Unforgettable true story

comfix

Member
Joined
Feb 15, 2014
Posts
59
Reaction score
11
Wakati mwingine kuna matukio ambayo naamini huwa ni nadra kutokea.

Sikia hii: Siku moja nilisafiri kutoka Dar kwenda Mza kwa basi. Katika kiti cha mbele yangu alikaa dada mmoja mrembo, baada ya kufika Chalinze aliniomba nimwitie wale wachuuzi wa bidhaa ndogondogo kwani mimi nilikaa dirishani, baadae safari iliendelea na baada ya kufika Morogoro tulikwenda kupata chai ambapo tulisabahiana na kujuzana ni wapi tunaelekea, alisema anakwenda Nzega then Sikonge kikazi na angerudi baada ya kazi yake kukamilika.

Baada ya wiki mbili mimi nilirudi Dar nikiwa safarini tulipofika Nzega nilimwona yule dada akijongea kulikaribia lile basi nililokuwemo kisha akapanda, amini usiamini alikuwa amepewa seat # kwenye kiti nilichokuwepo mimi.

Tulisafiri km marafiki tukishirikiana kwa kila jambo, alishuka Morogoro na aliniahidi kuwa baada ya shughuli zake atakuja Dar kunitembelea, baada ya siku nne alinipigia simu nikampokee stand.

Nilimkaribisha na kuwa nae kwa siku mbili tulienjoy sana, kisha aliondoka kuelekea Arusha, tuliendelea kuwasiliana kwa simu na email pia, lakini ghafla nikawa simpati kwenye simu hata nikimtumia email hareply.

Sielewi ni nini kilimtokea ukizingatia nilikuwa nimekwisha mweka moyoni na akilini pia. Nasikitika kumpoteza Rachel.
 
Hizo siku mbili ulimgegeda au mlikuwa mkipiga stori za kawaida?
 
Hakuna tulichobakiza mkuu, ndio maana roho inaniuma kumpoteza.

kweli kizaz hiki kinaangamia kwa kukosa maarifa....... Nina was was na huyo mtu. Kuna dada mmoja anapiga sana route za mikoa anajifanya yupo kikaz ila ni mwathirika sasa chunga sana
 
Heee huyo namjua sana,muathirika shauri yako kachek afya.
 
Pole sana mkuu, siku nyingine usishoboke kiivyo.
 
Tangaza kwenye vyombo vya habar kwamba anatafutwa hahahahahaaaaa.

not seriously mkuu
 
Tamaa znakuua sasa.Hata rafki yangu alikufa Kwa uzembe kama huo.Iliniuma sana.
 
Mkuu hakukupiga mzinga kweli? Maana hii mitoto ya siku hizi kwa mizinga ni hatari.
 
Du Huyo Kazma Forever Na Kama Haukutumia Ili Kitu NETI bas anza kuangalia jua kwa mahesabu
 
Hahaha. Pole mwaya, safiri tena labda utabahatisha ingizo jipya.
 
loh! pole sana, nenda usafiri tena utamuona, ila tamaa mbaya utakufa siku si zako.
 

ulimweka rohoni?? alitoka mwenyewe au ulimtoa.pole sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…