Unazikumbuka enzi za Barua! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Unazikumbuka enzi za Barua!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Safety last, Jun 2, 2011.

 1. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Leo kuna njia mbalimbali za kuwasiliana ila kile kipindi tunaandikiana mabarua ",....kwako wewe uliyembali sijui na upeo wangu..,,.....," dhumuni la barua hii......"jamani barua (sio kadi) zimepoteza mvuto??? au ndo kwenda na wakati!
   
 2. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Hahahahhah
  dahhh kipindi cha barua kilikuwa
  na raha yake dear.... sanasana zile
  za shule ya msingi mnapeana
  chini ya dawati....

  dahhh unanikumbusha mbaliiiii
   
 3. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Hahaaaaa, umenifanya nichangie fasta hii thread maana juzi nilikua nawafundisha wanafunzi wangu mahali fulani nikawaambia kuwa hawajui kuandika essay kwasababu wao siku hizi wanategemea sms ambazo zimefupishwa kiasi kwamba huwezi jua hata maana yake. Enzi hizo nipo pale Magamba Boys now ( SeKUCo- Sebastian Kolowa University College-Lushoto) ndio nilikua nafanya dili za kuwaandikia washkaji barua halafu wananilipa....serious nilikua bingwa wa kuandika hizo barua hasa kwa lugha ya kigeni maana zilikua zinaenda Mazinde Juu ( St.Mary's) au Kifungilo Girls' ambako ndio by then kulikua na watoto wakali kinoma na ngeli inapanda sana, sasa ukiaka uwapate lazima uandike barua kwa kiingereza.

  Nilikua naenda kununua karatasi maalum za kuandikia barua za mapenzi halafu nawauzia jamaa, kisha kama nitaandika Mimi hio barua inabidi uongeze dau! Ndio maisha yangu yalivyokuwa, huwezi kwenda kununua kadi bila kupata ushauri wangu.....next time nitawaeleza kisa nilichokifanya kwa mshkaji aliekua anataka nikamnunulie Card amtumie Demu wake pale Mazinde Juu.

  Barua zilisaidia sana kuweza kuandika essay zenye maana na kanuni za uandishi zilizingatiwa......Umenikumbusha mbali saaaaana
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,816
  Likes Received: 10,106
  Trophy Points: 280
  Sisi tulikuwa boarding hivyo kila jumapili tukienda kusali ndio muda muafaka wakubadilishana hizo barua, nakumbuka hata waislamu ilibidi wawe wanaenda Church kule Oaklands kwa R.C na Magamba Coast kwa Walutheri.......hahahaaa, nimekumbuka mbaaaali sana. Tulikuwa tunafua, kunyoa na kupiga pasi jumamosi hadi basi hasa viongozi wa UKWATA watutatangazie kuwa jumapili hii kanisani watakuja wageni toka Kifungilo au Mazinde Juu, Lwandai hawakuwa na dili sana maana ili ilikua ni mchanganyiko ila Mazinde na Kifungilo ni single for girls na Magamba ni for Boys.....patamu hapo.
   
 5. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  nimeziandika sana nikiwa sec .siku zikisomwa assembly usipopata unajiskia vibaya
   
 6. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  broo i love letter mwanamke anayendika barua kwangu huwa namheshimu sana
   
 7. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Barua za mapenzi zilikuwa nzuri na za kusisimua zaidi kuliko meseji za simu, kwa sababu.

  1. Mtu alikuwa anaandika kitu alichokibuni kutoka moyoni
  2. Barua ilikuwa na michoro ya kusisimua yenye ishara za mapenzi
  3. Barua ilikuwa ndefu haaishi hamu
  4. Wakati mwingine ilikuwa na nyongeza ya mashairi au nyimbo za wakati ule ambazo zilikuwa zinasisimua sana sio hizi za sasa eti demu wangu, demu wangu sijui kachakachuliwa aaah!
  SIMU HAZINA UTAMU

  1. Mapenzi yake ni ya kompyuta yaani mtandao unatengeneza meseji za mapenzi wewe unatuma tu.
  2. Ujumbe wake ni mfupi sana na hauingii moyoni
  3. Ubunifu wa maneno matamu ya mapenzi unakuwa mdogo kwa sababu yanakuwa mafupi mno.
  4. Watu hawabuni kutoka moyoni ndio maana meseji ya aina moja unaweza kutumiwa na watu kumi tofauti Natamani zama za barua zirudi tena.
  5. Halafu unajua tu kuwa hizi ni kamba za mtandao
   
 8. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  men thats true ila sikuhizi madem wanasema ar you on facebook,twitter or ..!zamani unaomba box number ni lazima ukienda shule utafute bahasha ambazo ziko sex
   
 9. GAZETI

  GAZETI JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 3,524
  Likes Received: 1,005
  Trophy Points: 280
  Dah! umenikumbusha mbali mpaka nacheka yuko rafiki yangu mmoja kwa sasa yuko mjengoni. Tukiwa primary yake ilikamatwa na kusoma kwenye paredi. Sehemu ya maneno ilisomeka hivi " Nakupenda sana vick miguu yako mizuri kama cherehani...." Mwalimu akawauliza hivi ninyi wasichana munaambiwa miguu kama cherehani bado munafurahia? Shule mzima iliangua kicheko. Ilikuwa ni gumzo siku inayokamatwa barua ya mapenzi, lazima isomwe kwenye paredi.
   
 10. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  ha ha ha ha ha, sisi kulikuwa na mtu kutuma kama jenga ukwata au YCS !kuna jamaa aligonganisha madem kwenye shule moja wakamwandikia barua moja wote wakijieleza it was funny!
   
 11. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sikubaliani na wewe kwa jinsi ulivyoanisha kwamba kwa text huwezi kubuni/jaza hisia kama ilivyo kwa barua.Binafsi hua naandika text/email ndefu mpaka nashangaa na sio copy n paste mind you.We sema siku hizi watu ubunifu haupo kiwango...hata ingekua lwa barua bado tu wangeandika mistari kadhaa au mingi isiyotoka moyoni(yakuambiwa).Kwahiyo tatizo hapa sio njia ya mawasiliano bali ni watu wanavyowasiliana!!!
   
 12. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  lizzy ndo uyo ninae kufaham au mwingne? maana kwa umri wako cdhani kama umeandika hizi barua! maana umekulia kwenye simu. au?
   
 13. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #13
  Jun 2, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  hata ivyo umenikumbusha mbali sana! nilikuwa na binti mmoja anasoma uganda basi palikuwa hapatoshi. barua zilikuwa znawekewa poda au marashi yanayonukia. barua zilikuwa tamu usiseme! ukisoma iyo barua utadhani unamwona, na siku ukiipata barua utaisoma hata mara ishirini kwa siku! ful kuwatambia wenzio ukipata barua.
   
 14. Gaga

  Gaga JF-Expert Member

  #14
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,565
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  Mie nakumbuka enzi zetu kuna vikaratasi vya kuandikia barua tulikuwa tunanunua tahfif vinanukia hatari na vibahasha vyake, uko radhi u save pesa ya matumizi shule ili ukanunue hiyo kitu
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Mmh mwenzenu juzi tu nimemwandikia wa ubani wangu barua ya mkono!

  Alipoipata, kiodgo apagawe,.....hatukulala!
   
 16. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #16
  Jun 2, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mimi mimi unaenijua....
  Nimeandika kiasi japo sio za mapenzi!!Btw kuna kitu nataka kukuuliza...
   
 17. G

  Gathii Senior Member

  #17
  Jun 2, 2011
  Joined: Feb 9, 2011
  Messages: 164
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lizzy,
  najaribu ku-comment majibu yako kwa "GAZETI"
  Nakubaliana na wewe kitu kimoja-kwamba ile ladha ya ujumbe hata kwa sms au email inaweza kuwepo ileile kulinganisha na barua-what matters ni muandishi,maana kuandika ni sanaa,lakini bado ukiandika toka ndani ya moyo kuna uzito wake.

  Ila nakubaliana na woote waliopita kuwa bado "barua" kama kitu ambacho ni "tangible" na mazingira yake yanayoambatana toka inaandikwa na muandishi na mpaka inafika kwa mlengwa (msomaji) na vitu kama michoro,aina ya karatasi,handwritings na ile hali tu ya kuisubiri ilikuwa ina uzito na utamu wa kipekee kabisa...Niliandika chache back in days,hazikuwa za mapenzi lakini i still miss letters.

  I beg to submit!
   
 18. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #18
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,192
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  mi hizo barua nakumbuka zilivyokuwa zinanizingua,
  mshiko unaisha, unatuma barua nyumbani kuomba pesa wanajifanya kama hawajaipata vile dah...
  demu wangu alikuwa hanitumii barua na mm simtumii tunakutana mwezi wa6 na disemba kitaa.
   
 19. J

  Jibaba Bonge JF-Expert Member

  #19
  Jun 2, 2011
  Joined: May 6, 2008
  Messages: 1,224
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Duu Umenikumbusha mbali sana. Hata kampuni ya Posta walikuwa wanatudangaya - wanatuuzia airform (karatasi ya kuandikia barua ambayo ni bahasha hiyohiyo) halafu imeandikwa " ukiweka kitu chochote ndani, haitasafirishwa kwa ndege" sasa sijui vijijini ndege zilikuwa zinatua wapi?

  Halafu kwenye barua unaandika ' salaam zikufikie hapo ulipo, ama baada ya salaam je u hali gani? Upendapo kujua hali yangu mimi ni mzima wa afya njema hofu na mashaka ni kwako uliye mbali na upeo wa macho yangu! haa haa haa du.
   
 20. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #20
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,654
  Trophy Points: 280
  Ebanaeee mkuu acha tu,ila kuna jamaa mpaka leo huwa anamuandikia dem wake barua anasema zina raha yake!
   
Loading...