unatakiwa kuomba ruhusa au kuaga | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

unatakiwa kuomba ruhusa au kuaga

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Joyceline, Jul 21, 2009.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nimeikuta www.harusiyangu.com

  wanandoa wakati unatoka unatakiwa umuage mwenzako au uombe ruhusa?
   
 2. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Inategemea na aina ya safari. Kwa mfano unaenda sokoni sidhani kama unatakiwa kuomba ruhusa. Yafaa kuaga. Lakini kama ni kasafari ambako una wasiwasi kuaga tu hakutoshi basi waweza ku-propose kwa mwenzako ukionesha lakini nia ya kile unachodhamiria kufanya.
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  taarifa ni muhimu kutoa kwa mwenzako, sio unakurupuka tu, unauhakika gani ukienda sokoni utarudi salama?, kuna mambo mengi siku hizi umegongwa na gari au pikipiki, umekamatwa huko sokoni kwenye purukushani zozote, na sio kwa mke hata mume umekwenda bar bila kuaga kwa my wife wako huko umesombwa na polisi si unajua polisi now wanapiga risasi ovyo ovyo, umelewa umefanya fujo ukarundikwa rumande mkeo huoni utakua unampa tabu kujua uko wapi?.
  pia kuaga kunaonyesha respect kwa mwenzako, sio kujifanya kichwa cha familia halafu huagi, inamaana hata watoto wako wakiwa hawaagi utamlaumu nani?

  kuhusu kuomba ruhusa hapa ni pale unapotaka kutoka lakini sio lazima ukubaliwe hiyo ruhusa, inategemea na umuhimu. mfano unasafiri inatakiwa uombe ruhusa na kutokana na uzito wa safari ruhusa itatolewa. ingawa kwenye hili suala la ruhusa mara nyingi inaonekana kuwabana sana wanawake, coz wanaume si unajua tena ndio vichwa vya familia, so sie huwa tunatoa tu taarifa kimtindo!!!
   
 4. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  nyie mnatoa taarifa kimtindo, kwa hiyo na mimi naweza nikaamka asubuhi nikasema leo naenda singida kikazi,itakuwaje?
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Kuaga/kuombe ruhusu ni kitu cha kawaida,, popote uendapo, na ikiwezekana ni bora mkawa pamoja

  Mi my wife wangu hata akienda sokoni/gengeni ananiambia, hiyo ni katika kuboresha mawasiliano ndani ya ndoa kitu ambacho mara nyingi ni chanzo cha migogoro mingi kwenye ndoa.

  Kuomba ruhusa pia ni kuonyesha heshima kama alivosema mchangiaji mmoja hapo juu,na maana yake ni kuwa tayari kukubali matokeo kwa umekubaliwa/kataliwa kulingana na umuhimu wa safari yenyewe.
   
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Jamani kuaga muhimu hata kama unaenda kuoga,msalani,kokote pale lazima uage bana sasa unajiondokea kama kuku alafu nakukuta mazingira tata lakini ndo kwenye njia hiyo hiyo uliko kuwa unakwenda nitakwelewa sikuelewi hapo hapo talaka 3.
   
 7. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #7
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Kutoa taarifa kimtindo ndo inakuwaje Joyceline, hebu tufafanulie zaidi?
   
 8. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #8
  Jul 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Iwe pamde zote .......... siyo mke tu ndo anayeomba/toa taarifa ya kwenda sehemu hata mume ni kuonyesha kuwa unamthamini mwenzi wako.
   
 9. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Dogo apo tupo pamoja, ila sasa umekuwa na siasa kali sana apo,, angalia utaharibu kule kwingine si unajua anapitia pitia hapa anaweza kuogopa,,hehehehehehe
   
 10. GP

  GP JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  patakua hapatoshi hapo chumbani.
   
 11. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hehehe kweli bro. Lakini ni vyema ajue kuwa mm sina mzaha lazima anapo toka aage anakwenda wapi saloon au bar lazima atoe maelezo sio anajiondokea tu kama kuku asubuhi.
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280

  hehehehe mkuu utamruhusu aende bar mwenyewe?
   
 13. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #13
  Jul 21, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  .......... Ila Fidel una vijineno.... utafikiri mkoma ngoma wa Msata lol
   
 14. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  hahaha ndo hivyo luv tukiwa pamoja lazima uwe unaaga sio kukurupuka tu kama jamaa aliyefumaniwa ugoni.
   
 15. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Ebwanee kama anaenda na mashosti wake namruhusu lakini sio akae peke yake ingawa wanasema wanao enda bar ni malaya wengine wanaenda kuwaona akina Fidel teh teh teh
   
 16. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #16
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nafikiri hata mwanaume anatakiwa kuomba ruhusa kwa mkewe. Kuna namna nyingi za kuomba. Si lazima aseme "Naomba ruhusa" kama wafanyavyo wanetu. Anaweza kutumia maneno tofauti. Kwa mf. "Mama fulani, nafikiria kwenda kuwaona wazee wiki ijayo na kurudi baada ya siku 2". Hapo jamaa anakuwa ameonesha nia yake ya kusafiri ambayo inasubiri kuungwa mkono na mkewe au kutoungwa mkono kama kuna sababu nzito. Kumbe kuomba ruhusa kunawafunga wote wawili.
   
 17. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280

  sawa Babu, hekima kubwa sana hii!
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,658
  Likes Received: 1,490
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwangu hiyo naiona hatari sana,, kama kwenda kawaida muende wote
   
 19. a

  agika JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2009
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 381
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nijuavyo mie mahusiano yenye mapenzi kati ya wawili hao wala si jambo la kujiuliza kumuaga mwenzio au kumjuza mwenzio uendako mie najua hiyo inakuja naturally yaani utahisi tu umesahau kitu kumwaambia mwenzio , "asali wangu wa moyo naenda sokoni kununua mahitaji' nae atajibu "sawa nyongo mkalia ini nenda salama au wataka nikusindikize darling?" ,........... so all am saying depends na upendo kati yenu kama mapenzi hafifu unaona poa tu hata usipoliaga hilo limwenza wako haijalishi. which is not the way.
   
 20. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #20
  Jul 22, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Unajua kwa sisi wanawake , mwanaume anataka aombwe ruhusa, fulani naomba ruhusa nataka kesho niende kwenye sherehe, anaweza akubali au akatae, mimi nakataa inatakiwa uage tu naenda sehemu fulani kutoa taaarifa siyo lazima uombe ruhusa huo ni ukoloni mamboleo,
   
Loading...