Ungekuwa mmojawao ungefanyaje?????

Tangopori

JF-Expert Member
May 11, 2012
1,629
1,282
Wanafunzi watano wa chuo kikuu kimoja hapa nchini walikuwa wanatakiwa wafanye mtihani siku inayofuata. Wale wanafunzi walikunywa pombe mpaka saa kumiza usiku,asubuhi ya siku ya mtihani kila mmoja alikuwa na uchovu hivyowalishindwa kufanya mtihani.
Wakatunga uongo wa kwenda kumuongopea ticha wa somo husika. Wakaenda kumuongopea ticha kuwa wameshindwa kufanya mtihani kwa sababu jana walikuwa kwenye harusi na wakati wanarudi gari yao ikapata pancha na wakavamiwa na vibaka na kuibiwa pamoja na kupigwa.
Ticha akakubali akawapa siku tatu za kujiweka sawa na kujiandaa na special exam. Siku ya mtihani wa Special yule ticha aliwapa mtihani naaliwasimamia mwenyewe.
Mwongozo wa mtihani ulikuwa kama ifuatavyo,
1.Mtihani huu ni kwa wanafunzi watano
2.Majibu yao lazima yawe sawa na yakiwa tofauti wote wanapata ziro na wanafeli 3.Mtihani huu una maswali matano na yote lazima yajibiwe.
Maswali ya mtihani yalikuwa hivi.
1.Harusi ilifanyika katika ukumbi gani?
2.Gari mliomtumia mpaka mkapata pancha inaitwaje?
3.Ajali imetokea eneo gani?
4.Nani alikuwa dereva?
5.Tairi ipi ilipata pancha,ya mbele auya nyuma?
NAWATAKIA MTIHANI MWEMA!!
 
Mie napata ajali nyingine ya heart attack on the spot ili nipate siku nyingine
 
Ilisha wekwa hapa hii!

Any way ukiwa muongo unatakiwa kujipanga vema!
 
Back
Top Bottom