kjinga utakufa siku si zako.

Mange kawashika pabaya.

Mtanyooka tu.
 
Dada yetu Mange kule Instagram kaja na mapya juu ya ununuzi wa Boeing 787-8 Dreamliner.Anaetaka kujua kaandika nini aende huko akajione mwenyewe.

Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia na mashaka ya aina hii yataendelea kujitokeza kila siku.

NIMEIPENDA HII YA DADA KWANI INATUSAIDIA CHADEMA KUPATA WAFUASI..TUTAHAKIKIASHA ANASEMA UWONGO ILI WANANCHI WATUAMINI CHADEMA VIZURI TU
 
photostudio_1491726175403.png

ukisoma maelezo hayo hapo unaina kabisa kuna kitu hakipo sawa
 
Dada yetu Mange kule Instagram kaja na mapya juu ya ununuzi wa Boeing 787-8 Dreamliner.Anaetaka kujua kaandika nini aende huko akajione mwenyewe.

Mimi sijui ukweli uko wapi ila yote haya pengine ni matokeo ya kukosekana kwa uwazi katika huu ununuzi wa hizi ndege.

Naishauri serikali ianze kulishirikisha Bunge katika baadhi ya mipango yake inayohusu manunuzi vinginevyo ya Richmond yanaweza kujirudia na mashaka ya aina hii yataendelea kujitokeza kila siku.

Hataki kusikia ushauri wa mtu yeyeto kwa kuwa hamkumsaidia kwenda kuchukua fomu ya kugombea,iko siku hizo ndege zitafungiwa uwanja wa chato na kuwa Mali ktk himaya ya mfalme wa chato ndipo mtajua ana PhD questionable
 
Kipi Mange alichofanikisha katika serikali hii? Alianza na Makamba taahira wewe na wenzio wa chadema mkalivalia njuga mkiamini Mh Magufuli atamtumbua, ikashindikana. Ikaja maneno ya kusu mama Janet kuugua ghafla. Nayo ukayabeba kama zuzu. Kawaona mafurushi sasa kaingia kwa Paul Makonda nayo umeshupaa kiasi hata kushindwa kuihudumia familia yako. Jana mange alikuonesha mali za Makonda. Ulivyojuha unaziamini alizozitaja mange kuliko zilizopo tume ya maadili. Leo kakupa ununuzi wa ndege nawe unamuamini kuliko atakavyosema CAG. Kweli mmeo kapata hasara huyo.
Nasema hv MANGE CHAPA KAZIIIIIIIIII.
Tandika mikwaju tu mpk wajinyee.
 
Back
Top Bottom