Ungekuwa wewe ungefaya kitu gani?

Ungekuwa wewe ungefaya kitu gani?

mkwezi kidonda

Senior Member
Joined
Mar 20, 2014
Posts
163
Reaction score
32
Ndoa ni ya kanisani na Umeishi na mkeo kwa miaka mnne na kubarikiwa kupata watoto wawili. Ghafla unagundua mkeo ni mshirikina kwa kuwasiliana na waganga ili ndugu zako wathurike tena kwa kumwambia mganga awatupie majini ndugu zako wapatao saba kwa kuwataja majina kisa kuhisi wanaleta maneno ndani ya nyumba yenu. Je Wewe mdau ungefanya kitu gani kwa mkeo na ndugu zako je utawaambia?
 
Mzee mmoja aliwahi kumtoa mbio na bunduki mkewe na mganga baada ya mke kuleta mganga nyumbani eti azindike nyumba!!
 
Hakikisha kwanza isiwe ni maneno tu ya watu
 
Ningevunja vunja kazi za roho ya uchawi/uganga na kuwafunika ndugu zangu kwa damu ya Yesu Kristo ,ila sitawaambia ndugu maana watamchukia sana,baada ya muda ataacha tu na kuwa mke mzuri...kuna nguvu ya ajabu katika maombi"......ombeni lolote kwa jina langu nami nitawapa ili furaha yenu iwe timilifu"

 
Ndoa ina mitihani jamani,Allah aepushie mbali
hapo ni kumkanya wife na kuleta mtumishi wa Mungu aombee nyumba yenu
 
Nenda kwa mchungaji aliyewafungisha hiyo ndoa au kanisa lililo karibu na wewe ukapate msaada humu ndani ukiona wanaguna ujue yako juu ya uwezo wao
 
Ningemwuliza kwanini ameamua kujihusisha na maswala hayo. ila majibu kama hayaridhishi mpe muda aende kwao kupumzika bila kumpa muda rasmi wa kurudi najua itamwumiza kukaa bila kujua lini arudi naitapelekea kuwaambia ndgzke ukweli sasa from there ndo mlijadili kifamilia na kumpeleka kwenye huduma za maombezi akombolewe fikra
 
Ndoa ni ya kanisani na Umeishi na mkeo kwa miaka mnne na kubarikiwa kupata watoto wawili. Ghafla unagundua mkeo ni mshirikina kwa kuwasiliana na waganga ili ndugu zako wathurike tena kwa kumwambia mganga awatupie majini ndugu zako wapatao saba kwa kuwataja majina kisa kuhisi wanaleta maneno ndani ya nyumba yenu. Je Wewe mdau ungefanya kitu gani kwa mkeo na ndugu zako je utawaambia?

Wewe umefanya nini baada ya kugundua hayo Mr/Miss kidonda?
 
Back
Top Bottom