Mapendekezo yangu nui:
1. Wabunge wa viti maalumu wawe maalumu kweli, wawe watu waioweza kusimama kwenye majukwaa na kuomba kura, na kuomba kura na watoke ma makundi maalumu kama Albino, Viwete, Vilema n.k si kama sasa ambapo ni nafasi za wanawake mabilionea na wenye ushawishi wa kisiasa na kiuchumi. Mfano, Getrude Lwakatare.
2. Kuwe na mahakama maalumu ya Uhujumu uchumi, ambayo itashughulikia makosa yote ya kifisadi, viongozi kujimilikisha mali n.k. Mahakama hiyo ipewe mamlaka kamili, ikiwamo kufilisi mali zilizopatikana visivyo, kutoa hukumu ya kifungo cha maisha n.k
3. Ielekeze vipaumbele vya Taifa, ikiwano kilimo n.k. Kila chama kitakachochukua madaraka lazima kifuate vipaumbele hivyo.
4. Iweke wazi aina na mfumo wa uchumi na seriklali. Pamoja na jinsi watu wa hali ya chini watakavyopunguziwa mzigo wa kodi.
5. Itenge siasa na biashara. Mfano, kama kionozi ni mmiliki wa kampuni fulani asiwe kwenye tume au kamati inayohusiana na kazi za kampuni yake.
6. Viongozi wa Bunge (Spika, Katibu n.k), na serikali kama Waziri Mkuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, n.k wasitokane na Wabunge au chama chochote cha siasa. Wawe waajiriwa.
7. Kuwe na mfumo wa wazi unaoeleza mishahara pamoja na malipo yoyote yale kwa watumishi wa serikali (watumishi na viongozi wote).
8. Kiongozi au mtumishi yeyote yule wa umma aliyeshindwa kutimiza majukumu yake asipate tena nafasi ya kutumikia Taifa.
9. Tume huru ya uchaguzi, tume ambayo haitokani na ushawishi wowote wa kisiasa.
10. Ieleze mikakati ya kulinda na kusaidia sekta binafsi. Sekta binafsi ndiyo ingine ya uchumi kwa mataifa yaliyoendelea.
11. Na kadhalika....