Unawezaje kumsamehe mwanaume aliyekusaliti kwa kumleta mwanamke mwingine nyumbani mnakoishi?

Mathew 18:21 Kisha Petro akaja kwa Yesu akamwuliza, “Bwana, ndugu yangu anikosee mara ngapi nami niendelee kumsamehe? Hata mara saba?” 22 Yesu akamjibu, “Sikuambii mara saba, bali saba mara sabini.”
Nakazia
 
Yani Najikuta nakosa raha kabisa. .hata sina hisia nae kabisa sikuhizi
Hiyo haitakaa ikutoke kichwani maana ni bora angefanya huko mbali ila alikudhalau mpaka akamua kuleta mchepuko ndani.Mm na kufanya ujinga wangu sio siri naheshimu sana tunapolala na mke wangu ama makazi
 
Pole sana, msamehe endelea na maisha kupata mwanamme ambayebm hacheat ni ngumu sana sasa hivi, tumebaki 9 hapa Tz lakin namie naenda kushindwa sio muda hivyo watabaki 8
mkuu njoo kwenye chama letu la kutotuma na ya kutolea chaputa ....mwenyekiti bado anasajili.
 
Pole Sana mamiloo, Kama unamsamehe msamehe kwa moyo mmoja usibebe fundo ama kuwa unamkumbushia kumbushia,, jitahidi hisia zisife walau kaonyesha kujutia komalia kuwaza hilo ili kubembeleza hisia, lakini zikishafifia ndo basi tena huwaga hazifufuki na utaishi kwa kisasi,, utateseka sana naandika haya kwa uzoefu,, msamehe kwa moyo mmoja ukishindwa muache😥japo inauma Sana sana
 
Unajua nini kaka,, kwako ni kwako tu. Niliporudi the same day niliona mabadiliko hapo nyumbani ambayo yalinipita wasiwasi mkubwa! Yani kulikua na vitu tofauti na nilivyoviacha mimi pia katika kufanya usafi mara nikute cheni . Kuna vyombo vyangu vingine nilikua sivioni. Nguo yangu fulani hivi ( kikoi) pia sikuvikuta sasa kumuuliza hanyooshi maelezo dah..
Cha muhimu we njoo pm nikushauri kitu kizuri cha kufanya uweze kumsamehe jamaa na upuuzi wake!
 
Kazi Ndugu.. nilienda kufanya kazi kuongeza pato!!
Me nataka kujua hali ya mawasiliano na mme wako huwa ikoje kabla ya hili tatizo? Nimekwambia njoo PM ila naona kama unachelewa!

How have you guys been interacting hapo ndani before the incidence!? Unajua kuna wakati huwa wanawake mnakosea sana halafu mna expect kwamba mwanaume ni mbuzi tu ata swallow your bullshit! Baadhi yetu hatunaga huo ujinga at all!

Jamaa unaweza kuwa ulikuwa ukimfanyia drama na kujikuta we ndio wewe with flirting around na watu wengine na kumletea dharau huku ukim deny sex na kujifanya uko busy na kazi daily unamtoa mswaki akitaka tunda mpaka mkabane kabane! Hilo halipendezi kwa mwanaume na kama atakuvumilia ni kwa muda tu.

Aidha jamaa alishakususpect unamchiti ila uka capitalize kwenye ile kauli ya “huyo wala sina mpango nae”...”Tatizo lako hujiamini wewe”...Yamkini amehangaika sana na kujaribu kukwambia tabia hio inamkera ukawa unaona raha anavyolalamika mwisho ameona bora nawewe akunyooshe tu. Very likely!

Hebu kuwa honest useme tu huwa unam treat vipi! Kuna wanawake kazi kwenu ndio mume ukifika home mume unamuona kidampa tu!
 
Likely
 
Asante Nimepata kitu hapa! Shukrani
Habari ndugu, kwanza nikupe pole na pongezi maana kama mpaka sasa hivi bado uko ndani ya ndoa basi huo mtihani umeshaushinda kaa tulia.
Fahamu kuwa hata ukisema uachane n huyo bado uendapo hutompata mkamilifu badala yake pengine ukaingi kwenye majanga kuliko hayo ya sasa.
Mwanaume akishakuoa na kukuweka ndani ju kuwa huyo amekukubali kwa vigezo kabisa hivyo hatabkama ataonja onja huko nje jua kuwa shibe yake haswa ni nyumbani kwake.
Usifikirie kuchepuka kulipiza kisasi utafeli zaidi, dereva wa mbele ako akipitea njia akaingia mtaroni kamwe na wewe usiingie huko zaidi simama mpe msaada.
Cha kufanya kwa sasa muite, mwambie kuwa umemsamehe lakini mueleze kwa utulivu namna alivyokuumiza.
Kamwe usifoke, mwanaume hana uwezo kihisia wa kuvumilia kufokewa hivyo mueleze taratibu kish achana nae apate muda wa kutafakari.
MWISHO mvizie akiwa amelala ila sio usingizi mzito kisha anza kumuombea ukitaja madhambi yake yote nanumuombee Mungu amsamehe kama wewe ulivyomsamehe. Ukimuombea hivyo na akasikia unavyoomba akili y mwanaume imejaa mantiki/logic itamsumbua sana kichwani n itapunguza uwezekano wa kurudia tena.
KUPATA NASAHA, MASOMO NA ELIMU YA MAHUSIANO BORA NICHECK PM NIKUPE GROUP LINK YA WATSUP UTAJIFUNZA MENGI HUKO.
Karibu
 
"Aliponiona alishtuka!"

Kuna uwezekano mumeo kashampiga chini, otherwise asingekuja wakati upo...

Kuna uwezekano pia, alishakuwa huru sana na mumeo na sasa ametaka kuwa huru na hapo kwenu...

Pia kuna uwezekano kwa akili zenu wadada/wanawake, alikuja makusudi ili tu umuone, ujue huyo ndio bi mdogo

Again, tafuta kujua kwa nini mumeo ameleta mbususu ya kando home kwenu...
Kuna uwezekano alidanganywa bwana hajaoa, au kaachana na mkewe. Nyie watu nyie
 
Evidence zinatosha kabisa nyingine sijazisema tu na mbaya zaidi siku nimefika tu huyo mwanamke siku kama ya 3 alikuja Akanikuta nje ya nyumba napika huku nimevaa shati la bwanaetu niseme . Aliponiona alishtuka sana kaniangaliaaaaa hajasema kitu akaondoka .
Kwahio jamaa kambato jirani kabisa hapo😅 hapa nimeelewa kwanini jamaa alifanya importation of goods😅!

Angekuwa mwanamke wa mbali isingekuwa rahisi hivyo msamehe bana! Unajua sometimes hata nyumba za kupanga zinashawishi imagine member wa kwenye apartment jirani alimtega jamaa na ukizingatia genye zetu za fasta akaona amvute rum amuweke usiku ambao ulikuwa haupo. It has alot to do na wivu wa kike wa huyo jirani kutaka kujua wewe unafaidi nini!

Jamaa kukiri maana hio ilitokea bahati mbaya basi bila shaka! Msamehe jamaa bana ila kama ingalikuwa ni mwanamke kamtoa mbali ningekusihi usimsamehe. Wa hapo hapo jirani ni vitamaa vya kiume tu vimemponza ila ingekuwa mwanamke wa mbali ingalikuwa makusudi kabisa.
 
Kuna baadhi yetu wanaume ni wapumbavu sana,unapelekaje malaya nyumbani?kabisa unakoishi na mke na watoto unaokota mwanamke unaenda kulala nae humo?na anadhihirisha upumbavu wake kwa kukiri kufanya hayo!

Ni pombe au kitu gani!!!
Kweli kafanya Jambo la kijinga Sana..pamoja na ujinga wetu wanaume lakini binafsi siwezi kufikika kiwango hiki Cha upuuzi.
 
Back
Top Bottom