Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Ni upumbavu kuweka kitu cha Google hapa! ni kiwango gani cha hiyo sumu ndo kinakuwa na madhara kwa binadam, namaanisha katika kipimo cha ppm?
 
Aliyekufundisha kakupoteza kabisa, na kama umetumwa kamwambie amechemsha!
 
Ni upumbavu kuweka kitu cha Google hapa! ni kiwango gani cha hiyo sumu ndo kinakuwa na madhara kwa binadam, namaanisha katika kipimo cha ppm?
Soma "post" ya Mr Mtui uelimike na si swuala la "google". Tunaelimishana na wala siyo siasa wala udaku

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Nimesoma post zote zioni ushahidi wa utafiti wa kueleweka.

After one month nitakuja na majibu ya hili baada ya kuingia maabara mwenyewe.
 
Mold
 
Najua wewe si mwehu,wala Juha,Huenda labda ulichanganyiwa kiroba udanganye watu hapa,Hivi kwa sisi hapa namanyere tunaolima mahindi wenyewe hiyo sumu inatokea wapi,na je vipi kwa wanaoosha mahindi kabla ya kukoboa?Na utafiti wako hmefanyia wapi?

Hata mimi nilisikia mwaka jana TFDA wakiongelea kwenye TV, Kama mahindi ya dona yasipokaushwa vizuri na kuondolewa yale yenye ukungu ni hatari yanasabisha kansa.
 
Kabla sijakuuliza maswali Mengi...
Kwanza Hongera kwa POST NZURI...
Pili..hiyo sumu unajua inakaa muda gani kwenye mahindi?
Tatu Kwani ni mahindi yooote yanawekewa hiyo Dawa,all sources?
Nne yaani hiyo dawa inakaa kwenye Kiini tuuuuu?
Tano Je ni madawa yote kwa mimea ni hatari? mbona binadamu tunatumia "Superflaxon"
Sita...ni Kiwango gani ndo kinadhuru?
Ahsante Mkuu

monaco;
Hujaniuliza mimi maswali yako ila nataka tu kukujibu kwa sababu wengi wamevamia kwa kebehi uzi huu. Kwa sababu wanazo zijua wenyewe, wanataka kujitoa ufahamu. Ati, kwa sababu hatujamwona mtu akifa kwa sababu tu ya kula ugali dona basi hiyo sumu haipo. Naomba niseme yafuatayo:
Sumu hii huingia kwenye mahindi yalio vunda kidogo haswa wakati wa uvunaji. Ukiyahifadhi yakiwa na unyevu usio sahihi. Sasa, kwa kuwa wengi tunakula kwa mama lishe, wale ni watafutaji. Akikuta mahali bei imepungua kwa senti kidogo tu anauchukua kwa wingi ili aongeze faida yake.
Kumbuka, mahindi hayo yakianikwa huondoa ule uvundo na kuwa mazuri tu ila rangi inakuwa ya chungwa (yellow). Ukisaga, tiyari unga unakuwa mweupe. Haya, yalitakiwa yakobolewe kuondoa kile kiini.
Pumba ya mahindi ka hayo, huua mifugo (Kitimoto) haraka kuliko mara moja. Wataalam wa kilimo na mifugo njooni saidia hili.
Hatusemi ni yoote huua ila nikienda kununua pumba, nikiikuta ni yellow huwa naipita kwa mbaali. Si lazima huyo mdudu awepo lakini, mara nyingi sana ndiyo inakuwa hivyo.
Kama ni dona, nakula nilo tengeneza mwenyewe.
Wadudu "scania" alipoingia hapa nchini, watu wengi walitumia sumu mbalimbali kuzuia wadudu wale. Je, ni wangapi waliamini kuwa zile sumu zilileta saratani?? Watz kwa ubishi, hatujambo
 
Hata mimi nilisikia mwaka jana TFDA wakiongelea kwenye TV, Kama mahindi ya dona yasipokaushwa vizuri na kuondolewa yale yenye ukungu ni hatari yanasabisha kansa.
 
Nimesoma post zote zioni ushahidi wa utafiti wa kueleweka.

After one month nitakuja na majibu ya hili baada ya kuingia maabara mwenyewe.
Mimi mtoa mada nasubiri kwa hamu utafiti wako. Ni suala linalogusa afya na kwa jinsi ugonjwa wa kansa (km matiti, tezi,nk) ulivyo juu hapa nchini, ni vizuri kuwa na uhakika wa kiwango cha hiyo sumu na madhara yake. Kwangu bado ni tetesi, imenigusa.

CHAMBUA CHUNGUZA AMUA CHUKUA HATUA
 
Daaaah maisha ni magumu kama ni hivyo, ukichukua demu utaambiwa ukimwi, ukivuta sigara utaambiwa cancer, ukinywa konyagi utaambiwa livercirhosis, ukila kiti moto utaambiwa kisukali , shenzi kabisa sasa nimeamua sifuati tena maushauri yenu
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Ni wachache watakaokuelewa mkuu. Tatizo letu watu weusi ni wavivu sana
 
Back
Top Bottom