Unawezaje kukata kodi pesa ambayo mtu ameihifadhi hajauza kitu?

themagnificient

JF-Expert Member
Dec 13, 2016
988
3,318
Yaani kwa sasa wameshakopa sasa wamefikia kikomo wanatafuta mahali pa kukamua kuendana na hayo madeni, ni mwendo wa kubuni kodi za vichwa sasa maana huwezi kata kodi akiba ya mtu ambayo hajaifanyia kazi or kuuza kitu hiyo sio kodi badi ni unyang'anyi.

Umemuingizia mshahara mtu umemkata kodi, kisha anaenda kuitoa pesa yake unadai unamkata kodi nyingine pesa ambayo hajauza kitu wala kuifanyia biashara ni yake ila umemkata kodi, na akiipeleka kwenye Biashara unataka kodi nyingine tena sasa kwa mwendo huu kuna mtu anatataka kulipa kodi TRA wakati kashakamuliwa kwenye miamala huko.

Lameck ajitafakari kumshauri mama njia nzuri za kukusanya mapato hivi wanazidi kuharibu mbona awamu zote zilizopita haya mambo ya unyonyaji hayakuwepo na nnchi ilienda?

Mnawakaba wananchi alafu mmeacha uchochoro wa bidhaa za Kichina zinaingia nchini kama utitiri nyingi hata hao TBS na TRA hawazijui ila zimejaa nchini kila kona zinauzwa, yaani wachina na makampuni ya wahindi kama wangebanwa ipasavyo hizi kodi za ajabu ajabu zisingekuwepo.

Laiti tungezingatia rasilimali zetu kuanzia madini na mambo mengine tungeuza nnje kwa wingi tusingekuwa tunasumbuana hivi, ogopa sana kununua bidhaa nnje alafu wewe hauuzi ni hatari mwisho wa siku utabaki na idea ya kukamua wananchi.
 
Tumeanzisha miradi mikubwa wenyewe kuwa tunaweza, sasa Kwann unataka wafanyabiashara tu ndo waumizwe na kodi ili miradi ikamilike?

Serikali inajitahidi kuchukua kodi halali kutoka kwa wafanyabiashara bila kuwaumiza kama hapo nyuma na wananchi nao wachangie kodi za maendeleo.

Hayo mambo ya mfanyabiashara ndo akamuliwe mpaka kufungiwa imeamua kuachana nayo maana imeshaona athari zake.
 
Umemuingizia mshahara mtu umemkata kodi, kisha anaenda kuitoa pesa yake unadai unamkata kodi nyingine pesa ambayo hajauza kitu wala kuifanyia biashara ni yake ila umemkata kodi, na akiipeleka kwenye Biashara unataka kodi nyingine tena sasa kwa mwendo huu kuna mtu anatataka kulipa kodi TRA wakati kashakamuliwa kwenye miamala huko
Mwisho wa kuwaza na kufikiri kwao ni umegotea hapo ndugu! Yaani wanajiita wachumi ndio wanafanya huu utopolo tutafika kweli? Mshahara wa mtu mmekata PAYE halafu kwenda bank kuchukua mnakata tena? Shame!
 
Mnawakaba wananchi alafu mmeacha uchochoro wa bidhaa za kichina zinaingia nchini kama utitiri nyingi hata hao TBS na TRA hawazijui ila zimejaa nchini kila kona zinauzwa , yaani wachina na makampuni ya wahindi kama wangebanwa ipasavyo hizi kodi za ajabu ajabu zisingekuwepo.
Hatutaki kuwaudhi wawekezaji wataondoka, wacha tuwakamue nyinyi mtalalamika siku mbili tatu halafu maisha yataendelea.
 
IMG_5011.png

Gharama za vikoba
 
Acha mkatweee tuuu na ndo mtapata akili ya kuwakata kwenye kisanduku cha kura!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom