Ungependa kitu gani kiwemo kwenye katiba mpya?

Mi maoni yangu katika katiba mpya kusiwepo na sera za ksiasa kabisa,na badala yake kuwepo na sera za maendeleo,amani na uhuru kabisa,pia katiba izingatie mila zetu na culture zetu na lugha zetu.

Lakini kwa hali ilivyo anza katika mchakato huu,hii katiba inaonekana imebezwa sana kisiasa zaidi,kwani ccm tayari wameshalazimisha ziwemo sera zao ambzo sera hizo hutumia katika siasa zao na kufaidika wao kibinafsi kabisa.

Tumeona makada wa ccm wakiongea juu ya sera hizo za kisiasa zienziwe na ziwemo ndani ya katiba ili waendelee kuwatawala wananchi kwa tamaa zao binafsi,na kuwanyima uhuru wananchi kuamua wanacho kiamua nini wanataka katika katiba hio.

Ni nyema JK afahamu kuwa hii katiba ni muhimili wa nchi,kama anataka kuweka amani ya nchi na vizazi vijavyo,ni vyema katiba hii wakaachiwa wananchi wakajidili na kutoa maamuzi yao,na kuachana mambo ya kisiasa,tuweke taifa mbele,viongozi waelewe kuwa leo wapo kesho hawapo,maisha ni mapito tu,cha kujiuliza jee nimewafanyia nini na nimeiyandalia nini nchi yangu na vizazi vyangu nilivyo viacha ?
 
Kwa kuanzia napendekeza yafuatayo:

1. Nafasi za wabunge wa vitimaalum na wa kuteuliwa zisiwepo.2. Muundo wa serikali tatu:mbili zikiwa ni zile zilizoungana nay a tatu ile ya muungano3. Mawaziri wateuliwe nje yaBunge na siyo miongoni mwa wabunge4. Spika wa bunge asitokane nachama cha siasa, na asiwe mwakilishi wa jimbo lolote5. Mgombea wa nafasi yoyotesiyo lazima atokane na chama cha siasa.6. Idadi ya mikoa/majimboirekebishwe na wakuu wake wtokane na wananchi, na kila mkoa/jimbo liwe namamlaka kamili kuhusu mambo yake ya maendeleo.7. Nafasi mojawapo kati ya mkuu wa wilaya na mkurugenziivunjwe, na majukumu ya atakayebaki yalenge ktk utumishi wa umma na si wakichama.8. Raisi asiwe sehemu yabunge, na asiwe na nguvu ya kukataa muswada wowote uliopitishwa na bunge (asiwena mamlaka juu ya bunge)9. Makatibu wakuu wa wizara nawakurugenzi wapatikane kwa ‘interview' na siyo kuteuliwa10. Raisi apunguziwe madaraka; kamakuteua wenyeviti wa bodi mbalimbali, majaji, n.k.

You have the right vision. I support all your points. I reiterate your point about election of all political leaders. It is important that people are free to elect their leaders, not only at the national and village level, but also at the district and regional levels. Regional Commissioners must be elected. Do away with district governments. We have far too many leaders. We are over governed and underserved.
 
1. katiba yote ifundishwe kwenye somo la civics ili kila anaye maliza form 4 awe anaijua katiba vizuri. na in primary schools ifundishwe kwa kifupi. 2. nafasi za ukurugenzi wa mikoa, mkuu wa jeshi la polisi,jaji mkuu,makatibu wa wizara,wakuu wa wilaya na nafasi zote ambazo huteuliwa na raisi wakati zinahitaji taaruma zigombewe na zitangazwe kama nafasi za kazi nyingine ili kuweka uhuru wa kiutendaji na uwajibikaji. 3. spika wa bunge asiwe mbunge wa jimbo lolote na nafasi hiyo itangazwe wenyesifa wagombee wakipitishwa na bunge. 4.tuwe na serikali tatu tanganyika, zanzibar na muungano. 5. katiba itambue ushahidi wa kielectronic ili kwenda sawa na technolojia. 6. uchaguzi mkuu ukifanyika kama mbunge atafariki,kujiuzuru au kwa namna yoyote ile jimbo likabaki wazi mshindi wa pili apewe nafasi ya kuwa mbunge halali wa jimbo husika. 7. raisi asiwe na madaraka yoyote na bajeti na mda wa gunge la bajeti uongezwe. 8.raisi asiwe mtu wa mwisho kupitisha mswada. 9. tume huru ya uchaguzi ni muhimu tume isiteuliew na raisi bali wajumbe na viongozi wote wa tume ya uchaguzi wapate nafasi hizo kwa kuzigombea. 10. katiba idhibiti bidhaa feki kwa kuweka sheria kama kumshaki kila mwenye bidhaa feki hata kama ameinunua k/koo hii itasaidia kupunguza bidhaa feki nchini na ili mnunuaji asishitakiwe basi atakiwe kutoa risiti ya aliye muuzia ili ashugulikiwe na hii itafanya kila mwananchi kuthamini risiti na kuiongezea TRA mapato. 11. hela noti iliyokunjwakunjwa isitumike ili kusaidia utunzaji wa hela zetu na kila kitu/huduma nchini zitolewe kwa TZS na sio dola ili kukuza thamanni ya fedha yetu. 12. raisi asiteuwe wabunge na hawa wabunge wa kuteuliwa iwe mwisho. 13. hakuna ulazima wa kuwa na mkoa,wilaya na jimbo na vyote kuwa na viongozi lukuki, mkoa na majimbo ja uchaguzi vinatosha. ni hayo tu kwasasa.
 
Mapendekezo yangu nui:
1. Wabunge wa viti maalumu wawe maalumu kweli, wawe watu waioweza kusimama kwenye majukwaa na kuomba kura, na kuomba kura na watoke ma makundi maalumu kama Albino, Viwete, Vilema n.k si kama sasa ambapo ni nafasi za wanawake mabilionea na wenye ushawishi wa kisiasa na kiuchumi. Mfano, Getrude Lwakatare.
2. Kuwe na mahakama maalumu ya Uhujumu uchumi, ambayo itashughulikia makosa yote ya kifisadi, viongozi kujimilikisha mali n.k. Mahakama hiyo ipewe mamlaka kamili, ikiwamo kufilisi mali zilizopatikana visivyo, kutoa hukumu ya kifungo cha maisha n.k
3. Ielekeze vipaumbele vya Taifa, ikiwano kilimo n.k. Kila chama kitakachochukua madaraka lazima kifuate vipaumbele hivyo.
4. Iweke wazi aina na mfumo wa uchumi na seriklali. Pamoja na jinsi watu wa hali ya chini watakavyopunguziwa mzigo wa kodi.
5. Itenge siasa na biashara. Mfano, kama kionozi ni mmiliki wa kampuni fulani asiwe kwenye tume au kamati inayohusiana na kazi za kampuni yake.
6. Viongozi wa Bunge (Spika, Katibu n.k), na serikali kama Waziri Mkuu, Mawaziri, Makatibu Wakuu, n.k wasitokane na Wabunge au chama chochote cha siasa. Wawe waajiriwa.
7. Kuwe na mfumo wa wazi unaoeleza mishahara pamoja na malipo yoyote yale kwa watumishi wa serikali (watumishi na viongozi wote).
8. Kiongozi au mtumishi yeyote yule wa umma aliyeshindwa kutimiza majukumu yake asipate tena nafasi ya kutumikia Taifa.
9. Tume huru ya uchaguzi, tume ambayo haitokani na ushawishi wowote wa kisiasa.
10. Ieleze mikakati ya kulinda na kusaidia sekta binafsi. Sekta binafsi ndiyo ingine ya uchumi kwa mataifa yaliyoendelea.
11. Na kadhalika....
 
1. Nashauri katiba iunde mahakama ya katiba ambayo itatatua kero zote za kikatiba na itashughulikia ammendments za katiba.

2. Nashauri Katiba iweke wazi kwamba Tanzania ina mikoa mingapi na wilaya ngapi. Sitaki kuona kiongozi anaongeza au kupunguza mikoa, majimbo, wilaya kwa sababu za kisiasa. Katiba iseme Tanzania ina mikoa xx, wilaya xxx na majimbo xxxx. Kiongozi asiruhusiwe kuongeza au kubadili chochote isipokuwa kwa aidhini ya bunge na mahakama ya katiba.

3. Ningependa kuona katiba ikimpunguzia nguvu Rais wa Serikali ya JMT, viongozi wote wanaoteuliwa na Rais wasiapishwe mpaka watakapopitishwa na Bunge. Hii ni kwa majaji, gavana, mabalozi na tume zote zilizopo nchini

4. Ningependa kuona katiba ikiwapa uhuru TAKUKURU ya kushitaki watuhumiwa bila kupeleka jalada la kufungua kesi kwa Mwanasheria Mkuu na Mkurugenzi wa Mashtaka wa Serikali.

5. Ningependa kujua kama mawazo yangu yamefika sehemu husika
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom