Unapenda mwanao ajue vitu gani?

Unapenda mwanao ajue vitu gani?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,028
Reaction score
168,651
Napenda nimfunze mwanangu upendo,
amjue Mungu, nimfundishe heshima na adabu.
Nimfundishe kazi za mikono, nimfundishe kuwa juhudi na bidii katika kila afanyalo.
Nimfundishe mazingira yanayomzunguka na namna ya kuyafanya yawe bora zaidi.
Je wa kwako unamfundisha nini?

942827_604728659547055_2092594284_n.jpg
 
Napenda nimfunze mwanangu kukua huku akiamini kuwa Dini ndio Silaha tosha.
Nampenda sana mwanangu.
 
Mi mwanangu ningependa ajue matusi. Huu unyonge nilionao mbele ya majirani zangu nisingependa mwanangu awe nao

Baby+Finger.GIF
 
Nitajitaidi kwa hudi na uvumba kumfunza mwanangu mambo ya msingi ambayo naamini yatamsaidia katika maisha yake ya baadae. Ningemfundisha kuwaheshimu wakubwa zake na hata rika lake.

Sitoacha kumkemua mwanangu pindi nionapo anaenda njia isiyo sahihi.

Nisingependa mwanangu ajihusishe na tabia ambazo baadae zingemuharibia mfumo wa maisha yake, au kumuathiri kiafya hata kiakili.
Master nyeto.gif
 
Wanangu nawafundisha Upendo kwa Mungu na kwa watu wote. Napenda wamjue Mungu na kutekeleza yale mema aliyotuamuru kuyatenda na kuyaacha mabaya (dhambi) aliyotukataza.

Nawafundisha wanangu wazijue haki zao na kutimiza wajibu wao.

Pia napenda watoto wangu wakue wakiwa na uthubutu na wasiwe watu wa kukata tamaa!
 
Kuthamini utu kuliko vitu
kuwa positive on just about everything and everyone
kumuamini Mungu lakini na kujua manna dont fall anymore. Go through the clouds and grab. Upandacho ndo uvunacho.
Namfundisha mengi lakini nakuwa mfano pia!
 
Back
Top Bottom