Bushmamy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2019
- 8,990
- 15,600
Wanawake hao wamekuwa wakienda Dampo/jalalani kutafuta nguo zilizotupwa na zilizoletwa na magari ya taka na hivyo kuchukua nguo hizo kwa kununua kutoka Kwa vijana wanafaonya kazi Dampo na kwenye magari ya taka kwa bei ya shilingi elf kumi hadi kumi na tano kwa kiroba kimoja cha nguo.
Wafanyabiashara hao kuzifua na kwenda kuziuza tena minadani/sokoni kwa bei ya shilingi mia tano (500), elfu moja moja (1000) na shillingi elfu mbili (2000) kwa nguo moja.
Wafanyabiashara hao wamedai sababu ya Kufanya biashara hiyo ni kutokana na utofauti mkubwa wa bei uliopo kwenye kununua belo jipya za kutoka ulaya na na kununua jalalani kutoka na kukosa mitaji.
Bei ya kununua jalalani ni rahisi sana na yenye faida ya haraka tofauti na kununua mabelo ya mitumba kutoka ulaya ambapo ni kati ya shilingi laki mbili Hadi lakini tano kwa belo moja.
Wanawake hao wamedai Kuwa kwa soko moja hupata kiasi cha shilingi elfu 70, hadi elfu 80 kama faida.
Wafanyabiashara hao wanadai biashara hiyo inawasaidia kuendesha maisha ya Kila siku kama vile gharama za watoto wa shule ,kodi na mahitaji muhimu ya Kila siku.