Elections 2010 Unaupa point ngapi mdahalo (hotuba) ya JK? - Toa sababu...

kama mimi ni mwalimu wake, namtuma yeye mwenyewe akatafute bakora nimchape, au namfukuza shule kabisa, au namrudisha madarasa mawili nyuma.
 
Pamoja na hayo lakini bado mimi nampa 20%...kwasababu hajaanguka kama kawaida yake
alikuwa amekaa, hakusimama this time. ila tusimpime kwa kuanguka kwani ni binadamu, anyone can fall. tuangalie uwezo wa kiutendaji zaidi
 
Binafsi siwezi kutoa alama maana hatukuweka vigezo vya alama hizo mapema.
Kwa kuzingatia kanuni za mawasiliano bora na pia malinganisho na wengine waliopata nafasi kama yake i.e CUF & CHADEMA na mazingira yetu ya TZ katika kufanya midaharo au mahojiano kama haya napenda kutamka wazi
MAWAZO YANGU kutokana na nilichokishuhudia kama ifuatavyo:

1. Mshereheshaji pamoja na kuuliza maswali mazuri na kutoa maelekezo mazuri alionekana kupooza na hivyo kufanya mahojiano kutokuwa na hamasa itakiwayo. Aidha pia alishindwa kudhibiti vyema muda wa kujibu swali. Hakuonekana ku-'take charge' yaani kama mtu anauliza swali too general mf. "Tutegemee nini juu ya............. ya Serikali yako??" au penye jibu lisilo wazi basi angeweza kuingilia na kumuuliza muhusika afafanue zaidi.

2. Wazo la kuwashirikisha Vyombo vyote vikuu vya habari nimelifurahia. Kama mwakilishi angeuliza swali bovu basi ni aibu kwa chombo chake.

3. Pasipo mining'inio, kama majadaliano ya wengine, Maswali karibu yote yalikuwa mazuri tu na Waulizaji walikuwa straight pasi kuzunguka (pengine uzoefu katika media uliwasaidia hapo).

4. Bila upendeleo wa kutaka kusikia kile tunachotaka aseme, Mh. Kikwete hakika amejitahidi kujibu maswali mengi akionyesha na takwimu na pia mifano na kwa uwanja mpana. Aidha kujibu akiwa ametulia pasi kufoka ndani ya mic au kukurupuka au kuonyesha jaziba ni credit kubwa kwake.

5.Kwa mgombea wa urais, hitimisho lake lilibeba rai ya nguvu sana aliposisitiza Umoja wa Kitaifa usio na ubaguzi wa Kikabila, Dini, Maeneo n.k. na kutofumbia macho madhara yanayoweza kutupata endapo tutajiingiza huko.

6. Yapo mapungufu machache ambayo naweza kuyataja hususani katika weredi kwenye Public Speaking mfano:

i. Tatizo la kusita sita katika kile anachotaka kukisema kwa wakati fulani (sio wakati wote). Nadhani sasa naelewa kuwa hii ni hali ya kuzaliwa nayo ambayo watu wengi pia wanayo.

ii. Hali ya kufurahi au kucheka au kutabasamu kabla ya kujibu baadhi ya maswali ingawa ni rukrsa maana anaonyesha hisia zake, ingeweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa katika Session kama hii maana inaweza kutuma a wrong communication signal kwa hadhira.

iii. Majibu marefu sana yanaweza kukufanya kuondoka katika kiini cha swali na au kukanganya watu kwa kudandia sehemu ndogo tu ya mfano ambayo haikuwasilishwa vyema ndani ya maelezo marefu.

iv. Mabadiliko ya sauti (kupanda na kushuka) na mchanganyiko wa mwenendo maungo na ishara (Kinesics) zenye muonyesho wenye uvumilivu sifuri (Zero Tolerance) zingeweza kuboreshwa katika kuzungumzia mambo fulani mfano. Rushwa na Kutokuwajibika kwa baadhi ya Watumishi Serikalini.

v. Kuomba watu wajitokeze kwa wingi na kutumia haki yao kuchagua wanayempenda tahehe 31/10 ni sawa lakini asingeishia hapo tu. Akiwa kama Mgombea aliyekuwa anawasilisha CCM alistahili kumalizia kwa kuomba kura Wananchi, haijarishi kuwa hilo amesha litamka kote alipo kampeni.
 
Anatuletea hadithi za mahawara zake aliokutana nao na mtoto zinahusu nini ktk taifa lililojaa uozo kama hili,hapa mi naona heading ingekuwa tunampa bakora ngapi instead of points!!

Sasa huu upuuzi hautaitwa "insulting" kwa mujibu wa Moderators wa ukumbi huu. Lakini ukiandika S L A A mean Sex & Love Addicts Anonymous na kuweka website ya #SLAA Online Group of Sex and Love Addicts Anonymous - Home unaanza kupewa mikwara. Hapo bado mtu anakataa kuwa ukumbi huu si mali ya Chadema! :nono:
 
Niupe point nitazitoa wapi wakati JK mwenyewe hajajishugulisha kuzitafuta. Ni aibu, aibu, aibu... Mzee kigugumizi muda wote, kageuza mdahalo kijiwe cha stori na mwisho wa siku ametoka bila kuelezea hata sera moja. Alichokifanya ni kuwashawishi waliokuwa hawajaamua kumpa kura Dr Slaa wampe bila kinyongo. Hivi wanamwita Dr JK hawaoni aibu???

Kama UONGO utakuwa unapiga kura kesho, basi watu wa kijiwe hiki na chama chao washashinda uchaguzi. Kwa bahati mbaya hivyo sivyo! Teh teh teh!!!!!!!
 
Wakuuu

Wakati mdahalo unaendelea mimi niliingi kwenye gari kufanya kautafit kidogo
nilianzia magomeni kwa shekh yahaya, all the way to shekhlango, sinza yote
sikuona ushabiki wowote wa mdahalo.

Niliona sehemu tatu tu wanaangalia huo mdahalo Kuna salon ya kiume Kamanyola
kuna baa moja sinza madukani na T garden karibu na Lion Hotel ndio walikua wanaangalia
sehemu zingine walikua wanaangalia either mpira au music.

Maana yake ni Nini watu hawamtaki JK hata kusikia sauti yake hawataki.
Pili hakuna effect yeyote kwa compaign aliyofanya Dr. Slaa
sana sana watu wamesikitishwa na jinsi media zimefamya ugaidi kufanya coverage ya
JK bila kutoa fursa sawa kwa vyama vingine vya siasa. Hivyo wapiga kura wengine
ambao walikua hawajamua watapiga kura za sympathi which is credit to Dr. Slaa

God bless Tanzania, God bless our New President
 
Binafsi siwezi kutoa alama maana hatukuweka vigezo vya alama hizo mapema.
Kwa kuzingatia kanuni za mawasiliano bora na pia malinganisho na wengine waliopata nafasi kama yake i.e CUF & CHADEMA na mazingira yetu ya TZ katika kufanya midaharo au mahojiano kama haya napenda kutamka wazi MAWAZO YANGU kutokana na nilichokishuhudia kama ifuatavyo:

1. Mshereheshaji pamoja na kuuliza maswali mazuri na kutoa maelekezo mazuri alionekana kupooza na hivyo kufanya mahojiano kutokuwa na hamasa itakiwayo. Aidha pia alishindwa kudhibiti vyema muda wa kujibu swali. Hakuonekana ku-'take charge' yaani kama mtu anauliza swali too general mf. "Tutegemee nini juu ya............. ya Serikali yako??" au penye jibu lisilo wazi basi angeweza kuingilia na kumuuliza muhusika afafanue zaidi.

2. Wazo la kuwashirikisha Vyombo vyote vikuu vya habari nimelifurahia. Kama mwakilishi angeuliza swali bovu basi ni aibu kwa chombo chake.

3. Pasipo mining'inio, kama majadaliano ya wengine, Maswali karibu yote yalikuwa mazuri tu na Waulizaji walikuwa straight pasi kuzunguka (pengine uzoefu katika media uliwasaidia hapo).

4. Bila upendeleo wa kutaka kusikia kile tunachotaka aseme, Mh. Kikwete hakika amejitahidi kujibu maswali mengi akionyesha na takwimu na pia mifano na kwa uwanja mpana. Aidha kujibu akiwa ametulia pasi kufoka ndani ya mic au kukurupuka au kuonyesha jaziba ni credit kubwa kwake.

5.Kwa mgombea wa urais, hitimisho lake lilibeba rai ya nguvu sana aliposisitiza Umoja wa Kitaifa usio na ubaguzi wa Kikabila, Dini, Maeneo n.k. na kutofumbia macho madhara yanayoweza kutupata endapo tutajiingiza huko.

6. Yapo mapungufu machache ambayo naweza kuyataja hususani katika weredi kwenye Public Speaking mfano:

i. Tatizo la kusita sita katika kile anachotaka kukisema kwa wakati fulani (sio wakati wote). Nadhani sasa naelewa kuwa hii ni hali ya kuzaliwa nayo ambayo watu wengi pia wanayo.

ii. Hali ya kufurahi au kucheka au kutabasamu kabla ya kujibu baadhi ya maswali ingawa ni rukrsa maana anaonyesha hisia zake, ingeweza kudhibitiwa kwa kiwango kikubwa katika Session kama hii maana inaweza kutuma a wrong communication signal kwa hadhira.

iii. Majibu marefu sana yanaweza kukufanya kuondoka katika kiini cha swali na au kukanganya watu kwa kudandia sehemu ndogo tu ya mfano ambayo haikuwasilishwa vyema ndani ya maelezo marefu.

iv. Mabadiliko ya sauti (kupanda na kushuka) na mchanganyiko wa mwenendo maungo na ishara (Kinesics) zenye muonyesho wenye uvumilivu sifuri (Zero Tolerance) zingeweza kuboreshwa katika kuzungumzia mambo fulani mfano. Rushwa na Kutokuwajibika kwa baadhi ya Watumishi Serikalini.

v. Kuomba watu wajitokeze kwa wingi na kutumia haki yao kuchagua wanayempenda tahehe 31/10 ni sawa lakini asingeishia hapo tu. Akiwa kama Mgombea aliyekuwa anawasilisha CCM alistahili kumalizia kwa kuomba kura Wananchi, haijarishi kuwa hilo amesha litamka kote alipo kampeni.

Very good and unbiased analysis. Well done!:smile-big:
 
Wakuuu

Wakati mdahalo unaendelea mimi niliingi kwenye gari kufanya kautafit kidogo
nilianzia magomeni kwa shekh yahaya, all the way to shekhlango, sinza yote
sikuona ushabiki wowote wa mdahalo.

Niliona sehemu tatu tu wanaangalia huo mdahalo Kuna salon ya kiume Kamanyola
kuna baa moja sinza madukani na T garden karibu na Lion Hotel ndio walikua wanaangalia
sehemu zingine walikua wanaangalia either mpira au music.

Maana yake ni Nini watu hawamtaki JK hata kusikia sauti yake hawataki.
Pili hakuna effect yeyote kwa compaign aliyofanya Dr. Slaa
sana sana watu wamesikitishwa na jinsi media zimefamya ugaidi kufanya coverage ya
JK bila kutoa fursa sawa kwa vyama vingine vya siasa. Hivyo wapiga kura wengine
ambao walikua hawajamua watapiga kura za sympathi which is credit to Dr. Slaa

God bless Tanzania, God bless our New President

kuna watu niliwaambia huu mdahalo unamuongezea dr.slaa kura wakabisha, ulivyoisha wakasema ni kweli umemuongezea credit.
 
Wakuuu

Wakati mdahalo unaendelea mimi niliingi kwenye gari kufanya kautafit kidogo
nilianzia magomeni kwa shekh yahaya, all the way to shekhlango, sinza yote
sikuona ushabiki wowote wa mdahalo.

Niliona sehemu tatu tu wanaangalia huo mdahalo Kuna salon ya kiume Kamanyola
kuna baa moja sinza madukani na T garden karibu na Lion Hotel ndio walikua wanaangalia
sehemu zingine walikua wanaangalia either mpira au music.

Maana yake ni Nini watu hawamtaki JK hata kusikia sauti yake hawataki.
Pili hakuna effect yeyote kwa compaign aliyofanya Dr. Slaa
sana sana watu wamesikitishwa na jinsi media zimefamya ugaidi kufanya coverage ya
JK bila kutoa fursa sawa kwa vyama vingine vya siasa. Hivyo wapiga kura wengine
ambao walikua hawajamua watapiga kura za sympathi which is credit to Dr. Slaa

God bless Tanzania, God bless our New President

Duh! Kama kuna kura za "sympathy" kwa wagombea ambao hawakupata coverage kweli zipo, basi hizo zitaenda kwa Bw. Dovutwa na Hashim Rungwe.

Na hicho "kautafiti kidogo" nacho, kimekaa kibangi bangi vile!
 
Wandugu,

naomba link ya youtube kwa alieweza kurekodi hicho kikao cha halmashauri ya CCM, sorry i mean mdahalo wa JK
 
Ulikuwa mdahalo wa kisanii uliomkutanisha na vibaraka walioandaliwa maswali ya kijinga ili aonekane mahiri ambapo hata hivyo
aliishia kupiga porojo na wapambe wake kupiga makofi hata alipokuwa anacheka! Kama ni kweli anaamini kushinda kwa kishindo mbona alionekana kutotulia?
Bado sijaelewa kwa vipi hata waandishi niliowadhani makini waliuliza maswali fyongo na yenye kutia kichefuchefukiasi cha mtu kushawishika kuzima au kuhama stesheni.
Wanaojiita wahariri au waandishi wameiangusha fani na hapa ndipo namkumbuka Mkapa (mwenyewe mwandishi ) aliyewahi kuwaponda na kusema ni vigumu kuwapata nchini waandishi wa kiwangoche Rhiz Khan. Mimi nampa 20% yeye, na waliomwuliza 0.20%.
 
"Ngumu sana kwa kiungo mkabaji kuwa mchezaji bora"
with that qoute naomba niseme X-prezdaaa a.k.a Mkwere leo alikua in som kend of tension' he knew he had a lot to defend kuliko to add' he was trying hard to show what he has done.. but am not sure that should have been the purpose of the mdahalo.. lakin aliongea mambo machache ya ku-add kama matumizi ya teknohama na mkonga wa mawasiliano' which in the current world it is inevitable.. Nadhani prezidaa alichagua watu wa kumuuliza maswali coz sijaona watu critical ambao hawamwofii kumuuliza maswali challenging nadhani hilo limepunguza changamoto za mdahalo.

Lakini pia he was not focused wakat wa kujibu maswali, ni kama alikua anapga story hivi' amehadithia story nyingi kuliko kuelezea mambo ya msingi'

Nadhani amejitahidi, ila ukilinganisha na Dr Slaa (PhD) na Prof Lipumba (PhD).. Dr Kikwete ameonyesha dhahiri tofauti ya udaktari wa kupewa na udaktari wa kusomea'

Kwa sababu na mi ni mwalimu makini na si wa kubabaisha nampa B (plain) ukilinganisha na wenzake wenye A
 
Mi sijaona sababu ya kumpa marks coz jamaa amedisco yaani ni aibu 2pu kuangalia ukweli MKWERE yeye ngoma 2,me nahisi jamaa ni sharobaro mzee ameenda kuuza sura 2!me simlaumu ntakulaumu wewe ambaye trh 31 utapoteza kura yako kwa kumchagua kiongozi mbabaishaji!
 
Sipendi kuamini sana kuwa maswali yalipangwa ila nina uhakika kwa aslimia mia moja kuwa wauliza maswali wote walimuona kama Rais na si mgombea,walionekana wote kukwepa kumkera mkubwa.
binafsi naona alijitahidi kueleza kwa uelewa wake ila HATARI kubwa ni kuwa inaelekea mambo mengi hayaendi kwa mfumo unaotakiwa ila urafiki.
Nilisikitishwa na kusifia Muhimbili kitengo cha meno kuwa kime improve lakini ni kutokana na mambo ya urafiki,je sustainability itakuwepo urafiki ukivunjika?
Alieleza ya kuwa anajenga mfumo wa utawala bora (in respect to Takukuru) lakini amesahau ya kuwa mambo haya yote na taasisi za utawala bora zilikuwepo na CCM ikazivunja -kamati ya maadili ya viongozi,usalama wa taifa n.k.
Nihitimishe kwa kusema ameshindwa kutuonyesha njia.\Akijaaliwa kuingia IKULU ni lazima aingize watu waliokuwa na uchungu na nchi hata kama wapo opposition pia ni lazima achukue maamuzi magumu
 
Mdahalo haukuwa huru, maswali na majibu na waulizaj, muulizaji aulize nini na mjibuji ajibu nini vilikuwa vimepangwa nampa 25%
 
binafsi sikuona logic ya wauliza maswali kujirudia wakati kulikuwa na watu wengi tu pale ukumbini.... Kwa nini hawakuruhusu maswali toka kwa waulizaji huru???
 
Back
Top Bottom