Je, ungependa nini kiwemo kwenye Katiba Mpya? Mimi napendekeza Ruzuku ya Vyama vya Siasa iondolewe!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,840
141,763
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo.

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi.

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa.

Karibu
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Mimi napendekeza Rais anapostaafu ashitakiwe kwa mujibu wa sheria iwapo alikiuka utaratibu wakati anatawala .
 
Nakubali vyama vyote vifutwe, watu wachaguliwe. Kutokana na michango yao kwa jamii na jamii husika.

Mfano mbobezi wa sheria, daktari bingwa, kiongozi wa mama ntilie, kiongozi wa machinga, viongozi wa, wakulima, wanafunzi, walemavu, mafundi, wafanyabishara, wafanyakazi nk hawa wote wateuliwe na jamii zao kwenda kuwawakilisha wananchi.
 
Pia viongozi wa mkoa wapunguzwe, pia mtu akifanya kazi miaka mitano arudi mtaani akajiajiri, waingie wengine mzigoni(kuhusu uzoefu mimi sijui, sababu siyo HRM)
Hii point ni muhimu hizi kazi za kiuongozi ziwe kadhi za wito.

Mshahara uwe sawa /karibu na walimu, polisi, machinga, mama ntilie nk. Wajue uchungu wa maisha ya wengi.

Wapewe sehemu za kuishi kama mabweni, chakula bure, huduma za afya, elimu ya watoto bure kwenye shule za kata. Sawa na wengine wote.

Miaka ya kuwa kiongozi isizidi mitatu kuanzia uongozi wa wilaya hadi Urais. Baada ya hapo rekodi yako inaangaliwa na kijiji, kata, wilaya mkoa, taifa. Umefanya nini kwenye maisha yao.
 
Ningependeza kuondoa kinga kwa viongozi wote nchini. Hata wale waliokuwepo madarakani dhamani. Ili kuwe na uwajibikaji na uwajibishwaji.

MIkataba yote muhimu iwekwe wazi pamoja na mishahara / vipato vya viongozi.

Waonyeshe wamepataje hizo pesa kila baada ya miezi sita kupitia tax return, or tax summary kupitia TRA.
 
Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo

Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi

Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa

Karibu
Rais wa Tanzania lazima atoke Tanganyika, Haiingii akilini kisiwa chenye watu milion mbili, kitoe marais wawili kuongoza watu milion 60,
 
Wananchi wote walipe kodi hasa matajiri, wanasiasa. Sheria za kukwepa kodi na kuiibiwa serikali ziwe ni kunyongwa hadi kufa, au risasi kumi.

Mali yote iliyoibiwa itaifishwe na kurudishwa kwenye mikono ya umma.
 
Sheria za kodi ziwe za uhalisia, no double taxation, 10% kwa wenye vipato chini ya milioni kumi kwa mwaka. Unalipa baada ya kupata faida. Ukidanyanya imekula kwako. Maisha yako yanaishia hapo hapo.
 
Napendekeza elimu ya haki ya wananchi ifundishwe kuanzia shule za msingi.

Hizi haki tukae chini na kutafakali ni zipi.

Haki za msingi ni elimu, afya, hati ya kusafiri, maadili, makazi, kipato, utu hata yule ambaye hafanyi kazi apate pesa ya kula.

Kiufupi haki, mazingira wezeshi ya kuishi na kustawi.
 
Siasa ni ajira, na wafanya siasa wawe treated kama wafanyakazi wengi na si kakundi flani special, social security fund na taa sisi zingine zinazo wahusu watumishi walazimishwe kuwa wana chama.
 
  1. Wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo wasiwe wakurugenzi wa halmashauri za wilaya kwani hawawezi kumuangusha aliyewateua.
  2. Matokeo ya urais yahojiwe mahakamani.
  3. Rais asiteue watendaji wa tume.
  4. Cheo cha katibu tarafa na mkuu wa wilaya vifutwe.
  5. Kusiwe na ubunge au udiwani wa viti maalumu. Kuwe na utaratibu mwingine wa kuhakikisha wanawake wanashinda nafasi na si kupewa.
  6. Rais apunguziwe madaraka ya kuteua kila mtu. Hali hiyo imechochea watu kuwa machawa kwa Rais ili wapate vyeo vya kuteuliwa.
  7. Mambo ya ushoga yapingwe kiuwazi kwa kuwekewa ibara kabisa kwamba mashoga, wasagaji, na washirika wao wakipatikana wauawe.
  8. Mtu atakayeharibu uchaguzi kwa namna yoyote, kwa mfano kumtangaza mgombea aliyeshindwa kama mshindi, awekwe kifungo cha maisha.
  9. Kusiwe na mwanya wa kumtangaza mgombea yeyote kwamba ameshinda bila kupingwa.
  10. Kuwe na muda maalum wa uendeshaji wa kesi zote zinazogusa maslahi ya jamii na ziwe na taarifa zinazotolewa moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom