alikuwa amekaa, hakusimama this time. ila tusimpime kwa kuanguka kwani ni binadamu, anyone can fall. tuangalie uwezo wa kiutendaji zaidiPamoja na hayo lakini bado mimi nampa 20%...kwasababu hajaanguka kama kawaida yake
Anatuletea hadithi za mahawara zake aliokutana nao na mtoto zinahusu nini ktk taifa lililojaa uozo kama hili,hapa mi naona heading ingekuwa tunampa bakora ngapi instead of points!!
Niupe point nitazitoa wapi wakati JK mwenyewe hajajishugulisha kuzitafuta. Ni aibu, aibu, aibu... Mzee kigugumizi muda wote, kageuza mdahalo kijiwe cha stori na mwisho wa siku ametoka bila kuelezea hata sera moja. Alichokifanya ni kuwashawishi waliokuwa hawajaamua kumpa kura Dr Slaa wampe bila kinyongo. Hivi wanamwita Dr JK hawaoni aibu???
Binafsi siwezi kutoa alama maana hatukuweka vigezo vya alama hizo mapema.
Kwa kuzingatia kanuni za mawasiliano bora na pia malinganisho na wengine waliopata nafasi kama yake i.e CUF & CHADEMA na mazingira yetu ya TZ katika kufanya midaharo au mahojiano kama haya napenda kutamka wazi MAWAZO YANGU kutokana na nilichokishuhudia kama ifuatavyo:
1. Mshereheshaji pamoja na kuuliza maswali mazuri na kutoa maelekezo mazuri alionekana kupooza na hivyo kufanya mahojiano kutokuwa na hamasa itakiwayo. Aidha pia alishindwa kudhibiti vyema muda wa kujibu swali. Hakuonekana ku-'take charge' yaani kama mtu anauliza swali too general mf. "Tutegemee nini juu ya............. ya Serikali yako??" au penye jibu lisilo wazi basi angeweza kuingilia na kumuuliza muhusika afafanue zaidi.
2. Wazo la kuwashirikisha Vyombo vyote vikuu vya habari nimelifurahia. Kama mwakilishi angeuliza swali bovu basi ni aibu kwa chombo chake.
3. Pasipo mining'inio, kama majadaliano ya wengine, Maswali karibu yote yalikuwa mazuri tu na Waulizaji walikuwa straight pasi kuzunguka (pengine uzoefu katika media uliwasaidia hapo).
4. Bila upendeleo wa kutaka kusikia kile tunachotaka aseme, Mh. Kikwete hakika amejitahidi kujibu maswali mengi akionyesha na takwimu na pia mifano na kwa uwanja mpana. Aidha kujibu akiwa ametulia pasi kufoka ndani ya mic au kukurupuka au kuonyesha jaziba ni credit kubwa kwake.
5.Kwa mgombea wa urais, hitimisho lake lilibeba rai ya nguvu sana aliposisitiza Umoja wa Kitaifa usio na ubaguzi wa Kikabila, Dini, Maeneo n.k. na kutofumbia macho madhara yanayoweza kutupata endapo tutajiingiza huko.
6. Yapo mapungufu machache ambayo naweza kuyataja hususani katika weredi kwenye Public Speaking mfano:
i. Tatizo la kusita sita katika kile anachotaka kukisema kwa wakati fulani (sio wakati wote). Nadhani sasa naelewa kuwa hii ni hali ya kuzaliwa nayo ambayo watu wengi pia wanayo.
ii. Hali ya kufurahi au kucheka au kutabasamu kabla ya kujibu baadhi ya maswali ingawa ni rukrsa maana anaonyesha hisia zake, ingeweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa katika Session kama hii maana inaweza kutuma a wrong communication signal kwa hadhira.
iii. Majibu marefu sana yanaweza kukufanya kuondoka katika kiini cha swali na au kukanganya watu kwa kudandia sehemu ndogo tu ya mfano ambayo haikuwasilishwa vyema ndani ya maelezo marefu.
iv. Mabadiliko ya sauti (kupanda na kushuka) na mchanganyiko wa mwenendo maungo na ishara (Kinesics) zenye muonyesho wenye uvumilivu sifuri (Zero Tolerance) zingeweza kuboreshwa katika kuzungumzia mambo fulani mfano. Rushwa na Kutokuwajibika kwa baadhi ya Watumishi Serikalini.
v. Kuomba watu wajitokeze kwa wingi na kutumia haki yao kuchagua wanayempenda tahehe 31/10 ni sawa lakini asingeishia hapo tu. Akiwa kama Mgombea aliyekuwa anawasilisha CCM alistahili kumalizia kwa kuomba kura Wananchi, haijarishi kuwa hilo amesha litamka kote alipo kampeni.
Wakuuu
Wakati mdahalo unaendelea mimi niliingi kwenye gari kufanya kautafit kidogo
nilianzia magomeni kwa shekh yahaya, all the way to shekhlango, sinza yote
sikuona ushabiki wowote wa mdahalo.
Niliona sehemu tatu tu wanaangalia huo mdahalo Kuna salon ya kiume Kamanyola
kuna baa moja sinza madukani na T garden karibu na Lion Hotel ndio walikua wanaangalia
sehemu zingine walikua wanaangalia either mpira au music.
Maana yake ni Nini watu hawamtaki JK hata kusikia sauti yake hawataki.
Pili hakuna effect yeyote kwa compaign aliyofanya Dr. Slaa
sana sana watu wamesikitishwa na jinsi media zimefamya ugaidi kufanya coverage ya
JK bila kutoa fursa sawa kwa vyama vingine vya siasa. Hivyo wapiga kura wengine
ambao walikua hawajamua watapiga kura za sympathi which is credit to Dr. Slaa
God bless Tanzania, God bless our New President
Wakuuu
Wakati mdahalo unaendelea mimi niliingi kwenye gari kufanya kautafit kidogo
nilianzia magomeni kwa shekh yahaya, all the way to shekhlango, sinza yote
sikuona ushabiki wowote wa mdahalo.
Niliona sehemu tatu tu wanaangalia huo mdahalo Kuna salon ya kiume Kamanyola
kuna baa moja sinza madukani na T garden karibu na Lion Hotel ndio walikua wanaangalia
sehemu zingine walikua wanaangalia either mpira au music.
Maana yake ni Nini watu hawamtaki JK hata kusikia sauti yake hawataki.
Pili hakuna effect yeyote kwa compaign aliyofanya Dr. Slaa
sana sana watu wamesikitishwa na jinsi media zimefamya ugaidi kufanya coverage ya
JK bila kutoa fursa sawa kwa vyama vingine vya siasa. Hivyo wapiga kura wengine
ambao walikua hawajamua watapiga kura za sympathi which is credit to Dr. Slaa
God bless Tanzania, God bless our New President