Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 22,471
- 33,012
UNAWAFAMU VIPI WAIRANI?
Vita vya Iran na Israel vimevuruga ratiba yangu ya kazi kwani muda wangu mwingi unakuwa katika kufuatilia vita hivi katika vyombo vya habari mashuhuri ulimwenguni – Al Jazeera, CNN, BBC, Fox News halikadhalika nafuatilia katika media nyingine si maarufu kama hizo lakini zina mengi ya ‘’maana’’ mtu anaweza kujifunza hasa katika somo la ‘’propaganda.’’
Vyombo hivi vya habari visivyorusha mabomu ni mstari wa mbele katika mapambano haya ya silaha.
Hili ni jeshi bila silaha.
Vyombo hivi vinatumika kwa njia ya ujanja sana kupiga vita upande ule ambao wao wanauona ni wa adui yao na kwa kufanya hivyo kuutia nguvu upande ambao wao wanaupenda.
Iran na Sudan ni katika nchi ambazo mimi nimefika na ninaweza kusema kitu.
Yemen nimefika lakini sitaizungumza hapa.
Iran na Sudan ni katika nchi duniani ambazo ni ‘’pweke’’ zimetengwa na dunia.
Iran na Sudan zimetengwa kwa sababu ya Uislam wao.
Iran na Sudan nchi hizi mbili kwa hivi sasa zote zinakabiliwa na vita.
Iran inapigana na Israel na Marekani na Sudan wako katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Historia ya kale ya nchi hizi inasisimua.
Nini nimekiona Sudan ambacho kimebaki katika kumbukumbu yangu?
‘’Masjid Kabir,‘’msikiti mkubwa uko mjini Khartoum ambao msikiti mzima baada ya sala kuna darsa watu wameweka duara wanasoma.
Naogopa kukupa hesabu ya darsa hizo lakini ni watu wengi wa kukustaajabisha ikiwa wewe ni mgeni.
Lakini starehe utaipata Masjid Kabir, Sala ya Fajr usikilize, ‘’Kiraa.’’
Imam hana haraka.
Siwezi kueleza yote itahitaji kuandika kitabu.
Wasudani wana msemo wanasema, ‘’Sisi hatupendwi na dunia nzima sisi tunapendwa na Allah.’’
Hili linawatosha.
Nimeingia Tehran na Emirates, Al Fajr.
Kitu kilichonishtua ni kuwa uwanja wa ndege nimeukuta mtupu una watu wachache sijapata kuona kote duniani nilipopita.
Kawaida ni kuwa viwanja vya ndege muda wote vimejaa watu.
Uwanja wa Tehran nimeukuta umetulia, tuli.
Mtupu hakuna watu wengi.
Ninachokisikia ni Qur’an inasomwa katika vipaza sauti.
Barabarani nikaona picha nyingi za watu zimewekwa mfano wa matangazo ya biashara ambayo hapa kwetu yametundikwa katika ‘’billboards’’ yakitangaza kila aina ya bidha kuanzia pombe hadi vitu vingine, matangazo mengi yakiwa na picha za wanawake warembo.
Nilipowauliza wenyeji wangu hizo picha katika barabara za Tehran ni za nani wakaniambia hao ni mashahidi waliouliwa katika njia ya Allah.
Siwezi kuandika yote.
Natokea Berlin na Egypt Air narudi Dar es Salaam.
Mwezi wa Ramadhani niko Uwanja wa Ndege Cairo nasubiri ndege kurudi Dar es Salaam.
Niko transit na nimekuta watu wengi wake kwa waume wamevaa Ihram wanakwenda Umra katika Mwezi wa Ramadhani.
Abiria tuliofunga tunasubiri Adhana tufungue.
Vipaza sauti vilivyoko hapo uwanja wa ndege vinapiga miziki kwa fujo kama vile ni mwezi wa kula mchana.
Huu ni Mwezi Mtukufu wa Ramadhani, Cairo.
Nimetoa radio yangu na kuipitisha FM Station zote zilizoingia kutafuta Qur’an ili ikifika wakati wa kufungua nisikie Adhana.
Hakuna kitu.
Napokelewa na miziki ya kila aina.
Nikajisogeza kwenye mgahawa na kuuliza muda gani wa kufungua?
Wakanifahamisha na pia kunionyesha menu.
Naangalia menu.
Muda wa kufungua umefikia.
Hakuna Adhana.
FM Stations zinaendelea na muziki.