Ungekuwa wewe ungefanya nini?

thadei kimambo

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2013
Posts
220
Reaction score
126
Vuta picha umelala mida ya alfajiri hivi, usingizi ule wa kukesha jana yake, halafu kuna mtu anakuja kukugongea mlango kwa fujo sana kwenye mida ya saa moja moja hivi.

Ile unaamka kwa hasira kwenda kumfungulia unajikwaa kidole cha mwisho cha mguu katika kona ya kitanda - ile ndiii!, ukaruka kwa maumivu ukapamia ndoo ya maji yakamwagika sakafuni.

Mara unateleza katika yale maji unaangukia meza unaangusha TV, deki na wewe chini mara waya wa umeme unakupiga short mgongoni unafika mlangoni na maumivu ya kidole na uchovu + hasira+hasara na short juu unakutana na jamaa anakwambia nasajili line za simu halafu anakutolea meno kwa tabasamu, eti pozi la biashara.

Sipati picha utamfanyaje?
 
nampigisha deki yale maji mpaka yakauke kah
 
Hahaha! Dah kwa hasira nampamia nayeye asikie maumivu nlopata!
 
kwa hasira nampa laki moja halafu namwambia nenda.
 
Duh! Kweli ataacha kufanya tena hio biashara kwa atakachokipata.
 
Hapo saa hiyo naishi mtaa gani.........?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…