Maonesho ya kazi za kishirikina

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Waafrika kuna mahali tumepigwa chenga ya mwili kisha tukaachwa solemba. Mabeberu (kwa jina pendwa la chama kikuu) walitukuta na sayansi yetu ya asili ikiwa imepiga hatua kubwa kwenye utafiti, matokeo na utendaji pia, wakaona tukiendelea nayo tutakuja kufanya makubwa na kuwaacha mbali na pengine hata kuwatawala.

Wakaona hatari na kitisho kinachowakabili. Wakaja na mbinu ya kukandia vya kwetu na kusifu vya kwao, wakafanikiwa kwenye hili. Kishapo badala ya kutufunza vya kwao vizuri wakatunyima maarifa haya.

Nasikitika kusema kwamba mwaka jana tulipanga kuwa na kongamano kubwa la wachawi na washirikina lakini lilishindikana kufanyika kutokana na serikali kutoitambua hii kaliba. Lakini cha ajabu kuna mkoa mwaka huu kuna waganga wachawi zaidi ya mia walikusanyika na kutoa ultimatum kwenye jambo la kisiasa. Imagine huo ni mkoa mmoja tu. Kuna walozi zaidi ya mia.

Kuna huyu ndugu yetu 4G LTE ameanza kutuletea simulizi za visa vya kushangaza visivyo na majibu huko Ulaya. Nina hakika visa kama hivyo vilivyokosa majibu ya kisayansi huko kwao hapa Africa vingepatiwa ufumbuzi kupitia kaliba ya ushirikina uchawi na ulozi.

Sasa hivi tumebaki tupotupo tu. Ushirikina tunaambiwa ni mbaya na hauna faida. Sayansi tunayohubiriwa kuwa ndio mkombozi tunabaniwa maarifa yake. Hebu katembelee tume ya sayansi ya Tanzania utaniambia.

Sasa ili kuweza kuwa na way forward ni vema sasa tukaandaa msimu wa kazi za kishirikina, kichawi na ulozi ili kuvunja ile miiko na dhana dhanifu kuwa hii tasnia haina mema wala faida. Maonesho husika yatasaidia kuleta mwamko mpya wa elimu ya giza, utafiti na hata matokeo yenye faida kwa jamii.

Maonesho husika yatasaidia kuondoa woga kwa baadhi ya mafundi na kufanya waoneshe kwa uwazi zana za maangamizi walizo nazo. Licha ya kuwa ni maonesho yatayakostua na kushangaza wengi lakini yatalifanya taifa lijulikane zaidi huku yakivutia utalii na kutoa msukumo wa wageni wengi zaidi kutaka kufahamu zaidi.

Najaribu kuandaa andiko mradi kisha nilipeleke wizara husika, pengine kipindi hiki tutasikilizwa.

tapatalk_1564948276253.jpeg
 
Ama kweli usimchezee usiyemfamu, kama kwa umri huo ulishapinda namna ile je , kwa sasa bro Mshana Jr, ukoje ?

 
Tukiwa serious tunaweza kufanya hii kitu ikawezekana kabisa... Lakini wengi hatuwezi kuwaza nje ya box tunaiga na kunakili tuu
Nimeangalia show kidogo, nikawa bored maana wanaiga wamarekani lakini wanafeli vibaya. Wakati mmoja angeingia na ungo apae ukumbini na kuzunguka angepata point lukuki na mialiko Ulaya na Marekani, kwa sababu wenzetu hawana utaalamu huo..
 
Waafrika kuna mahali tumepigwa chenga ya mwili kisha tukaachwa solemba... Mabeberu (kwa jina pendwa la chama kikuu) walitukuta na sayansi yetu ya asili ikiwa imepiga hatua kubwa kwenye utafiti, matokeo na utendaji pia....wakaona tukiendelea nayo tutakuja kufanya makubwa na kuwaacha mbali na pengine hata kuwatawala...

Wakaona hatari na kitisho kinachowakabili... Wakaja na mbinu ya kukandia vya kwetu na kusifu vya kwao... Wakafanikiwa kwenye hili... Kishapo badala ya kutufunza vya kwao vizuri wakatunyima maarifa haya

Nasikitika kusema kwamba mwaka jana tulipanga kuwa na kongamano kubwa la wachawi na washirikina lakini lilishindikana kufanyika kutokana na serikali kutoitambua hii kaliba.... Lakini cha ajabu kuna mkoa mwaka huu kuna waganga wachawi zaidi ya mia walikusanyika na kutoa ultimatum kwenye jambo la kisiasa... Imagine huo ni mkoa mmoja tuu...!!! Kuna walozi zaidi ya mia

Kuna huyu ndugu yetu 4G LTE ameanza kutuletea simulizi za visa vya kushangaza visivyo na majibu huko ulaya.... Nina hakika visa kama hivyo vilivyokosa majibu ya kisayansi huko kwao hapa Africa vingepatiwa ufumbuzi kupitia kaliba ya ushirikina uchawi na ulozi.....

Sasa hivi tumebaki tupotupo tu... Ushirikina tunaambiwa ni mbaya na hauna faida... Sayansi tunayohubiriwa kuwa ndio mkombozi tunabaniwa maarifa yake... Hebu katembelee tume ya sayansi ya Tanzania utaniambia...

Sasa ili kuweza kuwa na way forward ni vema sasa tukaandaa msimu wa kazi za kishirikina, kichawi na ulozi ili kuvunja ile miiko na dhana dhanifu kuwa hii tasnia haina mema wala faida... Maonesho husika yatasaidia kuleta mwamko mpya wa elimu ya giza, utafiti na hata matokeo yenye faida kwa jamii

Maonesho husika yatasaidia kuondoa woga kwa baadhi ya mafundi na kufanya waoneshe kwa uwazi zana za maangamizi walizo nazo... Licha ya kuwa ni maonesho yatayakostua na kushangaza wengi lakini yatalifanya taifa lijulikane zaidi huku yakivutia utalii na kutoa msukumo wa wageni wengi zaidi kutaka kufahamu zaidi...
Najaribu kuandaa andiko mradi kisha nilipeleke wizara husika, pengine kipindi hiki tutasikilizwaView attachment 1172515

Naunga mkono hoja!
Hivi, wizara inayo husika na utamaduni, wanajali utamaduni gani kama hawataki ku acknowledge utamaduni huu?
Wazungu wakiongea kwa simu ni sayansi, wakati sisi walikuta tayari tuna simu zetu za upepo (wakaziita ushirikina)
Wazungu wakienda makaburini, wanasema kuhiji au kuombea marehemu - sisi tulikuwa nautaratibu huu wa kwenda makaburini kuombea na kuwaomba marehemu, wakaita kuwanga makaburini.
Wafu wa kizungu ni watakatifu, wafu wa kwetu ni mizimu, daaah😳😳😳😭😭
 
Back
Top Bottom