Unataka Skolashipu?

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Habari.

1. Kwa nini unataka skolashipu -- hasa zile za kwenda nchi za nje?

NB: Bongo-michosho, natamani tu na mimi nikasome nje, eksipozjha, duh!, ni majibu ya waombaji kama wewe 28,715.

2. Kwa nini mwenye kugawa skolashipu akuchague wewe, na siyo wenzio 28,714.

NB: Sijui, mimi kipanga, nina hamu sana kusoma nje, ndio ndoto zangu toka mtoto, nk., ni jibu la waombaji 28,711

3. Wafahamu taasisi/mfadhili/programu inayotoa skolashipu?
Mi sijui, lakini nataka skolashipu! Nasikia scholarship yao ni fully-funded, Yaani nikiipata hiyo skolashipu bongo watanisikia tu, n.k, si majibu ya tija.


HITIMISHO: Bila maelezo ya hakika kwa maswali hayo hapo juu, na jitihada za kukusudia kupata, zikiwemo kumuomba Mungu, ni vigumu kupata.
 
Back
Top Bottom