Unaweza kumsomesha mchumba wako?

dada yangu anasomeshwa chuo tangu 1st year na mwakahuu anamaliza st. john! na kibunda cha matumiz anapewawa vizuri tu! ukiwa na imani kila kitu kinawezekana
 
Aisee ndugu nakushauri wekeza kwingne sio kwa mwanamke mana hawana utu hata chembe akishafanikiwa kukubwaga kawaida.
 
Kusomesha ngoja kwanza wazazi wake wamsomeshe hadi atakapofikia.
 
we saidia tu mkuu, utalipwa mbinguni
 


hapo huwa hakuna guarantee kama umeamua kumsaidia we msaidie tu, lolote linaweza kutokea
 

Wengi waliosomesha wachumba wao wameambulia patupu. Kwa nini usioe ndio mambo ya kusoma yafuate? Najua tatizo wengi huwa ni shida kupangilia mambo yao maana baada ya ndoa kinachofuata ni mimba na huwa mwisho wa hadithi ya shule. Kwa wenye mipango na msimamo thabiti inawezekana!
 
Ww somesha tuu mwenzio wiki ya mwisho field anamalizia aliniacha solemba na machozi na jana yake ndo nlitoka kummalizia fees laki8 ila somesha and don't expect anything in return

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums
 

Jamaa zangu wengi walio wasomesha hao wachumba waliishia kupigwa vibuti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…