Unapopita maeneo ya kambi ya Jeshi!!

Unapopita maeneo ya kambi ya Jeshi!!

chakii

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Posts
21,683
Reaction score
28,908
Habari zenu wakuu,..

Mara nyingi nimekuwa nikikatiza maeneo ya jeshi ninapoelekea mjini au ninaporudi nyumbani,.

Wakati ninapoingia maeneo haya ya jeshi mtandao au network ya simu yangu ya mkononi huwa inasumbua sana lakini tukishapita eneo hili la kambi ya Jeshi mtandao hurejea tena hewani kama kawaida!!

Kwa wenye uelewa wa hii hali tafadhali tujuzeni hii hali inasababishwa na kitu gani!!

Eneo nilipoiona hii hali ni kambi ya Jeshi LUGALO MILLITARY BASE!!!
 
Kama umesha jua hapo ntwk haishiki sasa wataka kujua nini tena zaidi ya hilo? Kwani lazima upige cm ukiwa hapo? Unataka ujue halafu iweje?
 
aroooo mura unataka kujua siri za jeshi ili iweje?
 
Kama umesha jua hapo ntwk haishiki sasa wataka kujua nini tena zaidi ya hilo? Kwani lazima upige cm ukiwa hapo? Unataka ujue halafu iweje?

siyo vibaya kufahamu mkuu!! Hakuna dhambi ya kujua hali hiyo inasababishwa na nini,. Kama hujui basi tusubirie wanaojua waje kutufahamisha,..
 
mimi nikiwa kwangu network haifanyi kazi kwa hiyo hapa ni kambi ya jeshi

sina maana hiyo mkuu, hii hali inatokea sana maeneo ya jeshi na ni wakati wote utakaokuwa unakatiza maeneo hayo!!
 
Ni coincidence tu mkuu

hapana kaka, hii hali inatokea kila wakati!! Kama upo dar jaribu kupita maeneo haya alafu uje hapa kutupatia mrejesho mkuu,..
 
Electronics jamming device at work

mkuu huenda point yako ikawa ya msingi sana ila lugha uliyoitumia inawapiga chenga watu wengi, hasa sisi wa kayumba Big Results Now!!
 
Habari zenu wakuu,..

Mara nyingi nimekuwa nikikatiza maeneo ya jeshi ninapoelekea mjini au ninaporudi nyumbani,.

Wakati ninapoingia maeneo haya ya jeshi mtandao au network ya simu yangu ya mkononi huwa inasumbua sana lakini tukishapita eneo hili la kambi ya Jeshi mtandao hurejea tena hewani kama kawaida!!

Kwa wenye uelewa wa hii hali tafadhali tujuzeni hii hali inasababishwa na kitu gani!!

Eneo nilipoiona hii hali ni kambi ya Jeshi LUGALO MILLITARY BASE!!!

JIBU MASWALI HAYA MARA MOJA:

1:Unataka kujua kinacho sababisha ili ufanye nini?

2: Je ni lazima upige simu ukiwa eneo hilo tu au waweza kupiga simu kabla ya kufika eneo hilo na baada ya kupita hilo eneo?

3: Je ulisha wahi kuwauliza wakazi wa eneo hilo (Wanajeshi) kuhusu jambo hilo na walikujibu nini?

Namalizia kwa kusema - Huna uzalendo na nchi yako, mtandao huu unapitiwa na watu wa aina tofauti na wenye nia tofauti na nchi yako, sasa wewe unataka kutoa siri za Jeshi lako hapa Jamvini?

Back
Top Bottom