Ungependa kitu gani kiwemo kwenye katiba mpya? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungependa kitu gani kiwemo kwenye katiba mpya?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by binti ashura, Apr 16, 2012.

 1. b

  binti ashura Senior Member

  #1
  Apr 16, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 120
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  ndugu zangu ni muhimu sana wote tushiriki katika uandaaji wa katiba mpya! itakuwa jambo la muhimu sana iwapo kila mwananchi mwenye ufahamu atoe mchango wake wa mawazo ili katiba itakayoundwa isiwe na vilakavilaka. mie ningependekeza hata kama wewe unanafasi fulani serikalini changia mawazo kama vile wewe hupo kwenye nafasi fulani jifanye kama ni raia wa kawaida. mfano wewe waweza kuwa mbunge unapochangia futa mawazo ya kuwa wewe ni mbunge.
  naomba kuwakilisha!
   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Napenda katiba iweke wazi mfomo wa serikali tatu. Hii ni kusema kwamba ningependa kuwe na serikali ya Tanganyika, Serikali ya Zanzibari iliyopo sasa na Serikali ya Muungano.
   
 3. k

  kula kulala Member

  #3
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi ningependa na sisi watanganyika tukawa na serekali yetu bedera yetu bunge letu maana tumeshachoka na kelele za wazanzibar na matusi yao kila siku
   
 4. Lavie

  Lavie Member

  #4
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Ningependa katiba mpya iwemo Tume huru ya uchaguzi ambayo haiwajibiki kwa rais aliyeko madarakani wala chama chochote cha siasa.
   
 5. Mwana Mpotevu

  Mwana Mpotevu Platinum Member

  #5
  Apr 16, 2012
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 3,294
  Likes Received: 333
  Trophy Points: 180
  umetumwa na Warioba ama ndio unaomba u-katibu myika kwake??
   
 6. M

  Mnyama Hatari JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2012
  Joined: Apr 10, 2012
  Messages: 335
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mimi ningependa katiba mpya iwe na kipengele kinacholazimisha kuweka wazi mishahara ya viongozi wote wa juu wa serikali kuanzia raisi, makama wake, raisi wa Zanzibar, waziri mkuu, mkuu wa majeshi ya ulinzia na usalama, polisi, magereza, mgambo, JKT, majaji wote, na kadhalika.
   
 7. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #7
  Apr 18, 2012
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,436
  Likes Received: 1,017
  Trophy Points: 280
  Katiba mpya ningependa isifanane kabisa na katiba iliyoposasa kwa maana muundo mzima wa katiba ya sasa ni ya kindharia na maisha ya kusadikika zaidi. Katiba mpya iwe muongozo wa kuelekea katika mazingira ya kuleta maendeleo, umoja na mshikamano.

  Ujamaa na kujitegemea haupo kabisa na hatua ya juu kabisa kufikia katika maendele na si rahisi kufikia for the next 50 yrs therefore hata kama ni sera ya CCM usionekane tena katika kaiba mpya. Mfumo mzima wa kiutawala na kiutendaji upo katika kutumikia watawala na viongozi. Kama binadamu wote ni sawa basi katiba iendembali zaidi katika kuainisha usawa, Raisi asipite kwa ving'ora na apange foleni kama kalumanzila isipokuwa kwa lazima sana kama anakwenda shamba lazima ajue ni muda gani muafaka na si for inconvinience ya wengine.

  JESHI la Polisi ni la kulivunja kabisa na polisi wawe watumishi wa umma vyovyote vile wasiwe kwa ajili ya kutumikia viongozi bali wawatumikie walipa kodi wa nchi hii ambao ni wananchi maskini watumiaji wa bidhaa zinazozalishwa na viwanda.

  TRA iwajibike kwa walipa kodi na tafsiri ya walipa kodi itafsiriwe upya isiwe mwenye TIN au VAT number, kipaumbele kiwe kwa who bear the tax burden sio madalali wa kukusanya kodi. walipa kodi wakubwa na wadogo wapate respect sawa.

  Secta binafsi ndio engine ya maendeleo, kila kipengele katika katiba kitoe msisitizo kwa fursa kwa wafanya biashara wadogo na wazawa ili wakue na next 50yrs tuwe na mabilionea wazawa. Ilivyo sasa ni kinyume kabisa na hata uteuzi wa Raisi uzingatie nyanja zote za umma sio lazima wawe watumishi wa serikali na recycling ya watu walioshindwa kuleta maendeleo na wastaafu. Vijana, NGO na sector binafsi iwe na nafasi katika teuzi mbali mbali za raisi.

  Rushwa iongezewe hukumu na mla rushwa anyongwe na kesi mahakamani zisiwe zinakawia. Katiba mpya iendane na sera, miongozo mipya ili kuharakisha utekelezaji, kazi za kuchaguliwa ziwe na ukomo ubunge mwisho 2 terms.

  Nasisitiza, unafiki wa kutunga sheria zisizotekelezeka ukome kabisa kwa mfano, sheria za kuboresha biashara zipo ila polisi, sumatra na wengine wanakuwepo kuweka vikwazo na kufungua mianya ya rushwa. Mamlaka za udhibiti, zisigeuke kuwa polisi na mahakimu.

  Polisi jeshi, usalama wa Taifa na jeshi viwe mbali saana na kushiriki uchaguzi na kukibeba chama tawala. sheria mpya iwe na vipengele vya kuwatafuta, kuwaandalia mashtaka wale wote walioua viwanda, mashirika ya umma na mabenki na kurudisha nyumba zote za serikali.

  Kuchunguza upya utajiri wa wahindi, waarabu na waswahili kuonyesha wamepataje utajiri
   
 8. nkawa

  nkawa Senior Member

  #8
  Apr 18, 2012
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 181
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Katiba mpya ionyeshe wazi nafasi sawa kwa wanawake na wanaume katika nyanja zote, kumiliki mali, ardhi, elimu na uongozi.
  Wananchi wote wanapata sehemu ya ardhi iwe kwa wanaoweza kununua na hata waasio na uwezo wagawiwe sehemu ardhi kupitia serikali za vijij.
   
 9. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #9
  Apr 18, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,952
  Likes Received: 1,824
  Trophy Points: 280
  hili nalo la muhimu binafsi ningependa katiba iangalie watumisha wa umma hasa wale wanaotoa huduma. pia ingepunguza nafasi za wateule wa rais wengine wasiwepo manake hakuna sababu ya kuwa na mkuu wa wilaya na tukawa na mkurugenzi wa halmashauri.
   
 10. Kiraka

  Kiraka JF-Expert Member

  #10
  Apr 18, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 2,551
  Likes Received: 613
  Trophy Points: 280
  Wakurugenzi wa mikoa/wilaya na Mawaziri au makatibu wakuu wa wizaraziwe nafasi za kuajiriwa kwa kuomba kazi na sio kuteuliwa.
  Raisi azuiwe kujianzishia mikoa na wilaya , majimbo kama vile kwenda chooni.

  Hii sina uhakika kama ni issue ya kikatiba au vipi, Mifuko yote ya pension kama vile NSSF, PPF na the likes ilazimishwe kuwapa mikopo wafanyakazi wenye mafao yao huko kwa riba nafuu.

  Kodi kwa wafanyakazi haswa wa sector binafsi ipunguzwe kama wenzao wa serikalini, iweje wao wabaguliwe?

  nk.....ntaendelea...
   
 11. Maalim Jumar

  Maalim Jumar JF-Expert Member

  #11
  Apr 18, 2012
  Joined: Dec 28, 2010
  Messages: 1,443
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  katiba mpya sijaelewa...
  Ikiwa zile acts huwa hazipingani na katiba...ina maana nazo zitapitiwa upya?
  -kuhusu mtoa na mpokea rushwa...napendekeza afungwe mlaji si mtoaji.
  Mtoaji hua analazimishwa atoe...hivyo si mkosaji. Na akitoa kwa kua mpokeaji ndie atafungwa...itabidi akatae!
   
 12. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #12
  Apr 19, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimependa wana JF wanavyojadili jinsi ya wananchi kuwawajibisha wabunge hata kabla ya chaguzi kuu. Hivyo napendekeza kuwepo na kipengele cha wabunge kuwajibishwa na wanachi wa jimbo husika pale wanapoona wanasua sua katika kuleta maendeleo.

  1. Kuwe na kamati maalum ya mkoa/jimbo itakayojumuisha wawakilishi kutoka vyama vya siasa, sheria, wakulima, wafanyakazi n.k itakayokuwa inapokea maoni ya wanachi juu ya kuwa na imani na mbunge au la kila mwaka. Kuwe na viashiria vya kumpima Mbunge.
  2. Wananchi kupitia kamati ya jimbo wawe na uwezo wa kuomba uchaguzi mdogo wa jimbo lao ikiwa kama watajirijisha kuwa hawana imani au mbunge wao hana uwezo wa kuongoza.

  Haya ni mawazo yangu na sina utaalam wa sheria. Gharama za chaguzi hizo nashauri katika kila jimbo kuwe na utaratibu wa kuchangia mfuko maalum kwa ajili ya maendeleo ya jimbo kwa mfano kunaweza kuwa na miradi mbalimbali kwa ajili ya mfuko huo nk.
   
 13. B

  Baba Mchungaji Member

  #13
  May 19, 2012
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 32
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  katiba mpya izuie huduma kama vile matibabu na elimu kufanywa na watu binafsi ili kulinda viwango vya huduma katika nchi yetu visishuke, mfano elimu sasa inashuka kwa kasi kiasi cha mtu kuhitimu mafunzo ya chuo kikuu lakini watu wenyewe kielimu wakiwa bado wapo chini. mwaka uliopita kuna taasisi moja ilitangaza ajira na mwisho wakasema mtu yeyote aliyehitimu chuo kikuu chochote anaruhusiwa kuomba isipokuwa kutoka katika chuo furani. pili Afya inashuka kwa kasi hii inachangiwa na watu kufanya kazi katika hospitali za watu binafsi ambapo vifaa vya serikali huhamia huko, pia watu wengine hukesha wakifanya kazi kwenye hospitali za private asubuhi huingia kwenye ajira ya umma na kuhitaji kupumzika hivyo huja kazini kwa ajili ya kuonekana tu na kupumzika!


  kazi za ubunge ziwe ni za wito na siyo za masirahi makubwa mpaka zinawafanya wafanyakazi kuache kazi za ujuzi wao kwa na kukimbilia kwenye siasa!
   
 14. k

  kpm Member

  #14
  May 20, 2012
  Joined: Jan 16, 2012
  Messages: 57
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 15
  Kwa kuanzia napendekeza yafuatayo:

  1. Nafasi za wabunge wa vitimaalum na wa kuteuliwa zisiwepo.2. Muundo wa serikali tatu:mbili zikiwa ni zile zilizoungana nay a tatu ile ya muungano3. Mawaziri wateuliwe nje yaBunge na siyo miongoni mwa wabunge4. Spika wa bunge asitokane nachama cha siasa, na asiwe mwakilishi wa jimbo lolote5. Mgombea wa nafasi yoyotesiyo lazima atokane na chama cha siasa.6. Idadi ya mikoa/majimboirekebishwe na wakuu wake wtokane na wananchi, na kila mkoa/jimbo liwe namamlaka kamili kuhusu mambo yake ya maendeleo.7. Nafasi mojawapo kati ya mkuu wa wilaya na mkurugenziivunjwe, na majukumu ya atakayebaki yalenge ktk utumishi wa umma na si wakichama.8. Raisi asiwe sehemu yabunge, na asiwe na nguvu ya kukataa muswada wowote uliopitishwa na bunge (asiwena mamlaka juu ya bunge)9. Makatibu wakuu wa wizara nawakurugenzi wapatikane kwa ‘interview’ na siyo kuteuliwa10. Raisi apunguziwe madaraka; kamakuteua wenyeviti wa bodi mbalimbali, majaji, n.k.
   
 15. N

  Ngwahi Member

  #15
  May 20, 2012
  Joined: Jul 24, 2011
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Mimi ningependa baraza la maaskofu litambuliwe rasmi kikatiba na lipewe meno ili kuiepusha nchi kuangukia mikononi mwa shetani
   
 16. KALYOVATIPI

  KALYOVATIPI JF-Expert Member

  #16
  May 21, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,419
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 0
  Nimecheka sana duh!
   
 17. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #17
  May 21, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Adhabu ya kifo tuu. Mauzi tuliyopata kutoka kwa Radda, Wizara ya madini. wizara ya mali ya asili, wizara ya fedha na tawala za mikoa yasingetokea kama kungekuwa na adhabu ya kifo.

  Halafu ummekuja ujanjanja mpya wa kuwasamehe wezi wa mali ya umma kama wanapata presidential appointment. Baraza la mawaziri huvunjwa ili kuwaghilibu wananchi waone hatua zimechukuliwa kumbe za kisheria zinakwepwa. Ona Kigoda alivyomsamehe mkurugenzi mkuu wa B/of standard. eti kajifanya kumsimamisha cheo chake wakati hatua za kisheria kazikwepa kuchukua. huu ujanja kuokomesha lazima tuweka adhabu ya kifo tuu.
   
 18. S

  SURA SIO SOHO Member

  #18
  May 22, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [QUOTE=binti ashura;3707636]ndugu zangu ni muhimu sana wote tushiriki katika uandaaji wa katiba mpya! itakuwa jambo la muhimu sana iwapo kila mwananchi mwenye ufahamu atoe mchango wake wa mawazo ili katiba itakayoundwa isiwe na vilakavilaka. mie ningependekeza hata kama wewe unanafasi fulani serikalini changia mawazo kama vile wewe hupo kwenye nafasi fulani jifanye kama ni raia wa kawaida. mfano wewe waweza kuwa mbunge unapochangia futa mawazo ya kuwa wewe ni mbunge.
  naomba kuwakilisha
  ![/QUOTE]

  MI NAFIKIRI KATIBA YETU YA SASA IMEKAA KIMYA KUHUSU SUALA LA USHOGA, NI MUDA MUAFAKA SASA KATIBA INAYOKUJA IKAWEKA BAYANA HAKI ZA MASHOGA. MAONI YANGU NI HERI TUKARUHUSU MASHOGA KUTAMBULIKA ILI TUWEZE PATA MISAADA KUTOKA NCHI ZA MAGHARIBI AMBAZO WAMETUPA KAMA PRE-CONDITION.
   
 19. b

  big niga Member

  #19
  May 24, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 71
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....kwa upande wangu ningependa kiwepo kipengele kinchohusu hawa NSSF wawe wanawakopesha wateja wao fedha zinazokatwa kila mwisho wa mwezi,hawafanyi hivyo kwa walala hoi wanawakopesha wabunge tu na watu maarufu, kipengere cha tume huru
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  May 24, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,094
  Trophy Points: 280
  ...Kama ambavyo Rais anaruhusiwa kuwa madarakani kwa awamu mbili za miaka mitano mitano, iwe hivyo pia kwa Wabunge wapewe vipindi viwili tu vya miaka mitano mitano na siyo kama ilivyo sasa baadhi ya Wabunge wako Bungeni kwa vipindi zaidi ya awamu mbili.
   
Loading...