Unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,909
2,889
Nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya Magufuli na wenzie. Hivi jamani ni nani kawadanganya kuwa kufukuza mtu kazi ni mafanikio?

Hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? Mimi nadhani tungesubiri tuone matokeo kwani timua timua ndio ilikuwa fasheni ya Mwakyembe na Sitta walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuzi hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha.

Je, ile fukuza fukuza ililenga nini? Ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa Magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu.
 
Siku zote mtu anafanya kazi na mtu anayeendana na kasi yake. Private sector inafanya vizuri kuliko public sector kwa sababu nyingi moja ikiwa kukosekana kwa job security. Mwajiriwa ukifanya blunder hakuna msalia mtume...ni kutimuliwa tu.

Ikiwa hulijui hili....basi baki na upumbavu wako. Sio lazima wote tuelewe nia njema ya rais Dkt Magufuli ya kutuletea wananchi maendeleo.
 
Mkuu,
Ukiona malalamiko na vilio Ujue Jipu limeshaiva anaogopa appointment ya kumuona mpasuaji.
 
Hakuna cha mfumo wowote. Kinachofanyika ni kupangusa vumbi kwa misingi ya sifa na propaganda. Kwa kuwa majuha ni wengi, wala hawana ufahamu wowote, wanasifia wakidhani hikikitu kina misingi ya kuendelea.

Hakuna kitu hapa. Ni sanaa tu!
 
nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya kina magufuli na wenzie hivi jamani ni nani kawadanganya kua kufukuza mtu kazi ni mafanikio?? hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? mi nazani tungesubiri tuone matokeo kwani timuatimua ndio ilikua fasheni ya mwakyembe na sita walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuz hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha je ile fukuzafukuza ililenga nn? ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu kama mazuzu

Ukiona hivyo, basi ujue wewe ndiyo mpuuzi na siyo wengi!
 
Mwizi mwachie ATM card yako, nina hakika utapata mafanikio!!
 
Khaa!! Kama kazi yako huwezi kuifanya ulivyoagizwa kuna sababu gani ya kuendelea kuwepo kazini?? :mvutaji:
 
Awamu ya nne wizi na wakwepa kodi walivumiliwa na matokeo yake tumeyaona.

Hii ni awamu ya tano na mtazamo tofauti. Tuipe muda awamu hii.

Sehemu zote ambako wamefanikiwa hawacheki na wezi na wakwepa kodi. Mifano ipo lukuki. Serikali yoyote inayovumilia wakwepa kodi ni mafisadi. Hilo halina mjadala.
 
Siku zote mtu anafanya kazi na mtu anayeendana na kasi yake. Private sector inafanya vizuri kuliko public sector kwa sababu nyingi moja ikiwa kukosekana kwa job security. Mwajiriwa ukifanya blunder hakuna msalia mtume...ni kutimuliwa tu.

Ikiwa hulijui hili....basi baki na upumbavu wako. Sio lazima wote tuelewe nia njema ya rais Dkt Magufuli ya kutuletea wananchi maendeleo.

Umekuwa wa kwanza kuchangia na umetoa mchango mzr saana. Binafsi sijawahi fanya kazi serikalini lkn nimefanya private. Ulichosema ni sahihi. Huku job security ni uwezo na mchango wako kwenye shirika au kampuni. Aliyeanzisha mada afanye utafiti kwanza. Kuna wafanyakazi ni mizigo. Wengine ni wazembe na wengine ni wezi. Pia wengine wanafanya kazi kwa mazoea. Dawa ya wapuuzi kama hao na mwanzisha uzi huu ni kuwatimua kabisa.
 
Siku zote mtu anafanya kazi na mtu anayeendana na kasi yake. Private sector inafanya vizuri kuliko public sector kwa sababu nyingi moja ikiwa kukosekana kwa job security. Mwajiriwa ukifanya blunder hakuna msalia mtume...ni kutimuliwa tu.

Ikiwa hulijui hili....basi baki na upumbavu wako. Sio lazima wote tuelewe nia njema ya rais Dkt Magufuli ya kutuletea wananchi maendeleo.

Mkuu kuna mijitu kichefuchefu humu jamvini!! Hata haielewi utendaji kazi wa Ikulu unakwendaje, inafikiri Magufuli akiamka tu anaenda kufukuza mtu kazi!!
 
Hakuna cha mfumo wowote. Kinachofanyika ni kupangusa vumbi kwa misingi ya sifa na propaganda. Kwa kuwa majuha ni wengi, wala hawana ufahamu wowote, wanasifia wakidhani hikikitu kina misingi ya kuendelea.

Hakuna kitu hapa. Ni sanaa tu!
Maneno ya kweli kabisa. Tunataka watanzania wafanye kazi, siyo wafukuzwe kazi. Kama kiongozi umeshindwa kuhakikisha watu wako wanafanya kazi, nawe umeshindwa kufanya kazi, ujifukuze kazi basi. Kazi si za maofisini tu. Je, wananchi wa kawaida wasipofanya kazi atawafukuza nani???
 
Hili ni swali kuntu sana , unajua mimi nilivyoona sitta amemtimua madeni kipande nikajua mchezo umekwisha , kumbe wapi ! Sasa tusubiri kitakachojiri .
 
Kwa hiyo kama mtu kaharibu aachwe tu ili iweje?!
Kufukuza watu kazi ni sehemu ya mkakati mpana wa kurejesha ufanisi katika utumishi wa umma.
JPM ilibidi aanzie mahali; sasa wale ambao 40 zao zimeshakita na madudu yao yako wazi ndio halua ya kuanzia!

Nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya Magufuli na wenzie. Hivi jamani ni nani kawadanganya kuwa kufukuza mtu kazi ni mafanikio?

Hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? Mimi nadhani tungesubiri tuone matokeo kwani timua timua ndio ilikuwa fasheni ya Mwakyembe na Sitta walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuzi hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha.

Je, ile fukuza fukuza ililenga nini? Ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa Magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu.
 
Hakuna cha mfumo wowote. Kinachofanyika ni kupangusa vumbi kwa misingi ya sifa na propaganda. Kwa kuwa majuha ni wengi, wala hawana ufahamu wowote, wanasifia wakidhani hikikitu kina misingi ya kuendelea.

Hakuna kitu hapa. Ni sanaa tu!

mtasubir sana na sanaa zenu.....sisi ni kazi tu!!!
 
Nawaskia watu wengi kwa maelfu wakubwa kwa wadogo wakisifia timuatimua ya Magufuli na wenzie. Hivi jamani ni nani kawadanganya kuwa kufukuza mtu kazi ni mafanikio?

Hivi unaweza pata mafanikio kwa kumfukuza mtu kazi? Mimi nadhani tungesubiri tuone matokeo kwani timua timua ndio ilikuwa fasheni ya Mwakyembe na Sitta walipofanya kazi kunako wizara ya uchukuzi hata hivyo tumeshuhudia maovu ya kutisha.

Je, ile fukuza fukuza ililenga nini? Ni kwa hoja hii nashauri tusubiri tuone ikiwa Magufuli ataweza kuleta mfumo madhubuti utakaodhibiti kabisa wizi na upotevu wa mapato hapo bandarini na kwingneko na si kushabikia tu.

- Ni kawaida sana kwa nchi zilizondelea Utawala mpya unapoingia utawala wa zamani unaondoka na wote, so ni kawaida it does not matter about anything ila mabadiliko ni mabadiliko wa zamani wote wanaondoka wanakuja wapya.

le Mutuz
 
pumba at its peak!?
 
Kikwete aliwavumilia wezi,mafisadi akalaumiwa akaitwa dhifu JPM hana uvumulivu na wezi,wazembe,mafisadi naye analaumiwa.

Sijui tunataka nini.
 
Back
Top Bottom