Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,559
- 41,075
Upatikanaji wa katiba mpya ni utaratibu wa kisheria, na mchakato mzima ni lazima uwe wa kisheria. Process nzima, kuanzia vikao mpaka ushirikishwaji ni lazima viwe vya kisheria.
Vikao vya mchakato wa katiba siyo vikao vya kitchen party ambapo mnakutana tu mnamchagua mwenyekiti; au binti anayeolewa au mzazi wake anatamka tu kuwa fulani utakuwa mwenyekiti wa vikao vya kitchen party.
Tumesikia kuwa Jaji Mutungi, mtu ambaye hana kabisa credibility ya neutrality hata kwenye nafasi yake ya sasa, ambapo mara nyingi ametumika kama kibaraka wa wanasiasa kuhujumu vyama vya upinzani, eti ameitisha kikao cha kuanzisha mchakato wa kupata katiba mpya. Mambo ya kujiuliza:
1) Ni sheria gani inampa mamlaka msajili wa vyama vya siasa kusimamia upatikanaj wa katiba mpya?
2) Ni sifa zipi na zimetamkwa na sheria ipi za mtu kuwa kiongozi wa mchakato wa katiba mpya? Na hizo sifa Mutungi anazo?
3) Mutungi ni kiongozi wa vyama vya saisa, ana mamlaka yapi anayoweza kuzialika taasisi na asasi ambazo hazipo chini ya ofisi ya msajili wa vyama vya siasa kushiriki vikao vinavyohusiana na upatikanaji wa katiba mpya?
4) Zipi ni hadidu za rejea ambazo Mutungi amepewa katika kuhakikisha katiba mpya yenye maslahi kwa umma wa Watanzania inapatikana? Hizo hadidu za rejea nani aliziandaa, na nani alizipitisha?
5) Kwenye taarifa iliyotolewa na Mutungi ni kwamba vyama vya siasa, kila kimoja eti kitawachagua watu watakaoshiriki kwenye mchakato wa katiba. Huu ni upuuzi wa hali ya juu. Mjumbe au mtaalam aliyeteuliwa na chama fulani kuingia kwenye hiyo kamati ya katiba, kwa vile ameteuliwa na chama fulani, kwa vyovyote vile ataingia huko akiwa na fikra kuwa anatakiwa kwenda kulinda maslahi ya hicho chama kilichomteua. Hali hiyo, itageuza vikao vya katiba kuwa vikao vya kugombea maslahi ya vyama vyao. Na je, wasipokubaliana, kutatokea nini? Nani atakuwa mwamuzi wa mwisho? Chama chenye wanachama 1,000 na 1,000,0000 vitakuwa na wawakilishi sawa? Hawa wanaenda kuandaa katiba ya vyama vya siasa au katiba ya nchi?
6) Mutungi anasema eti hiyo kamati itakayoundwa na wawakilishi wa vyama vya siasa itaandaa mapendekezo. Swali: Mapendekezo yanapelekwa kwa nani? Na huyo atakayetoa uamuzi wa mwisho juu ya mapendekezo, amepewa na nani hayo mamlaka? Asipoyakubali mapendekezo yote, kutatokea nini?
Wananchi tupinge matumuzi ya hovyo ya pesa yetu kupitia mgongo wa uandaaji wa katiba. Katiba ya nchi haitengenezwi kama katiba ya vikoba. Process nzima inatakiwa kuwa ya kisheria na jumuishi.
Katiba ya mpya ya nchi siyo ya Mh. Rais Samia, siyo ya Mutungi, siyo ya CHADEMA, siyo ya CCM, wala siyo ya ACT au kakikundi fulani ka watu. Ni aheri ijulikane kuwa hatuna katiba mpya kuliko kuletewa riwaya fulani iliyoandaliwa na kakikundi ka watu, halafu tukapewa tu kuwa hii ndiyo katiba ya nchi.
Katiba inatakiwa kuwa jumuishi. Zitafutwe asasi zote zilizo rasmi na zisizo rasmi. Hata JF inatakiwa kuwakilishwa maana ni kundi kubwa la watu. Kinachotafutwa ni ushirikishwaji mpana. Makundi ya wakulima, wafanyabiashara, wafanyakazi, vyama vya siasa na wanasiasa, vyama vya kitaaluma, makundi ya wastaafu, watetezi wa haki za binadamu, uwakilishi wa kimaeneo na kikanda,taasisi za elimu, n.k. kama ni suala la gharama, kila kundi linaweza kujigharamia lenyewe kwenye usafiri, malazi na chakula. Serikali ishughulikie ukumbi na uchapaji wa nyaraka mbalimbali. Lakini kama watu watajitegemea kwa gharama, kusiwepo hata mmoja, hata kama ni Waziri, atakayetumia pesa ya umma kwaajili ya vikao vya katiba mpya.
Kumpa Mutungi usimamizi wa jambo hili inaonekana hatupo serious, tunataka kupoteza muda na rasilimali nyingine.
Mapendekezo ya Tume ya Jaji Warioba ndiyo mapendekezo pekee yaliyojumuisha watu weng kutoka maeneo yote ya nchi, na yaliyofanyiwa uchambuzi mkubwa kitaalam. Hapo ndipo mahali pekee sahihi pa kuanzia kama kuna dhamira njema ya kuipata katiba mpya nzuri inayotokana na matakwa ya wananchi, na siyo hii ya sasa inayotakiwa kutengenezwa na akina Mutungi.
Majina huumba, tusisahau ule msemo maarufu kuwa SIRI YA MTUNGI INAIJUA KATA. Tujiukize kuna siri gani juu ya jambo hili, hata mpaka usimamizi wa jambo hili muhimu sana kwa Taifa letu, kwa kizazi cha sasa na baadaye, anapewa Mtungi, mtu ambaye iwe ni kwa sheria au hata katiba iliyopo, au kupima uadilifu wa mhusika katika utendaji wake wa kazi kwa majukumu aliyo nayo sasa, kwa vyovyote vile hakustahili.