Unatafuta nafasi ya masomo Australia?

Unatafuta nafasi ya masomo Australia?

IBSCS

Member
Joined
Aug 20, 2015
Posts
31
Reaction score
4
Habari?

Kama wewe ni mmoja wa wale wanaotafuta nafasi ya kusoma nchini Australia katika ngazi ya cheti, diploma, shahada, Uzamili na uzamivu tafadhali huu uzi ni wako.

Ni hivi, kuna baadhi ya Watanzania wamekuwa wakihangaika kutafuta nafasi za masomo nje ya nchi na kuishia kukosa kwa sababu kadha kwa kadha lakini kubwa ikiwa ni kukosa TAARIFA sahihi.

Kinachosikitisha zaidi ni pale hata wale ambao wanauwezo wa kujilipia karo (tuition fee) kushindwa kupata udahili (admission) sababu ya ama kutokujua vizuri namna ya kufanya maombi ya udahili ama kutokujua ni wapi aanzie kufanya maombi na kwanini.

Katika kusaidia Watanzania (na wa mataifa mengine) wanaotafuta nafasi za masomo Australia kampuni ya INTERNATIONAL BUSINESS AND STUDENTS CONSULTING SERVICES ipo kwa ajili yao.

Kampuni yetu inashughulikia kuwaombea udahili (admission) wanafunzi wanaohitaji kusoma (diploma, bachelor, masters, PhD) na wengi wa wateja wetu ni wale wenye mpango wa kujilipia karo. Kampuni yetu haishughuliki na kuombea ufadhili wanafunzi lakini inatoa ushauri bure kwa wanafunzi wanaohitaji taarifa (information) kuhusu ufadhili. Kama ikitokea mwanafunzi anayetaka kuomba udahili kupitia kwetu na kisha aombe ufadhili mwenyewe anakaribishwa kuwasiliana nasi.

Kama kuna mwanafunzi anayetaka kuomba ufadhili wa kusomea masters ama PhD tafadhali apitie hizi links zifuatazo:

1. Australian Postgraduate scholarships Search Engine
2. International Postgraduate Research Scholarships (IPRS)
3. Australia Awards for Tanzanian Students

Itembelee kampuni ya IBSCS hapa http://www.ibscservices.com/

Tuandikie kupitia barua pepe hii: admin@ibscservices.com

Kila la heri

IBSCS
 
Sasa nikitaka kuitafuta website yenu kwa google nafanyaje?
 
Sasa nikitaka kuitafuta website yenu kwa google nafanyaje?

Hamna haja ya kutafuta kwa Google. Ni swala la ku-click hiyo link, Mimi kwangu link ipo active na nikiclick inanipeleka moja kwa moja kwenye website.
 
Ni fursa kwani baadhi ya huduma zinatolewa bure kabisa!

So nyie ni madalali si ndio? Mnachaji ile inaitwa processing fees au ni free service?

Na je ni Australia pekee ama na kwingine?

Kupata visa ya 458 (working visa) pia mnaweza kuprocess?

I'm very interested, wakenya wamekua wanakula sana pesa zetu, naomba ujibu hayo maswali
 
Hello Jerrymsigwa, kampuni yetu inamembers kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, DRC na Thailand kwa sasa. Pole kama uliibiwa na kampuni nyingine, rest assured kuwa sisi hatutakuibia na hatunampango huo na ndo maana members wote tupo kwenye website na contact zetu.

Sisi tunafanya kazi kwa Australia pekee kwa sasa na tuna mikataba na baadhi ya institutions hapa Australia kama TAFE (TAFE ni kama VETA kwa Tanzania) na universities kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye sifa lakini wanashindwa kutokana na sababu mbalimbali.

Yes, tunacharge processing fee lakini ni ile ambayo mwananchi wa kawaida anamudu kulipa. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kiasi tunachocharge (ambacho kinategemeana na servive itakayotolewa) tafadhali click sehemu imeandikwa contact us kwenye website yetu na afisa mmoja atakujibu mwanzo mwisho!

Kuhusu working VISA, kampuni yetu haishughulikii lakini ushauri wa bure unatolewa pale mteja atakapoeleza shida yake.

Ushauri wa bure pia unatolewa kwa wale wanafunzi wanaotaka kuapply wenyewe scholarships mbalimbali.

Hope nimeeleweka lakini ukiwa na swali ama dukuduku andika tena tulonge.

Salaam

IBSCS
 
Ongeza maelezo kidogo mkuu! Scholarships katika ngazi ipi? Na katika field ipi?

Kama vipi ngoja nikuachie scholarship search engine ya Australia uicheki mwenyewe. Tembelea JASON is no longer available

Asante ngoja niipitie..

Ila scholarship in LLM in Corporate law kama IPO. Ila ngoja nipitie hio link kwanza
 
Asante ngoja niipitie..

Ila scholarship in LLM in Corporate law kama IPO. Ila ngoja nipitie hio link kwanza

Okay, hizo link mbili zitakupa mwanga wa scholarship ipi unaweza kuapply. Tip: scholarships nyingi zinatolewa kwenye research degrees na siyo taught.
 
Hello Jerrymsigwa, kampuni yetu inamembers kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, DRC na Thailand kwa sasa. Pole kama uliibiwa na kampuni nyingine, rest assured kuwa sisi hatutakuibia na hatunampango huo na ndo maana members wote tupo kwenye website na contact zetu.

Sisi tunafanya kazi kwa Australia pekee kwa sasa na tuna mikataba na baadhi ya institutions hapa Australia kama TAFE (TAFE ni kama VETA kwa Tanzania) na universities kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wenye sifa lakini wanashindwa kutokana na sababu mbalimbali.

Yes, tunacharge processing fee lakini ni ile ambayo mwananchi wa kawaida anamudu kulipa. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na kiasi tunachocharge (ambacho kinategemeana na servive itakayotolewa) tafadhali click sehemu imeandikwa contact us kwenye website yetu na afisa mmoja atakujibu mwanzo mwisho!

Kuhusu working VISA, kampuni yetu haishughulikii lakini ushauri wa bure unatolewa pale mteja atakapoeleza shida yake.

Ushauri wa bure pia unatolewa kwa wale wanafunzi wanaotaka kuapply wenyewe scholarships mbalimbali.

Hope nimeeleweka lakini ukiwa na swali ama dukuduku andika tena tulonge.

Salaam

IBSCS

Sawa sawa pia kuna ile Skilled migration mna-link yeyote na organisation kama hiyo yenu kwa upande wa Oz?
 
Okay, hizo link mbili zitakupa mwanga wa scholarship ipi unaweza kuapply. Tip: scholarships nyingi zinatolewa kwenye research degrees na siyo taught.

Mkuu kwenye s/ship nadhani hauko sawa. Kwa mfumo wa Tz hatuna bachelor honours (hons kwa maana ya Oz education). So kwenda kupiga masters by researche labda upige mwaka mmoja kwanza baada ya bachelor(ku-qualify hons) ndipo upate
 
Sawa sawa pia kuna ile Skilled migration mna-link yeyote na organisation kama hiyo yenu kwa upande wa Oz?

Hapana mkuu, hatuna link na organisation yoyote ile kwenye mambo ya skilled immigration! Lakini skilled immigration unaweza kuapply mwenyewe kokote ulipo sababu mambo yao yote unafanya online. Of course wapo ma-agenti lakini wanacharge fedha kubwa sana (ila kwa mtu mwenye uwezo wa kifedha si mbaya akawatumia kupunguza kuhangaika)

Pitia hii link na kama unaswali we uliza Working in Australia
 
Mkuu kwenye s/ship nadhani hauko sawa. Kwa mfumo wa Tz hatuna bachelor honours (hons kwa maana ya Oz education). So kwenda kupiga masters by researche labda upige mwaka mmoja kwanza baada ya bachelor(ku-qualify hons) ndipo upate

Sijakuelewa, unaweza kufafanua kidogo? Kwa nini uapply scholarship inayohitaji honors bachelor degree wakati wewe huna hiyo degree! Unapply unayoqualify na kuna watanzania wengi tu wanasoma na wengine wamemaliza masters za research na taught pia.
 
Back
Top Bottom