Ungekuwa wewe ndiyo boss, ungemfanya nini Bakari?

CHIEF MP

JF-Expert Member
Jul 6, 2011
1,559
678
Hi guys, nimependa tufurahie kidogo wote akili ya huyu BAKARI vs Boss wake....

Haya power to youuuu....

Bakari ni house boy mara nyingi huiba wine ya boss wake na kisha kuongeza maji kwenye chupa ili boss asigundue. Mara kadhaa boss alihisi ladha tofauti anapokunywa wine hivyo kuhisi kuna mchezo mchafu alihisi tu Bakari anahusika.

Ilikua ni bahati tu alimvizia na kumbamba Bakari akichakachua wine, kwa kuwa mkewe alikua anamtetea Bakari, ili kumthibitishia mkewe kuwa Bakari ndo culprit, boss alianza kwa kumuuliza Bakari maswali. Siku hiyo Bakari alikua jikoni, boss na mkewe walikua sebuleni.

Boss:- Bakariiii!

Bakari:- Naam baba!

Boss:- Nani anakunywa wine yangu?

Bakari:- Kimyaaaa hajibu kitu!

Boss:- Bakariiiii !

Bakari:- naam baba! Boss:- nauliza nani anakunywa wine yangu halafu anajazia majiii!

Bakari:- kimyaaaaa!

Boss akaamua amfuate hukohuko jikoni.

Boss: Kwanini nikikuita unaitikia, nikikuuliza unanyamaza?

Bakari: Baba huku jikoni ndo kulivyo, unasikia jina tu likiitwa lakini maneno menginehusikii, na kama huamini baki jikoni mi niende sebuleni.

Bakari akaenda sebuleni akaanza kuita.

Bakari:Babaa!

Boss: Naam Bakari!

Bakari: Saa sita usiku huwa unaenda kufanya nini chumba cha house girl?

Boss:- kimyaaaa!

Bakari:- Baba babaa!

Boss:- Ndio Bakari!

Bakari:- Nauliza hivii, chumbani kwa house girl saa sita za usiku huwa wafuata nini?

Boss:- kimyaaaaaaa!

Boss akatoka nje: Bakari huku jikoni ni kweli husikii kitu zaidi ya jina!.

Mama akasema msinizingue nyie... Mbna cwaelew..

Bakar: mama kama uamini na ww nenda uone.

Mama akaenda jikoni..

Bakari: akaita mamaa

Mama : bee bakari

Bakari: eti hyo mimba niya baba au yangu.?

Mama kimya

Bakari; mama akauliza tena hiyo mimba niyababa au yangu.

Mama aktoka aisee kweli humu unasikia jina tu
 
Hahahaa kweli ukiingia jikoni unasikia tu jina lako, maswali huyasikii, case ya bakari imeisha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Bakari....! Mbunifu sanaa msalimieni huko aliko ila aache tabia chafu atakatwa kichwa aanze kulaumu walimwengu.
 
Bakari....! Mbunifu sanaa msalimieni huko aliko ila aache tabia chafu atakatwa kichwa aanze kulaumu walimwengu.

Mwadunda zimefika salam!!!
Apo ujasiri WA kumkata kichwa utautoa wapi wakt kawabananisha n mkeo?!!!!
 
Hata ukiingia PM kuna vingine unakuwa huvisikii...!

Njoo PM uthibitishe, but lazima uwe ke!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom