Freelancer Wakala
JF-Expert Member
- Feb 6, 2016
- 1,193
- 828
Je unaunga mkono nguo za mitumba kupigwa maarufuku nchini Tanzania?
Hakuna sababu ya kujenga chuki kwa wadau wa mitumba na serikali kwa kuzuia mitumba bila kuwa na mbadala.
Angalia sababu za watu kupenda mitumba ni nini kuliko mali mpya imported ama za ndani kama zipo. Changanua tatizo llinaloletwa na mitumba kwanza na ndipo uone namna ya kulitatua. Unaweza kuona tatizo siyo uwepo wa mitumba.
Kama unataka kuimarisha soko la bidhaa za ndani, imarisha uzalishaji wa ndani kwa maana ya ubora na wingi ili kukidhi mahitaji.
Hakuna mtu atanunua mtumba wakati kuna kitu bora kuliko mtumba na kinapatikana kwa wingi nyumbani hapa.
Kama ni bei kwamba mitumba in bei ndogo, wekeni mazingira mazuri ya uzalishaji ikiwemo upatikanaji wa nishati na bei zake ziwe chini, uzalishaji na upatikanaji nafuu wa malighafi za ndani, na kupunguza mfumuko wa bei huku mkiimarisha uchumi wa familia badala ya kuishia kwenye GDP tu na kuanza kuchelea.
Automatically soko la vitu mitumba litapungua sana. Na itafika wakati kama ni lazima, kuwe na mitumba ya ndani siyo yakutoka nje kwa kuwa hii iko duniani kote.
Hii mabavu hii mtaishia kuwafanya watu waanze kuvaa ngozi na magome ya miti, wapandishiwe nauli za magari waanze kutembea kwa miguu ya masurufu ya njiani. I dont think this is what we want.