Unawakumbuka nguli hawa wa soka?

Kelvin yondani, Haruna Niyonzima, Emanuel Maltin, Deus Kaseke, Donald Ndombo Ngoma, Kamusoko, mbuyu Ntwite, Kakolanya, Didas, Amis Tambwe, Simon Msuva,Bousu na Shadrack NSajigwa hii list ilikuwa ni kiboko kwa simba enzi hizo.
 
Bora TFF irudishe michuano ya Kombe la Taifa. Halafu wahakikishe kila mchezaji akachezee timu ya mkoa wake, tunataka Mwanza heroes, Relu Eagles, Igembensabo, n.k
Duh ! umenikumbusha igembensabho kulikuwa na chuma kinaitwa silvester lugembe (msumbiji )jamaa alikuwa very slow ila mtaalamu wa kona alikuwa akipiga anafunga moja kwa moja .
 
Musimsahau Hussein Tindwa, aliekufa kiwanjani siku simba ilipocheza na Raccah Rovers ya Nigeria, hapo ilikuwa baada ya Simba kuipiga Mufulira Wandereres goli tano bila, kumbuka mechi ya mwanza iliochezwa uwanja wa taifa simba ilipigwa nne bila, huo ulikuwa ni mwaka 1978 sijui wangapi wanakumbuka hii

Ilikuwa 1979.
 
Hapana mkuu Simba walitoka sare ya bila kufungana na Raccah Rovers hapo Taifa siku ambayo Hussein Tindwa alifariki na mechi ya marudiano Naijeria mnyama akafa 2-0
 
Pamba FC (1980s)
Juma Mhina, Yusuf Bana, Abdallah Bori, Athuman Juma Chama, Ibrahim Magongo, John Mwakatika (Mzee Upara), Isaack Mwakatika, James Ng'ong'a (Mzee Mzima) Edward Hiza, Khalid Bitebo Zembwela, Abuu Juma,Beya Simba

Pamba FC (TP Lindanda Wana Kawekamo)
Madata Lubigisa, George Masatu, Husen Masha,Mao Mkami,Mkama Ntare,Kitwana Selemani,John Makelele,Msonga Rashid
Mzee wa upara aliitwa Joram Mwakatika na sio John
 
damian kimti, kasongo athumani, issa athumani, mwanamtwa kihwelo, eric sagala, often martin, madundo mtambo, lila shomari, kitwana manara (komputer) abuu jumaa, makumbi juma (homa ya jiji)
Kitwana Manara hakuitwa Computer bali Sunday Manara.
 
Hapo mbele alikuwapo Tuweni Ally na Saadi Ally
Saad Ally alicheza nyuma kabla ya Thuen Ally mainly 1974-1975 na nafikiri majeraha yalimharibia mpira wake ila alikuwa ni balaa, nakumbuka mechi yao na Mehalla El Kubra alipoamua mechi dakika za lala salama.

Thuen Ally alikuwa kwenye miaka ya 1979-1981. Wote hao waliichezea Simba.
 
CDA Watoto wa Nyumbani
Mkala Maulidi (golini), Yusuf Ambwene (alivunjwaga mguu na Ahmed Amasha), Jumanne Chale, Charles Sulemani, Selemani Abeid (Mkoba), Charles Mngodo, Eric Sagala, Denis Saigulan, Justine Simfukwe (Mawazo Nelson).
...Daniel Poka, Hamisi Kamungu, Eliakim Mbilike, Justine Simfukwe, Abbas ...........Huyo Dennis Seigulan hakuwa CDA nafikiri alikuwa Tumbaku au Reli za Morogoro.
 
@ Tongoni umenikumbusha Marehemu (R.I.P) Gibson Sembuli, maana kuna wimbo walimwimbia sina uhakika sn kama ni Marijani au Mbaraka mwinshehe
Uliimbwa na Mbaraka Mwishehe nafikiri ilikuwa ni wa 1978 akiwa Mombasa mauti yalikomkutia.
 
Msiwasahau akina Omar Zimbwe, Shaban Katwila, Uncle Shubert, Bernard Madale, Mohammed Kampira, Mohammed Salim, Mohammed Nyauba, Fikiri Magoso, Elisha John, Rashid Hanzuruni, Allan Shomari, Rajab Muhoza, Willy Kiango, Haidari Abeid, Omar Chogo, Omar Gumbo, etc
 
Jamani mbwana samatta m.bongo pekee aliewahi kukipiga club bingwa ulaya hapa atajwi kabisa yani dah! Au hao wachezaji mnavyowapamba hivyo kisa wengine hatukuwepo ndo Mana mbwembwe zimezidi
 
Musimsahau Hussein Tindwa, aliekufa kiwanjani siku simba ilipocheza na Raccah Rovers ya Nigeria, hapo ilikuwa baada ya Simba kuipiga Mufulira Wandereres goli tano bila, kumbuka mechi ya mwanza iliochezwa uwanja wa taifa simba ilipigwa nne bila, huo ulikuwa ni mwaka 1978 sijui wangapi wanakumbuka hii
Alipoibukia Tuweni Ali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom