Hujajibu swali langu! Bunge ni eneo huru-- wabunge wanatoka vyama mbalimbali na ni muhimili unaojitegemea na spika anaweza kutoka chama chochote kile. Si hivyo tu, mkuu wa bunge ni spika na sio rais lakini pamoja na yote hayo alielekeza pesa za kuwapongeza wabunge ziende Muhimbili na zikaenda! Nampongeza kwa hilo! Sasa ikiwa eneo ambalo lina watu wenye itikadi tofauti tofauti tu alielekeza pesa kutoka kwa watu binafsi ziende kwenye huduma za kijamii; how come tena ashindwe kuelekeza pesa za CCM ambazo na yeye mwenyewe ni mwana-CCM na serikali ni ya CCM na 100% ya wahusika ni CCM?!Wazo la kubana matumizi ni la Magufuli na sio CCM na wala halipo katika ilani ya CCM na ndio maana CCM hawabani matumizi. Labda hilo litawezekana endapo Magufuli atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CCM lakini sio vinginevyo.