Unapendelea kula nini?

EMT

Platinum Member
Joined
Jan 13, 2010
Posts
14,477
Reaction score
15,357
Utafiti uliofanywa na Oxfam unaonyesha kuwa Watanzania tunapendelea zaidi kula ndizi na nyama. Ghana wanapendelea fufu na Kenya ugali. Ifuatayo ni orodha ya vyakula vinavyopendwa zaidi kwa asilimia.

1. Ndizi na nyama - 12.9%

2. Wali na nyama - 10.9%

3. Wali na maharage - 9.9%

4. Ugali na nyama - 9.9%

5. Ugali na samaki - 8.8%

6. Ugali na maharage - 5.5%

7. Chipsi na Mayai - 5.5%

8. Ugali na mboga za majani - 4.5%

9. Wali na samaki - 3.6%

10. Wali na dagaa - 3.6%

11. Vyakula vya asili - 3.3%

12. Ugali na mboga mboga asilia - 2.4%

13. Ugali na kuku - 1.9%

14. Wali na kuku - 1.9%

Kwenye list sijaona kitimoto. Unapendelea kula nini?
 
halafu hizi research wamewafanyia watanzania wa masaki na mbezi beach naona

kila mtu anajua wali maharage ndio chakula cha taifa....

kuna nyumba ikipita siku tatu bila wali mandondo

watoto wanaandamana lol
 
Reactions: EMT
halafu hizi research wamewafanyia watanzania wa masaki na mbezi beach naona

kila mtu anajua wali maharage ndio chakula cha taifa....

kuna nyumba ikipita siku tatu bila wali mandondo

watoto wanaandamana lol

Nimeshangaa Wakenya wanapiga ugali zaidi yetu
 
 

Attachments

  • chapati-tanzania.jpg
    36.1 KB · Views: 87

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…