Wang Shu
JF-Expert Member
- Feb 1, 2014
- 2,573
- 3,758
Mwaka 2015 nilikuwa na rafiki yangu tukifanya kazi kwa ushirikiano mkubwa sana alinizidi umri kama miaka 10 tulikuwa marafiki wa ukweli, alibahatika kuwa na mke ambae alinisimulia jinsi alivyompata story fulani hivi inavutia sana.
Alikuwa ananiambia changamoto za mke wake ni nyingi sana, lakini kiini cha changamoto zote hizo ni kutokusoma, mke wake aliishia darasa la pili hii ikamfanya asijue kusoma wala kuandika.
Siku moja alinisimulia kwa masikitiko na kwa aibu yaliyomtokea baada ya kwenda naye Zahanati kupima ujauzito maana walihisi ni dalili za mimba, walionana na daktari akachukua maelezo yao kisha akampatia mwanamke vichupa 2 vidogo(container) kwa ajili ya kwenda kutia mkojo na haja kubwa ili upimaji ufanyike.
Alinambia alimwonyesha choo cha Zahanati akawa anamsubili kwenye foleni na wagonjwa wengine, chakushangaza mkewe aliingia sehemu iliyo andika MEN/WANAUME badala WOMEN/WANAWAKE.
Watu wote walishangaa walianza kucheka Zahanati nzima, kule chooni alikoingia kuna wanaume pia aliwakuta jamaa yangu alikuwa amechelewa kujua tukio alilofanya mkewe alivyojua tafrani tayari imezuka si unajua tena watanzania kwa kuchamba, aliniambia alienda fasta chooni kumchukua mkewe na kumtoa nje anakuta watu wananyooshea kidole yeye na kumsema ovyo "kusoma hujui hata picha huoni".
Ikabidi amwambie aingie upande wa pili wa choo, mke wake alikaa kama dk 30 hajatoka alivyotoka kwenye zile chupa mbili hakuna kitu hata tone la mkojo, alivyo muuliza akajibu alishindwa jinsi ya kuweka haja kubwa na mkojo kwa sababu chupa ni ndogo kuliko mkojo na haja kubwa atawekaje? jamaa alichoka alikasirika sana alimfokea mke wake mbele za watu.
Alipomwambia jinsi ya kufanya mwanamke alijibu kwa wakati huo hana tena mkojo wala haja kwa sababu tayari ameshajisaidia.
Iliwalazimu wasubiri masaa kadhaa mpaka mkewe abanwe na mkojo tena ili wakapime angalau mimba tu.
Anasema aliona aibu sana iyo siku...
Ushawai kuwa kwenye mahusiano na mpenzi asiyejua kusoma na kuandika?