Unaweza mpenda mwanamke bila kumtamani???

Unaweza mpenda mwanamke bila kumtamani???

bona

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2009
Posts
3,798
Reaction score
1,444
Nimeichukua hii remarks kutoka kwenye uzi hapa hapa... nadhan kuna haja ya kujadili hii kauli ya kina dada baada ya kumtongoza anakuajibu umenipenda au unanitamani tu? je inawezekana kumpenda mtu bila kumtamani? binafsi nadhan huwez mpenda mtu bila kumtaman lakini as a word of caution kwa wanaume kama ukitongoza ukijibu umetaman hutakubaliwa!!!
 
Fafanua kwanza maana ya maneno "kutamani" na "kupenda"?
 
ha haaa hadi umeanzisha uzi naona
cc mimi49 ...
 
Last edited by a moderator:
huwezi kwa kifupi

mwanaume kupenda na kutamani vinaenda pamoja
unless umpende mtu kama dada na kaka
 
Hii imenikumbushA kitchen party moja mc alimuuliza bibie mtarajiwa kuwa mchumbake kampendea nini akajibu tabia...
MC akipinga vikali akadai kuwa mwanaume anakuona halafu anakutongoza hyo tabia kaionea wapi..
Akadai kuwa lazima kuna kitu katika maumbile yako au sura mwanaume amekiona akakitamani kinachomshinikiza kuwa na huyo mwanamke...akasisitiza mwanaume anatamani kwanza ndio apende...
Sasa swali linakuja ipi tofauti ya KUPENDA na KUTAMANI
 
huwezi "kumpenda" mwanadamu mwenzio awe mwanamume au mwanamke bila "kumtamania"...!
 
hakuna kupenda bila.ya kutamani. ikitokea una mke hujawahi mtamani ujue huyo ni kama mwajiiwa wako umempa ajira. yaani humtamani hata kidogo? mimi paka nitamani ndio nianze kupenda labda penzi hilo liwe la kaka na dada.
 
Sista kwa mfumo wa sasa wa maisha hilo nigumu sana. ilikuwa posible kipindi hiyo ya kuchaguliwa mke wazee wanakukabidhi mke/mme washa mfanyia screening mpaka ya vinasaba vya ukoo kwamba havina chembechembe za wizi wala magonjwa ya kurithi. wewe kazi yako kupenda tu. kipindi hiki chetu tunakutana njiani, kwenye mitandao n.k chakwanza ni kutamani. kila mtu anapicha yake kichwani ya mpenzi anayemtaka ingawaje not necessarily kwamba atampata, infact wachache wanabahatika kupata wapenzi wenye sifa zote wanazo.zitaka.So wapo wanaoinvia kwenye ndoa kwasababu wanaona muda unaenda sio kwamba wamepata their soul mate. sasa siku ambabatize mahali! utajuta kuolewa, lazima akusahau kiaina.
 
Mim huwa napata wakati mgumu sana mwanamke anaponiuliza umenipendea nin??
 
Umeona eeh!!! unaona binti ana mvuto wa uhakika humjui hakujui. Hujui kama ana tabia nzuri au la lakini kwa mvuto aliokuwa nao unaamua kupiga speed. Ukikubaliwa na baada ya kumfahamu kwa kina na kufurahishwa na tabia zake hapo ndio unaanza kumpenda na si ajabu kutaka muda mwingi kadri ya muda wako unavyokuruhusu kuwa naye.


huwezi "kumpenda" mwanadamu mwenzio awe mwanamume au mwanamke bila "kumtamania"...!
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom