Ungekuwa wewe ungeuliza nini?. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ungekuwa wewe ungeuliza nini?.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mchemsho, Jul 23, 2011.

 1. mchemsho

  mchemsho JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 3,158
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Kama ungepata bahati ya kukutana na JK, halafu nchi nzima inawaangalia na kuwasikiliza, je ungemuuliza swali gani Mheshimiwa Kikwete?
   
 2. g

  geophysics JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 904
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa nini anatumia pesa za wananchi ovyo kwa kutembea nchi mbali mbali kwa ziara zisizo na tija?
  Kwanini tangu amechaguliwa kuwa mkuu wa nchi ameendelea kuacha mkoa wa Dar es Salaam ambao una watu wengi kukaa bila kuwa na mkuu wa mkoa?
   
 3. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Swali; Ku-break the ICE ningemuuliza unaionaje hali ya uchumi wa nchi na ya watanzania kwa ujumla?
  Jibu lake litakuwa; Uchumi kwa maana ya macroeconomy unakuwa kwa kasi ya 7% na Tanzania ni moja wapo kati ya nchi 20 duniani zinazokuwa kwa kasi hii. teh teh teh (atacheka). Na hapa tunastahili pongezi lakini wapo watu wanasema hatujafanya kitu kabisa!

  Swali: Lakini Mh. huoni hali ya wananchi wako inazidi kuwa duni wakati unasema uchumi unapaa kwa kasi?
  Jibu lake litakuwa: Ni kweli na hiyo ndiyo challenge yetu kama serikali. tunajitahidi kuutafsiri uchumi huu katika mazingira/uchumi wa mtu mmoja mmoja (microeconomy) ndio maana tunavutia wawekezaji, Tumekuja na mpango wa kilimo kwanza blah blah blah. Watanzania wavute subira tu

  Swali: Sasa Mh. Rais, watanzania watavuta subira vipi wakati hali inazidi kuwa mbaya! Mfumuko wa bei umepanda juu kuliko hali ulivyoikuta (mfano kilo ya unga wa ugali kwa mwaka 2004 ilikuwa sh 400 leo ni sh 1000), bei ya mafuta inazidi kupanda na mbaya zaidi mmepandisha mpaka mafuta ya taa ambayo yanamgusa mwananchi wa kima cha chini kwa kigezo cha kudhibiti uchakachuaji (hii ni institutional failure), thamani ya shilingi inaporomoka kwa kasi ambayo haijawahi kuonekana kwa miaka 50 ya uhuru wetu, nauli juu, nishati hakuna, ongezeko la mishahara haliendani na ongezeko la gharama za maisha, rasilimali za taifa zinachukuliwa bila wananchi kufaidika, mfumo wa serikali hautilii mkazo uwajibikaji bali kulindana, wizi na ufisadi wa mali ya umma umeshamiri na wananchi hawaoni hatua muafaka zinazochukuliwa na kibaya zaidi ni wewe mkuu wa kaya kutumia % kubwa ya muda wako nje ya nchi kuliko nchini kwako ukitatua kero za wananchi. Huoni ni muafaka kwa wewe binafsi kuachia ngazi katika maazimisho ya miaka 50 ya uhuru wetu ili kulinda heshima yako mbele ya jamii?

  Jibu: Kweli hali ya maisha ni ngumu... (ghafla umeme unakatika na watanzania wanashindwa kusikia majibu ya rais ktk maswali haya ya msingi
   
 4. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,004
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  swali: mbona unapenda kuchekacheka?
  jibu: unaju (kicheko) unajua watanzania hawapendi mtu mkaidi, (kicheko) wanapenda amani na hivyo hii ni isahara ya upendo na amani.
  (kicheko tena.)
   
 5. V

  Vonix JF-Expert Member

  #5
  Jul 23, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  1.Nini kinamfanya acheke kila wakati hata kwa mambo ambayo ni serious usingetegemea mtu acheke.
  2.Kifungu cha sheria alichotumia kuwaambia wezi wa epa wakirudisha hela hawatashitakiwa,huo ni utawala unaozingatia sheria!!
  3.Kama anahakika kutimiza ahadi zote alizoahidi wakati wa uchaguzi wakati mpaka sasa hivi hana hata moja aliyotimiza.
  4.Anazo sababu za maana za kusherehekea miaka hamsini ya uhuru wakati nchi imegubikwa na simanzi kila mahali,uchumi duni,umeme hakuna,maisha ya wananchi wake ni mabaya haijawahi kutokea.
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mkuu jibu la swali la mwisho ndo balaa yaani hapa mpaka mbavu zinauma kwa kicheko....
   
 7. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #7
  Jul 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwa nini mheshimiwa una shindwa kuelewa unachoulizwa..
   
 8. S

  SEAL Team 6 JF-Expert Member

  #8
  Jul 23, 2011
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 655
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Swali langu kwa JK lingekuwa kama ifuatavyo.
  1. Unajua kwa nini Tanzania ni Nchi masikini?
  2. Kwanini wanafunzi wa kike tanzania wanapata mimba wakiwa bado shuleni?
  3. Je ule ulinzi usioonekana aliopewa na Shekh Yahaya bado anao?
  4. Je safari hii amepanga kuanguka jukwaani lini na wapi.
   
 9. Tuyuku

  Tuyuku JF-Expert Member

  #9
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 3,149
  Likes Received: 1,407
  Trophy Points: 280
  Wewe ni genius aisee! Nimeipenda.
   
 10. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #10
  Jul 23, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,141
  Likes Received: 3,330
  Trophy Points: 280
  Kwanini asijiuzulu kwani ameshindwa.
   
Loading...