Ungekuwa wewe ungefanyaje, ungemsaidiaje?

Ungekuwa wewe ungefanyaje, ungemsaidiaje?

Sheffer95

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2020
Posts
274
Reaction score
771
Habari za ndugu, jamaa na marafiki wa JamiiForums

Katika maisha, tunakutana na watu tofauti ambao hatukuwatarajia na wanakuja kuwa kama ndugu zetu tulioshibana nao tukisaidiana katika changamoto za hapa na pale.

Nina kisa kimoja kilichotokea na kuniacha katika njia panda ya nn kilicho sahihi nifanye.

Iko hivi nina rafiki yangu ambae tumekuwa kama ndugu, kwanza tunafanya kazi sehemu moja, na pia katika investment tumewekeza pamoja na almost kila kitu cha kupiga hatua tunapambania pamoja.

Sasa kuna kipindi alikuwa na ugomvi na mke wake ambao ilifikia kuwepo Vikas vingi na usuluhisho usiofikia Kikomo. Jamaa yeye sio mnywaji ila mkewe ni mnywaji sana na mtu ambae anapenda kutoka kwenda Maclub na kujichanganya na ndio moja ya sababu ya wao kupumzishana ili ajirekebishe tabia.

Sasa weekend moja niko maeneo napata kinywaji, namuona mke wa huyo jamaa yangu nae yuko hapo anajiachia, kwanza kavaa mavazi ambayo yanasikitisha, pili kalewa balaa anashikwa shikwa hovyo na wanaume na yeye kajiachia hovyo.

Kiukweli roho yangu iliumia sana mpaka nikahisi ndio mm kama nafanyiwa, sikuwa na amani tena nikaondoka lakini jambo hili linanikosesha amani kiasi kwamba naona kama namsaliti jamaa yangu nisipomwambia.

Lakini pia sitaki kuwa sehemu ya kuwatenganisha kama wataachana mazima maana najua kwa Aina hii ya mwanamke watoto watapata shida sana 😢 maana mwanamke huyu sio mlezi mzuri kabisa na jamaa yangu ana Wadena sana wanae na hapendi walelewe na mzazi moja.

Je, wewe ungekuwa kwenye nafasi kama yangu ungefanya maamuzi gani?
 
Tulia kimya sababu siku wakipatana wewe utaonekana mchonganishi, maadam mume anajua tabia za mkewe waache wapambane wenyewe maswala ya kuhakikisha ulimuona kiwanja gani usitengeneze jumba bovu litakalokuangukia baadae kwa vitu ambavyo vilikuwepo toka mwanzo.
 
Mada ifungwe
 
Akija jua kwamba na wewe ulikuwa unajua ukapiga kimya + nyakati hizi za magonjwa mengi vipi yakimpata rafikiyo wa pekee
 
Habari za ndugu, jamaa na marafiki wa JamiiForums

Katika maisha, tunakutana na watu tofauti ambao hatukuwatarajia na wanakuja kuwa kama ndugu zetu tulioshibana nao tukisaidiana katika changamoto za hapa na pale.

Nina kisa kimoja kilichotokea na kuniacha katika njia panda ya nn kilicho sahihi nifanye.

Iko
Kama una nia ya kumsaidia huyo rafiki yako kwa faida ya wanae baadae. Ingependeza kama muda huo ukiwa club na huyo mkewe akiwepo katika haki hiyo ungemwita jamaa aje aone na umpe ushauri kuwa hapo mke hakuna atafute mwingine. Be a man.
 
Mmmmmmh!!!!
Nyamaza.. ungemjali kiukweli kuumia hivi ungemuita aje ulipo.. ajionee mwenyewe sio kumtumbulia macho mkewe masaa yote hayo.. na bila kukaa unapomuona mkewe.
 
Tumia ile mbinu ya kuchimba shimo na kusema mfalme ana masikio kama ya punda kisha panda mti ukikua utafanya kazi iliyokushinda.
 
Kama una nia ya kumsaidia huyo rafiki yako kwa faida ya wanae baadae. Ingependeza kama muda huo ukiwa club na huyo mkewe akiwepo katika haki hiyo ungemwita jamaa aje aone na umpe ushauri kuwa hapo mke hakuna atafute mwingine. Be a man.
Umenena vyema bora afanye hivyo mwenye Mke ashuhudie mwenyewe kwa macho yake aamue kunyoa au kusuka.
 
Muombe shem ako game afu uone
Akili za kipumbavu kama hizi, yaani ww uko tayari kurisk everything kwasababu ya pussy ambazo mtaani ziko za kutosha. Hakika tuliambiwa mwanaume ukiweza control your serial urge basi 70% ushatoboa, sasa ww unawaza mapenzi wenzio wanawaza kuacha legacy za udugu na mshikamano
Aiseeeeee!!!!
 
Huyo jamaa mwenye mke ni wewe usimsingizie rafiki yako. Cha kukushauri mpige chini mkuu, utakuja kunishukuru badae
Think critically, na naamini ww ni mtu ambae huna rafiki ulieshibana nae thus unafikiria hatua fupi kiasi hiki
 
Kama una nia ya kumsaidia huyo rafiki yako kwa faida ya wanae baadae. Ingependeza kama muda huo ukiwa club na huyo mkewe akiwepo katika haki hiyo ungemwita jamaa aje aone na umpe ushauri kuwa hapo mke hakuna atafute mwingine. Be a man.
U think it is easy to see ur friend cries infant of u, do u know how does that feel??
Sio rahisi kumuona mwanaume akilia au akikwambia mambo yake mazito na anakuwa kama anakata tamaa mtu ambae ana great vision, mpambanaji na anayependa kujitoa kisa tu mwanamke mshenzi
Anyway ahsante kwa ushauri
 
Mmmmmmh!!!!
Nyamaza.. ungemjali kiukweli kuumia hivi ungemuita aje ulipo.. ajionee mwenyewe sio kumtumbulia macho mkewe masaa yote hayo.. na bila kukaa unapomuona mkewe.
Kwanza yeye kanikuta hapo mahali, pili mwanamke mshenzi ni mshenzi tu why umlete rafiki yako aje adharirishwe na mjinga mmoja
Wanawake mkipata wanaume humble, caring na ambao wanapenda watoto wao ndio huwa mnatumia kama fimbo sio?
 
Back
Top Bottom