Unene wa mke wangu unamuweka matatani

ze big

JF-Expert Member
Apr 27, 2015
382
350
Nilifanikiwa kupata mwenza wa maisha (kuoa) mnamo mwaka 2006 kipindi ninaoa mimi nilikua na uzani wa kilo 50 na wife alikua na kilo 42 maisha yalisonga tukapata mtoto wakwanza. Wife alijifungua normal kabisa na tukalea mtoto wetu wa kwanza wife alikua na kilo 44 mpaka mwanetu anafikisha umri wa miaka mitatu mwaka 2009. Tukafanikiwa kupata mtoto wa pili ambae Mungu si athumani wife alijofungua salama pia na mpaka mwanetu anafikisha miaka mitatu wife alikua na kilo zile zile 44.

Hatujawahi kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ila mnamo mwaka 2014 wife alianza kunenepa katika kipindi cha mwaka mmoja alitoka kilo 44 mpaka 76. Nilijitahidi kumshawishi japo kwa njia ambayo isinge mkwaza kua tuwe tunakimbia kimbia jioni wife akisikia swala la mazoezi anakua mkali nitanuniwa hata wiki tatu haongei yeye ni ku deal na watoto tu.

Ilipofika mwaka jana mwishoni wife alifikia kilo 95 kuna kipindi alikuwa anappata dalili za pressure tukaenda hospitali daktari alimshauri apunguze weight lakini alimgombeza daktari kama mtoto mdogo kua amuache yeye ni mtu mzima kama kumtibu ameshindwa aseme. Sikuwa na jinsi zaidi ya kua mpole na kupewa baadhi ya vidonge na kurudi nyumbani.

Mwezi uliopita wife amefika kilo 110 ambazo zinazidi kumuweka katika hatari yakupata magonjwa mengine ya hatari zaidi. Ameanza kukoroma kwa sauti kubwa sana usiku na akilala hataki umuamshe hata kama kuna kitu chochote kile amekua mkali sana na hata haki ya ndoa anasema anachoka sana skuizi ananipiga kalenda. Unene wa wife umekua ukinipa uoga na kumuonea mke wangu huruma sana hasa nikiona anapokua akilalamika miguu inamuuma.

Kuna siku nilijaribu kumwambia miguu inakuuma kwasababu ameongezeka uzito katika kipindi kifupi mno, hili lilizua ugomvi mpaka tukaenda kusuluhisha kwa wazazi baada ya miezi miwili ya kuvutiwa mdomo na kukosa amani ndani ya nyumba kwa kumshauri wife jambo la busara tu.

Kwa sasa nina kilo 54 wife anachezea 110 ninaomba ushauri nifanyeje wife anielewe na aweze japo kufanya mazoezi amekua kibonge sana na anapata matatizo ambayo yananiogopesha naweza kumpoteza mama watoto. Nilishawahi kujaribu kumshauri tujiunge kwa pamoja gym hilo ndilo lilizua maneno kuwa ninafuata wanawake huko gym namshangaa wife japo ni msomi ana masters yake ila haoni umuhimu wa afya yake.

Kitu kinachomfanya wife awe hivi ni kula kupita kiasi na kupenda sana vitu vya wanga kuna siku kulikua na birthday ya mwanetu alikula keki ya kilo tatu na ile sukari ya juu yote baada yakuwakatia watoto. Anaweza kutoka kazini akapita mahali akala hata kilo mbili za kitimoto, kuna siku nilimfuma anakula kitimoto bar kwa makadirio kilikua kama kilo 2 nikajaribu kudadisi nikagundua huwa ana desturi yakupita pale kila siku na ameweka oda kabisa na akifika nyumbani pia anafanya majukumu yake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapikia watoto na hula tena mara yapili na kulala akimaliza tu kula.

Ninaombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kunusuru afya ya mke wangu.
 
Haraka haraka nahis mkeo anatumia njia za uzazi kwa siri...yaweza kuwa vidonge au sindano..wamama weng hufanya siri hili jambo..mana si kwa unene huo wa ghafla
Sidhani maana kuna kipindi nilimshauri kuhusu suala hilo alininunia sana hakupenda na hata kushiriki nae mpaka leo tunashiriki katika siku salama
 
Hivi wewe si ndio nimetoka kuchangia thread yako unasema huwezi kudumu na mwanamke zaidi ya siku nne? Eti ukisha do naye hamu inakuisha?

Au ndo umeamua kutuchanganyia madesa?


Habari wana jamvi. Nimekua nikishangaa kila siku katika haya maisha kuanzia nmekua na akili yakuwatamani hawa wanawake. Nina zaidi ya miaka 35 lakini nimebakia kuwa mshangaaji inakuaje wanaume wenzangu mnaweza kudumu na wanawake kwenye mahusiano kwa mda mrefu!!!

Mnawezaje kuhimili kero za kila kukicha na mnawezaje kuishi nae asikuishe hamu kwa miaka kadhaa au ndo wengine huapia mpaka kifo. Mimi upande wangu nikishapewa tu vile via vya uz...zi baasi sitomrudia tena huyo mtu ananiisha ham kabisa na staki hata kumtia machoni sjawahi kuwa na uhusiani wa mda mrefu zaidi ya siku nne.

Mnawezaje wanaume wenzangu???

Imebidi tu nikaikopi...

Kumbe anatuuzia chai
 
Nilifanikiwa kupata mwenza wa maisha (kuoa) mnamo mwaka 2006 kipindi ninaoa mimi nilikua na uzani wa kilo 50 na wife alikua na kilo 42 maisha yaliso tukapata mtoto wakwanza. Wife alijifungua normal kabisa na tukalea mtoto wetu wa kwanza wife alikua na kilo 44 mpaka mwanetu anafikisha umri wa miaka mitatu mwaka 2009. Tukafanikiwa kupata mtoto wapili ambae Mungu si athumani wife alijofungua salama pia na mpaka mwanetu anafikisha miaka mitatu wife alikua na kilo zile zile 44. Hatujawahi kutumia njia yeyote ya uzazi wa mpango ila mnamo mwaka 2014 wife alianza kunenepa katika kipindi cha mwaka mmoja alitoka kilo 44 mpaka 76. Nilijitahidi kumshawishi japo kwa njia ambayo isinge mkwaza kua tuwe tunakimbia kimbia jioni wife akisikia swala la mazoezi anakua mkali nitanuniwa hata wiki tatu haongei yeye ni ku deal na watoto tu.
Ilipofika mwaka jana mwishoni wife alifikia kilo95 kuna kipindi alikua anappata dalili za pressure tukaenda hospitali daktari alimshauri apunguze weight lakini aalimgombeza daktari kama mtoto mdogo kua amuache yeye ni mtu mzima kama kumtibu ameshindwa aseme. Sikua na jinsi zaidi ya kua mpole na kupewa baadhi ya vidonge na kurudi nyumbani.
Mwezi uliopita wife amefika kilo 110 ambazo zinazidi kumuweka katika hatari yakupata magonjwa mengine ya hatari zaidi. Ameanza kukoroma kwa sauti kubwa sana usiku na akilala hataki umuamshe hata kama kuna kitu chochote kile amekua mkali sana na hata haki ya ndoa anasema anachoka sana skuizi ananipiga kalenda . Unene wa wife umekua ukinipa uoga na kumuonea mke wangu huruma sana hasa nikiona anapokua akilalamika miguu ina muuma. Kuna siku nilijaribu kumwambia miguu inakuuma kwasababu ameongezeka uzito katika kipindi kifupi mno hili lilizua ugomvi mpaka tukaenda kusuluhisha kwa wazazi baada ya miezi miwili ya kuvutiwa mdomo na kukosa amani ndani ya nyumba kwa kumshauri wife jambo la busara tu.
Kwa sasa nina kilo 54 wife anachezea 110 ninaomba ushauri nifanyeje wife anielewe na aweze japo kufanya mazoezi amekua kibonge sana na anapata matatizo ambayo yananiogopesha naweza kumpoteza mama watoto. Nilishawahi kujaribu kumshauri tujiunge kwa pamoja gym hilo ndilo lilizua maneno kua ninafuata wanawake huko gym namshangaa wife japo ni msomi ana masters yake ila haoni umuhimu wa afya yake.
Kitu kinachomfanya wife awe hivi ni kula kupita kiasi na kupenda sana vitu vya wanga kuna siku kulikua na birthday ya mwanetu alikula keki ya kilo tatu na ile sukari ya juu yote baada yakuwakatia watoto. Anaweza kutoka kazini akapita mahali akala hata kilo mbili za kitimoto kuna siku nilimfuma anakula kitimoto bar kwa makadirio kilikua kama kilo 2 nikajaribu kudadisi nikagundua huwa ana desturi yakupita pale kila siku na ameweka oda kabisa na akifika nyumbani pia anafanya majukumu yake vizuri ikiwa ni pamoja na kuwapikia watoto na hula tena mara yapili na kulala akimaliza tu kula.
Ninaombeni ushauri ndugu zangu nifanyeje kunusuru afya ya mke wangu ....
Mpwandiooo ugonjwaa wetu rushaa kifurush
 
Back
Top Bottom