Ungekuwa raisi wa Tanzania kama JK Ungelifanyia nini Taifa?

MAGEUZI KWELI

JF-Expert Member
Jul 16, 2011
1,947
253
Jamani nimependa kupata upeo wa kila mwana jf, Maoni yenu kweli ni changamoto kubwa sana kwa Taifa na wanasiasa wanaoumia kwa kuwepo kwa huu mtandao,
Sasa hebu tuwaumize zaidi wanasiasa wanaochukia huu mtandao

Ungekuwa wewe ni Presidaa wa Tanzania, Ungelifanyia nini taifa lako kwa kipaumbele na kila mtanzania kuridhika na wewe??
 
Moja ya maswali ya msingi uwa najiuliza binafsi na majibu yake uwa ninayo mwenyewe binafsi na mabyo baadae uwa nikija kuwashirikisha baadhi ya jamaa na jamii inayonizunguka uamuzi wangu mwenyewe ndio uwa mlango wangu mwenyewe wa kunihukumu.

Kikubwa ninachokiona kwanza ni Tanzania kuendeshwa na mtu au watu na si taasisi [Institution] kwa umri wangu sasa toka nimekua na kufika kuwa ni mmoja ya wanajamii,nimejikuta najiuliza maswali mengi ambayo hayana wa kuyajibu,na kwa kuwa mimi ni wa kizazi cha dotcom basi kidogo uwa na google na surfing kujua juu ya lile ninalojiuliza je wenzetu uwa wanakuwa na majibu gani.

Mfumo wetu wa uongozi, utekelezaji na maamuzi umekaa kwenye mfumo wa pilamid yanio kuanzia juu kuja chini na kwa kuvest madaraka na maamuzi mengi kwa mtu au watu wachache na sio taasisi,yani ni mfumo.Na ndio maana yoyote anaeingia madarakani ndani ya jamii zetu kuanzia Rais mpaka Mwenyekiti kila anpoingia uanza mambo mapya yani uanza ukurasa mpaya tofauti na misingi na malengo ya mwelekeo wa jamii.

Je kama Taifa kabla ya Rais kuchukua maamuzi yoyote yale ni lazima awe amepata mawazo ya think tank [Wanataaluma na wasio wanataaluma wenye uwezo mkubwa wa kujua na kupima mambo muhimu yanayohitajika au yanayotokea kwenye jamii au Taifa na kuyapatia majibu ya muda mfupi na muda mlefu] ambayo ufanya nae kazi ili kuipa nchi mwelekeo sahihi kwenye kila sekta na kisha wananchi wake kuafikia mwelekeo uliozalishwa na think tank kuwa huko tunakokwenda ni sahihi na kupima madhara ya maamuzi yatakayotolea je yatakuwa na uzito upi kwa jamii husika?

Hivyo kusema Rais pekee awe muamuzi wa mwisho ni sahihi lakini pia tusisahau kuwa Rais ni taasisi [Institution] na sio yeye kama yeye japo uwa anawajibika kama yeye.,kwa kuwa gharama za maamuzi yetu tulivest kwake kupitia sanduku la uchaguzi.

Mwisho wa yote katika hali hii tulitonayo sasa kikwete ajiunge kambi ya Wananchi kwa kuwa kwa hali ya sasa Taifa limekuwa sana kimwamko na kuwa kwa mwamko huo anaweza kuona vijana na watoto wa sasa walivyo na ufahamu.Zile zama za watu wa kizamani ambao ni watiu wazima waliolelewa na kukuzwa kwenye mawazao ya kikoloni kuwa Kiongozi lazmia awe jinamizi linalotisha raia basi zama hizo azina nafasi tena.Kiongozi anapaswa kutembea na kuyatenda yale ambayo wananchi wake wamemtuma kuyatenda na kuyasimamia kwa niaba yao.

Hivyo jitihada zaote za kuenda kinyume na matakwa ya wananchi na kuunda kaburi la maisha yake binafsi, familia yake, na marafiki zake.Hivyo ni heri ya nusu shari kuliko shari kamili,urafiki ni muhimu lakini unapokabidhiwa madaraka ya jamii urafiki hauzidi dhamana ya wananchi juu yako wewe uliyepewa dhamana.

Hivyo kwa sasa JK hana budi kukubali lawama za upande mmoja na upande huo ni ule ambao yeye anahakika ndio walio mpa dhamana,nayo ni kukubali kusimamia maamuzi sahihi ya kuwachukulia hatua wale wote ambao wamekeuka makubaliano yake na wao ya kuendesha nchi basi awapige chini na kuliachia Taifa rekodi sahihi za kiushahidi hata kama ni marafki zake kupiti nini.Kwa kuwa kilichobora kwake ni Taifa liwepo na si marafiki zake wawepo.Kwani pasipo marafiki zake Taifa litakuwepo.
 
Kwa miaka hii mitatu iliyobakia ningewaachia tu nchi yenu nikaishi US maana nchi yenu ina matatizo mengi mno tena nafikiri ni ya kurithi. -- hayangoleki hata kwa kutumia mbinu za medani. :lol:
 
Back
Top Bottom