Unatimiza Ndoto Zako?

sensa

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
397
22
Wengi tumekuwa tumeweka mawazo yetu sana kwenye ajira,nakumbuka mara nyingi ukimwambia mtu ajiajiri anasema hawezi biashara lakini wakati huo huo kaajiriwa kuendesha na kusimamia biashara ya mtu mwingine.Halafu analalamika ana shida kipato hakimtoshi,ukweli ni kwamba aliyekuajiri ni kama wewe tu alichokuzidi ni maamuzi ya yeye kuwa na biashara yake.Pamoja na kutoridhika na hayo bado utamkuta mtu anang'ang'ania kazi hiyo hiyo bila kujua atabaki na shida hizo hizo mpaka atakapostaafu huku kikubwa atakachokuwa amefanya ni kutimiza ndoto za mwajiri wake akibaki na umaskini wa kutupa,stress zinaanza anajifia zake mapema.Badilika leo unaweza kufanya bishara yako,mtazamo wako ndio silaha yako,ndio furaha yako na nia kuu ya kukufanya uyapate yale unayoyataka na siyo anayotaka boss wako uyapate.Aliyenielewa na angependa tuzungumze zaidi ili tuweze kusaidiana na kukwamuana katika hii poverty cirlce anitumie email sensa28@gmail.com
 
Back
Top Bottom